Dhana ya utiifu na uasi (Walaa na B...

Egypt's Dar Al-Ifta

Dhana ya utiifu na uasi (Walaa na Bara'a)

Question

Ni nini dhana ya utiifu na uasi, na kwa namna gani makundi ya kigaidi yalitumia dhana hii kwa kueneza ugaidi?

Answer

Kwa kuangalia vitabu vya Maimamu wa zamani wa mwanzo na waliokuja baada yao hatupati kuona istilahi hiyo ya utiifu na uasi (Walaa na Bara'a), kwa kuwa ni istilahi mpya iliyobunuliwa na baadhi ya watu kwa kuashiria upendo na chuki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wakadai kuwa zipo dalili katika Qur'ani na Sunna zinazoeleza hali hiyo, ambapo kutokana na  Qur'ani Tukufu kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Utawaona wengi wao wanafanya urafiki na waliokufuru. Hakika ni maovu yaliyo tangulizwa na nafsi zao hata Mwenyezi Mungu amewakasirikia} [Al-Maidah: 80], kuchukua maana yake kumpenda na kujikurubia kwake, kinyume na kujitenga ambayo maana yake chuki na uadui, isitoshe, magaidi walitumia istilahi hiyo wakaichanganya na asili ya itikadi na Imani, hasa katika maana ya tamko la hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee, na kubuni itikadi iitwayo itikadi ya walaa na baraa wakiiongeza kuwa sharti ya Imani sahihi kwa kusema kuwa kutokuwa na itikadi hii kwa Muislamu humgeuza kuwa kafiri kwa dalili ya kauli ya Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao} [Al-Maidah: 51], kwa namna hii, wakawa na fikra mpya kama vile; kumpenda mtu awe Muislamu au si Muislamu lakini anafuata fikra hizo hizo zinazoambatana na fikra zao wakikufuru kwa Mwenyezi Mungu!

Share this:

Related Fatwas