Damu ya hedhi kutokwenda sawa kwa s...

Egypt's Dar Al-Ifta

Damu ya hedhi kutokwenda sawa kwa sababu ya maradhi

Question

Mwanamke mgonjwa na anatibiwa kwa njia ya dozi za kemia, kwa sababu hiyo masiku ya hedhi yake hayaendi kwa mpangilio basi ni namna gani atahesabu siku zake?

Answer

Mwanamke ikiwa ataona damu kabla ya kupita siku kumi za utwahara wake kutokana na hedhi yake iliyopita, basi damu hii inakuwa ni damu ya istihadha, ama ikiwa ataona na zikawa zimepita siku kumi au zaidi, basi hiyo ni damu ya hedhi ikiwa ni ya siku tatu au zaidi madamu haijavuka siku kumi na wala haikuwa ni kawaida yake, ikiwa zitapungua siku tatu basi hiyo itakuwa ni damu ya Istihadha, ikiwa itavuka siku kumi, ikiwa ni kawaida yake inayofahamika ni chini ya siku kumi basi itarudishwa kwenye kawaida yake, nayo ni damu ya Istihadha, na wakati huo atalazimika kulipia ibada za swala zilizompita kwa siku zilizozidi kawaida yake, ikiwa hana kawaida inayofahamika basi hurudishwa zaidi siku za hedhi nazo ni siku kumi, na zitakazozidia ni damu za Istihadha, ataoga baada ya kupita siku kumi, ama akiendelea kutoa damu, basi itazingatiwa ni kawaida yake kila mwezi na kuwa ndio hedhi yake, na masiku yaliyobaki katika mwezi zinakuwa ni siku za twahara madamu anafahamu kawaida yake na idadi ya masiku yake, na anafahamu mwanzo wake na mwisho wake, ikiwa hana kawaida, zitarudishwa siku nyingni zaidi za hedhi nazo ni siku kumi, hivyo hedhi yake itakuwa kiasi cha siku kumi, na siku zitakazozidi hiyo ni damu ya Istihadha, wakati inapothibiti ni damu ya Istihadha: Ni halali kwake kila kilichoharamu kwa sababu ya damu ya hedhi ikiwa ni pamoja na ibada ya swala funga na mfano wake baada ya kuoga hedhi, ifahamike kuwa makisio haya ni maalum kwa hukumu za ibada za swala funga na mfano wake, na wala si kwa hukumu za eda.

Share this:

Related Fatwas