Sala ya Adhuhuri Baada ya Sala ya Ijumaa
Question
Nini hukumu ya sala ya adhuhuri kwa mujibu wa madhehebu ya Imamu Shafi, baada ya sala ya Ijumaa pindi masharti ya sala ya Ijumaa yatakapokuwa yametimia katika eneo ambalo idadi ya watu wake haifikii idadi inayohitajika, kwani sisi – huku – Chechnya tunafuata madhehebu ya Imamu Shafi na wala hakuna madhehebu mengine?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
katika mambo yenye kujulikana kisheria ni kuwa, malengo ya kusimamisha swala ya Ijumaa ni kuonesha hali ya mkusanyiko wa waislamu katika ibada na kwamba wao ni wamoja katika neno lao, kwa ajili hiyo, wanazuoni wameweka sharti la kusihi kwa swala ya Ijumaa kwamaba isitanguliwe na wala isiswaliwe sambamba na Ijumaa nyengine katika mji mmoja isipokuwa kama mji huo utakuwa mkubwa, na ikawa watu hawawezi kukusanyika sehemu moja isipokuwa kwa tabu. Hapo itafaa kuswaliwa swala ya Ijumaa zaidi ya moja kwa sababu ya haja iliyopo. Na Imamu Shafi juu ya swala hilo ana kauli mbili: Kauli yenye nguvu kati ya hizo – na yenye kutegemewa – ni kuwa inafaa kuswali swala ya Ijumaa zaidi ya moja kwa mujibu wa haja. Na imesemwa: Haifai kuswali swala ya Ijumaa zaidi ya moja hata kama kuna haja, na wakaeleza kwa mapana hali ya kuchunga hitilafu, na kwa kauli yenye nguvu, ni ile inayosema, inapendeza kwa aliyeswali Ijumaa pamoja na kuwa zimeswaliwa zaidi ya moja kwa mujibu wa haja na wala hakuelewa kuwa swala yake ya Ijumaa imetanguliwa na Ijumaa nyingine kuwa airudie kwa kuswali adhuhuri kama ni akiba ili asiingie katika hitilafu.
Na kwa upande wa madhehebu ya Abu hanifa wao wanaruhusu – kwa kauli yenye kuzingatiwa – kuwa itaswaliwa swala ya Ijumaa katika mji mmoja katika maeneo mengi, kama alivyotaja imamu As sarkhasiy kuwa hivi ndivyo sahihi kwa upande wa madhehebu ya Abi Hanifa –radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie-.
Na katika hayo tunaelewa haya yafuatayo:-
• Katika sharti za kusihi kwa swala ya Ijumaa kwa upande wa wanazuoni ni kutotanguliwa au kutosaliwa sambamba na sala ya Ijumaa nyengine katika mji mmoja isipokuwa kwa haja.
• Inafaa kuwepo kwa swala ya Ijumaa zaidi ya moja pindi haja imepelekea hivyo, kama kutokuwepo kwa maeneo ya kutosha au kuna ugumu wa kukusanyika (sehemu moja).
• Inapendezwa kiakiba au kutoingia katika hitilafu kwa wale wanaosema kuwa haijuzu kuwepo kwa swala ya ijumaa zaidi ya moja hata kama kuna haja aiswali tena (kwa kusali) adhuhuri, pindi iwapo hana uhakika kuwa aliyeswali Ijumaa kama swala yake ya Ijumaa ndiyo iliyotangulia au kuwa haikwenda sambamba na Ijumaa nyingine. Na kuswali huku kiakiba kumewekwa kama ni jambo lenye kupendeza na sio jambo la lazima.
Na kwa mujibu wa swali: Kuiswali tena swala ya Ijumaa kwa kuswali adhuhuri baada yake kwa waliosema hivyo, hii ni kwa njia ya kupendezesha na sio kwamba ni lazima. Kwani hakuna yeyote mwenye kupinga jambo hilo, na pia ni kwa kulifanya jepesi jambo hilo kama walivyofanya waliotangulia katika watu wema na waliochunga heshima katika hilitafu zao na ambao walikuwa ni mwongozo katika maswala ya hitilafu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote