Ombi la Talaka Katika Mahakama ya Marekani, Mume Anapogoma Kutoa Fedha za Matumizi.
Question
Ni ipi hukumu ya Sheria kwa mwanamke mwislamu anayeishi Marekani ambako hakuna Kadhi mwislamu au anayeaminiwa katika kutatua tatizo lake? Mwanamke huyu amekuwa akimdai mume wake talaka kwa muda wa mwaka mmoja, mume ambaye hakuwahi kutoa fedha za matumizi katika kipindi chote cha ndoa isipokuwa miezi mine tu. Mume huyo alilipa kodi ya nyumba tu, na mwanamke ndiye aliyelipa gharama za kuhama kwake, masomo yake katika nchi yake mwanamke, gharama za chakula chake na nguo zake. Mwanachuoni mmoja alimwambia mwanamke kuwa yeye lazima amsaidie mumewe katika kukamilisha taratibu za uhamiaji, ikiwa hakufanya hivyo itazingatiwa ndoa yao ni uasi. Na kwa sasa mume amemwacha mke tangu miezi saba iliyopita bila ya fedha za matumizi, na mwanamke hajui mumewe alipo. Je inajuzu kwa mwanamke kutegemea hukumu ya mahakama ya Marekani kuhusu talaka yake?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Inawezakana kwa mwanamke huyu kuomba talaka mahakamani nchini Marekani, ili mume asiwe na haki kwa upande wa kisheria, kisha hukumu hii haitekelezwi juu ya Sheria ya dini, lakini kwa kuwa hakuwepo kadhi mwislamu, basi upande wa mwanamke unaweza kuivunja ndoa bila ya kuwepo haja ya kurejea kwa mumewe; kwa sababu wanachuoni wa madhehebu ya Shafiy walijuzisha mwanamke aivunje ndoa yeye mwenyewe katika hali ya kutokuwepo fedha za matumizi kwa upande wa mume, ikiwa mwanamke hakukuta kadhi mwislamu wa kuvunja mkataba wa ndoa.
Uvunjaji huu wa ndoa hauambatani na hukumu ya mahakama ya Kimarekani wala nyinginezo wala kufungamana nayo, lakini inakuwa ni kurejea mahakama za Kimarekani na nyinginezo katika nchi zisizo za kiislamu ni kwa lengo la kuhifadhi haki na utulivu katika jamii.
Ama kuhusu uhuru wake wa kuvunja ndoa, unatekelezwa kidini, ikiwa hakutokuwepo kadhi mwislamu au hakimu kati ya mwanamume na mwanamke wanaoweza kukubali hukumu yake, bila ya kuunganisha kati ya kuvunja ndoa na hukumu ya mahakama ya nchi zisizo na kadhi mwislamu, kwa mujibu wa madhehebu ya Shafiy, na kauli moja kutoka kwa madhehebu ya Hanbali.
Wanachuoni wa madhehebu ya Shafi walipothibitisha kuvunja ndoa kutokana na ugumu wa kumgharimia mke kwa upande wa mume, walitaja rai mbili katika uhuru wa mke kuvunja ndoa. Al-Mtawali alitaja rai moja kuwa: Mwanamke ana haki ya kuvunja ndoa peke yake pamoja na kuwepo kadhi mwislamu, na kuwa rai sahihi ni: Mwanamke hawezi kufanya hivyo peke yake, hasa kwa kuwepo kadhi au hakimu mahali hapa, na hata hivyo mwanamke akivunja ndoa kwa upande wake tu, basi tendo linatekelezwa Kiundani tu, na hayo yote ni wakati wa kuwepo kadhi au hakimu, lakini wakati wa kutokuwepo rai yao kuwa: Ana haki ya kuvunja ndoa peke yeke.
Kisha waliongeza suala la kukataa mume kugharamia mke hali anao uwezo, wakataja rai mbili katika madhehebu, kwanza: Mwanamke ana haki ya kuvunja ndoa kwa kupata udhuru, na rai hii ni ya Kadhi Attabari na Ibn As-Sabbagh, Ar-Rauyaniy na wengineo walitaja kuwa fatwa kwa rai hii ni masilahi.
Lakini rai sahihi ya hizi mbili ni: Hakuna kuvunja kwa sababu mwanamke anaweza kupata haki yake kwa njia ya kadhi.
Haifichikani kuwa hukumu hii inatekelezwa kwa kuwepo kadhi mwislamu ambaye anaweza kumpa mwanamke haki yake inayoamuliwa na sheria, lakini wakati wa kutokuwepo kadhi, basi inajuzu kwa mwanamke peke yeke kuivunja ndoa, kama alivyosema Imamu Al-Ghazali katika kitabu chake (“Al-Basiit), kwa ajili ya kuepusha madhara anayopata kutokana na ndoa isiyo na gharama, na hawezi kuzipata.
Kisha katika suala la kumpa fursa mume ili kugharamia mwanamke kuna rai mbili: Baadhi ya wanachuoni wanasema: Apewe muda wa siku tatu endapo atashindwa kumgharamia mwanamke, na mwishoni mwa muda mke ana haki ya kuvunja, na wengine wanasema: Mwanamke ana haki ya kuvunja bila ya kumpa mume fursa.
Na haifichikani kuwa fatwa ni kutokana na hali ilivyokuja katika swali, ambapo swali ni: Mume hagharamii mkewe tangu zaidi ya miezi minane, bali mwanamke ndiye alikuwa akimgahrimia, na kwamba hakuwepo kadhi mwislamu, na alipokwenda kwa washauri kuhusu talaka yake wanataka kumlazimisha amsaidie mume, isije ikawa ni maasi, na mume halali nyumbani kwa mke tangu miezi saba iliyopita, na mwanamke hajui alipo mumewe. Hayo yote yanajuzisha kwa mwanamke peke yake kuvunja ndoa kwa yakini kwa rai ya wanachuoni wa madhehebu ya Shafiy, na wakati wa kuwepo au kutokuwepo kwake.
Ama kusimama katika fatwa kwa ajili ya mke ni kwa kudhani kuwa mumewe asiyejulikana alipo kwa muda wa miezi saba anafikiri kuwa mwanamke ni asi, au kwa kudhani yeye ni bahili, au mume anataka kumtesa pamoja na uwezo wake wa kugharimia, hayo yote ni miongoni mwa madaraka ya kadhi ambapo anaweza kuchunguza kwa maneno yao kwa dalili na mashahidi, na hayo si miongoni mwa madaraka ya Mufti ambaye anafikiri kuwa hali ni kama ilivyokuja katika swali, na hali ya kweli kuwa: Kutokuwepo kadhi mwislamu, au hakimu mwislamu ambapo mwanamke anamwamini na anajitahidi kwa ajili ya kumpatia haki yake.
Imam An-Nawawiy katika kitabu cha (Raudatu-Talibiin) anasema: “Mlango wa tatu: katika ugumu wa kugharamia mke, kuna pande nne: Upande wa kwanza: Katika kuthibitisha kuvunjwa kwa ajili yake: Mume akishindwa kuleta mahitaji ya mke anayemhudumuia, basi Shafi R.A, alitaja katika vitabu vyake vya zamani na vipya kuwa: Ni hiyari ya mwanamke: Akitaka anasubiri na anajigharamia kwa mali yake, au kukopa na kujigharamia nafsi yake, na gharama hii ni kama deni juu ya mume mpaka atakapokuwa na uwezo, na akitaka ataomba kuvunja ndoa.
Na amesema katika baadhi ya vitabu vyake baada ya kutaja hivi kuwa: Imesemekana mwanamke hana hiyari.
Wanachuoni wana rai mbili, ya kwanza: Kuhakikisha kuwa mwanamke ana hiari ya kuvunja ndoa, na hii ni rai yenye nguvu zaidi kwa Ibn Kajj na Ar-Rauyaniy, pia kuna rai mbili zenye usahihi, moja ni mashuhuri ya kuwa: Ana haki ya kuvunja, na ya pili: Hana haki. Kwa hiyo madhehebu sahihi ni kuthibitisha kuvunjwa.
Ama kuhusu suala la kukataa kugharamia pamoja na kuwepo uwezo, kuna rai mbili, ya kwanza: Ana haki ya kuvunja kwa ajili ya kupata madhara, na rai yenye usahihi zaidi ni: Hakuna kuvunja, kutokana na kuweza kupata haki yake kwa njia ya kadhi. Vile vile mwanamke akiweza kupata kiasi kutokana na mali yake, au ametoweka na ana uwezo wa mali wala hatoi haki ya mke, basi kuna hukumu mbili zilizotangulia, na hukumu yenye usahihi zaidi ni: Hakuna kuvunjwa, na sababu ni kutoweka kwake na uharibifu wa dhima yake, lakini hakimu wa nchi yake atamtuma kwa hakimu wa nchi aliopo mume na kumwamuru kulipa ikiwa mahali pake panajulikana. Hukumu nyingine; inajuzu kuvunjwa ikiwa ni tabu kupata haki yake, na hii ni rai ya Kadhi At-Tabariy na Ibn As-Sabbagh; Ar-Rauyaniy na wengineo walitaja kuwa: fatwa kwa rai hii ni masilahi.
Tusipojuzisha kuvunjwa wakati mwenye kutoweka ni mwenye uwezo wa mali, basi tunajalia uwezo wake wa mali na kutokuwa kwake na mali, basi na hukumu mfano wake, kwa kuwa sababu haikuthibiti.
Upande wa pili: Hakika kuachana huku: Ikithibiti haki ya kuachana kwa sababu ya ugumu wa kutokuwa na mali, basi ni lazima kufikisha dai mbele ya kadhi kwa sababu yeye ni mwenye mwenyekujitahidi (Mwanachuoni). Al-Mutawalliy na wengineo walitaja rai nyingine kuwa: Mwanamke ana haki ya kuvunja ndoa peke yake na bila haja ya kufikisha dai mbele ya kadhi, mfano wa kuvunja bei ya kilichouzwa chenye kasoro, na rai sahihi hapa ni ya kwanza, na wanachuoni wengi waliitekeleza. Kwa hiyo kadhi mwenyewe atavunja ndoa au kumpa mwanamke idhini ya kuvunja, na kadhi ana hiyari katika mawili hayo na imesemekana kuwa: Kuvunja ni ujumbe wake tu baada ya kuthibiti ugumu wa kugharamia, lakini ya kwanza ni sahihi.
Itakuwa kuachana huku ni kuvunja ndoa kwa andiko sahihi, kwa rai nyingine ni talaka, kwa hiyo hakimu atamwamuru mume agharamie, na mume akikataa basi je hakimu mwenyewe amwachishe au atamfunga mume ili amwachishe? Zipo rai hizi mbili, akimwachisha basi hii ni talaka ya kwanza, talaka rejea, basi akirejea atakuwa na haki ya talaka ya pili na ya tatu.
Mwanamke asipofikisha dai mbele ya kadhi, bali mwenyewe alivunja ndoa kutokana na mume kushindwa, basi kuvunja huku hakutekelezwi kidhahiri, na je kutatekelezwa kindani? Hata ukithibitishwa ugumu wake kabla ya kuvunja –ikiwa kwa kukiri kwa mume au kwa dalili- je hiki kilitosha na eda itahesabiwi kwake? Kuna rai mbili:
Alisema katika kitabu cha Al-Basiit: Hii ni katika hali ikiweza kufikisha dai mbele ya kadhi, lakini ikiwa hapatakuwa na kadhi au hakimu mahali hapa, basi rai ni kuthibiti uhuru wa kuvunja (ni haki yake mwenyewe).
Upande wa tatu: Katika wakati wa kuvunja: Ilivyotangulia kuwa mke ana haki ya kupata gharama yake kila siku ichomozapo Alfajiri, lakini mume asipoweza, je kuvunja kutatekelezwa upesi au hupewa muhula wa siku tatu? Kuna rai mbili: Iliyo wazi miongoni mwake: Ni kumpa muhula, kama walivyosisitiza baadhi ya wanachuoni, na Ibn Kajj alidai kuwa hii ni rai ya wengi wa wanachuoni.
Tukisema: Hapewi muhula wa siku tatu, basi kuna rai mbili: Ya kwanza: Mwanamke ana haki ya kuvunja haraka mwanzoni mwa mchana, pili: Hana haki ya kuvunja haraka, kwa hiyo je kuvunjwa kutaahirishwa mpaka nusu ya mchana, au mwishoni mwa mchana, au mwishoni mwa usiku baada yake? Kuna rai mbali mbali, iliyo na nguvu zaidi ni ya tatu, kama alivyotaja Ghazali, na rai hii inatekelezwa, ikiwa hakuna mazoea, lakini pakiwa na mazoea ya kuleta chakula usiku, basi ana haki ya kuvunja. [Mwisho].
Mwanachuoni Al-Mardawi mfuasi wa madhehebu ya Hanbaliy amesema; katika mlango wa (mahari kutoka kitabu cha (Al-Insaaf): “Kauli yake (haijuzu kuvunja isipokuwa kwa hukumu ya hakimu) ndiyo madhebu inayotambuliwa, na wanachuoni wengi waliitambua, na wakaisisitiza. Na imesemekana kuwa: Hakuhitaji hukumu ya hakimu, mfano wa kukhiari kwa mjakazi ailiyetolewa huru wakati akiwa chini ya mtumwa”. [Mwisho].
Pia amesema katika mlango wa (Gharama): “Kauli yake (haijuzu kuvunja isipokuwa kwa hukumu ya hakimu) na ndiyo madhehebu yake, na ni kauli ya wengi. Mtungaji, Mwenye Sherehe, mwenye maelezo, na wengineo walitaja katika kitabu cha (Mahari): Mwanamke ana haki ya kuvunja ndoa bila ya hukumu ya hakimu, kama mume akiwa na ugumu wa kulipa mahari”.[Mwisho].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.