Kuvunja Ahadi na Kumtusi Mke

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuvunja Ahadi na Kumtusi Mke

Question

 Mimi ni mwanamke wa kutoka Marekani na nilisilimu na kufuata Uislamu wa kweli, na nimeolewa na Mwislamu kutoka Jordon na ndoa yetu ilifanyika kwenye Mskiti wa Chicago nchini Marikani, lakini mume wangu hakuwa mwaminifu nami na akavunja ahadi zetu zote, tukiwa nyumbani, mume wangu amekuwa na tabia ya kunitukana mimi pamoja na watoto wetu. Na amekuwa akifanya hivyo mara nyingi. Vile vile amekuwa akieneza maelezo ya maisha yetu binafsi katika majarida mbali mbali na kuyaeleza makosa yangu. Nini hukumu ya Sheria ya Uislamu kuhusu jambo hili?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uislamu umewaamuru Waislamu watimize ahadi. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Enyi mlio amini! Timizeni ahadi.} [AL MAIDAH : 1], Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W anasema pia: “Waislamu wanatimiza masharti isipokuwa sharti linaloharamisha jambo la halali au sharti linalohalilisha jambo la haramu”. [Imepokelewa kutoka kwa Tirmidhi.]
Tena Mtume S.A.W. akaweka wazi kuwa masharti yaliyo muhimu zaidi kutekelezwa ni yale ya ndoa, kwa kumheshimu mke na kuzilinda haki zake. Mtume Anasema: “Hakika masharti yanayopaswa kutimizwa ni masharti ya mke”. Na mtazamo sahihi kuhusu masharti ya mke ni kwamba kila sharti lenye manufaa kwa mke na halipingani na asili ya mkataba, basi sharti hilo ni la kutelekezwa na mume kwa lazima. Miongoni mwa masharti hayo ni Makazi ya mke. Kama mume atavunja ahadi hii, basi mke ana haki ya kuvunja ndoa na atachukua haki zake zote. Imam Ibn Qudamah anasema katika kitabu chake: [Al-Mughni] kuwa: Kama atamwoa na akamwekea sharti la kutooa mwanamke mwingine, basi mke ana haki ya kuvunja ndoa kama mume ataoa mwanamke mwingine. Muhtasari wa hayo ni kwamba: Masharti katika ndoa yana migawanyiko mitatu: Mgawanyiko wa kwanza ni masharti ya kutekelezwa kwa lazima, nayo ni yale yaliyo na manufaa kwa mke, kama vile mume akitaja sharti kuwa hatamtoa mke wake nje ya nyumba yake, au ya nchi yake, au hatasafiri pamoja naye, au hatamwoa mwanamke mwingine, au hatamficha siri yeyote, basi masharti haya yote ni ya kutekelezwa kwa lazima, na kama mume hatayatimiza masharti haya basi mke atakuwa na haki ya kuvunja ndoa.
Mtazamo huu umepokewa kutoka kwa Omar Ibn Khattab R.A, Saad Ibn Abi Waqqas, Muawiyah, na Amru Ibn Al-As R.A. Vile vile Shuraih, Omar Ibn Abdul Aziz, Jabir Ibn Zaid, Tawus, Al-Awzai, na Is-haq wote waliafikiana na mtazamo huo. Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: “Masharti yenye haki zaidi kuyatekeleza ni yale yanayofungamana na ndoa” Hadithi hii Imepokelewa na Said. Vile vile Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: “Waislamu wanatimiza masharti yao”, kwani Maswahaba waliotajwa hapo juu waliafikiana kuhusu mtazamo huu, basi hayo ni makubaliano kati ya Maswahaba.
Imepokelewa kutoka kwa Athram kuwa mtu mmoja alimwoa mke na akataja sharti la kumpa makazi yake, kisha akataka kumgeuzia nyumba nyingine, watu wakamshitaki mtu huyu kwa Omar, Omar akasema kuwa sharti hili ni haki ya mke. Mtu yule akasema basi tuvunje ndoa, Omar akasema kulitekeleza sharti hili ni jambo la lazima. Na kwa sababu sharti hili lina manufaa kwa mke basi ni lazima litekelezwe, pia kama mke atataja sharti la kuongeza mahari au kulipa pesa zisizo za kigeni”.
Kutokana na hayo yaliyotangulia hapo juu, kila yaliyotajwa katika swali hili ambayo ni pamoja na kuvunja ahadi, kuwatusi watoto, na kueneza maelezo ya maisha ya ndoa katika vyombo vya habari, hayo yote ni haramu kwa mujibu wa Sheria ya Kiislamu na yanapingana na mafunzo ya Uislamu yanayokataza dhuluma, mashitaka kinyume cha sheria, na kupindukia mipaka wakati wa kugombana, bali baadhi ya makosa hayo ni miongoni mwa madhambi makubwa ambayo hayahusiani na Uislamu kwa karibu au kwa mbali, na hayana uhusiano wowote na mafunzo yake matukufu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas