Kufanya arobaini na kumbukumbu ya m...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufanya arobaini na kumbukumbu ya mwaka.

Question

Ipi hukumu ya kumbukumbu ya siku ya arobaini na mwaka kwa maiti?

Answer

Wanachuoni wameelezea muda wa matanga ni siku tatu tu, na matanga baada ya hizo siku tatu ni jambo linalochukiza, isipokuwa kwa ambaye hakuwepo kisha akafika, au kwa asiyejua hali ya kifo isipokuwa akafahamu baada ya kupita muda, hii ni kutokana na uwezekano wa kurudisha tena majonzi na kuwalazimisha ndugu wa marehemu wasichokiweza.

Kisharia hakuna kizuizi cha kukusanyika ili kumpatia thawabu kwa kufanya matendo mema kwa maslahi ya maiti, kama vile kulisha chakula kusoma Qurani ni sawa sawa siku ya arobaini au mwaka.

Share this:

Related Fatwas