Kujenga ardhi ya kilimo bila kibali...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kujenga ardhi ya kilimo bila kibali.

Question

Je, ni ipi hukumu ya kujenga ardhi ya kilimo bila kibali?

Answer

Kujenga ardhi ya kilimo bila kibali hairuhusiwi kwa mujibu wa Sharia. Kwa sababu hii inapelekea madhara makubwa, na ni kinyume cha dhamira ya Sharia, ambayo ilihimiza kupanda na kulima. Katika Sahih mbili, imepokelewa kutoka kwa Anas Ibn Malik, (R.A), amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) Amesema: “Hakuna muislamu yoyote anayepanda mazao fulani, au mti fulani alafu akatokea ndege au mnyama yoyote akala kutokana na zao hilo inakua ni sadaka yake mtu huyo.”

Ardhi ya kilimo ndio tegemeo kuu la uchumi wa Misri, na kujenga juu yake ni upotevu wa wazi wa utajiri wa kilimo nchini Misri. Kuweka mbele maslahi ya kikundi na kutilia maanani matokeo yake kunahitaji kufahamu ufisadi unaoweza kusababishwa na upole katika kujenga ardhi ya kilimo na kudhoofisha athari za hali hii kwa uchumi wa taifa.

Share this:

Related Fatwas