Kutumia dawa zilizo na Gelatin
Question
Ni ipi hukumu ya kutumia dawa zilizo na mada ya Gelatin?
Answer
Ikiwa hiyo mada ya Gelatin inatokana na mnyama halali anayeruhusiwa kuliwa, basi hakuna pingamizi lolote kisheria kutumia dawa hii, lakini ikiwa Gelatin inatokana na mnyama asiyeruhusiwa kuliwa au asiyeruhusiwa kuchinjwa, basi ikiwa mada hii imebadilika na kugeuka kutoka hali kwa nyingine kwa sababu ya kusagwa katika kutengeneza dawa na kuchanganywa na kimekali na mada nyinginezo, mpaka kutoweka kabisa na kutokuwa na athari yoyote, hapo ndipo hakuna pingamizi lolote la kisharia kutumia dawa ya aina hii, lakini kwa kuzingatia ushauri wa tabibu mwenye uzoefu wa kutosha kuhusu kutumia dawa ya aina hiyo.