Kusherehekea Siku ya kuzaliwa

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusherehekea Siku ya kuzaliwa

Question

Je, sherehe za siku ya kuzaliwa ni halali au haramu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hakuna kizuizi chochote cha kisheria cha kufanya hivyo, kwa sababu ni kwa njia ya kuikumbuka neema ya Mwenyezi Mungu ya kumuumba binadamu, na hii haipingani na Hadithi ya Mtume S.A.W, ambayo aliipokea Abu-dawuud katika kitabu chake, kutoka kwa Anas bin Malik R.A, kuwa: Mtume S.A.W alikuja Madinah, akawakuta watu wana siku mbili za kucheza, akasema; siku hizi mbili ni za nini? Wakasema: Tulikuwa tukicheza ndani ya siku hizi wakati wa ujahili, na hapo Mtume S.A.W akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amekupeni siku mbili zilizo bora zaidi kuliko mbili hizi; siku ya Adh-ha na siku ya Fitri", kwa hiyo waislamu hawana sikukuu zingine ila hizi mbili: Fitri na Adh-ha (Idi kubwa na Idi ndogo)
Lakini haizuiwi kusherehekea siku ya kuzaliwa au sherehe nyingine yeyote miongoni mwa minasaba maalumu katika maisha ya binadamu, kama vile: siku ya ndoa, siku ya kuzaliwa watoto, au mke, n.k., na ni bora zaidi sherehe hizi zisiitwe sikukuu. Pia inatakiwa wakati wa kufanyika kwa sherehe hizi, kutokuwepo mambo yaliyoharamishwa.
Siku ya kuzaliwa siyo sikukuu kwa maana halisi, lakini ni kushereheka tu kwa siku hii. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu}. [IBRAHIM: 5]. Na miongoni mwa siku za Allah ni siku za kuzaliwa na siku za ushindi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.


 

Share this:

Related Fatwas