Kubadilisha Nasaba Iliyopo Pamoja n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kubadilisha Nasaba Iliyopo Pamoja na Kueleza Ukweli Wake

Question

Mimi ni mwanamke wa kiislamu, nimezaliwa na ninaishi nchini Marekani, na nimekuwa nikikutana na mwanamume wa Kikristo Mmarekani kwa miaka mitatu, na nimebeba ujauzito nje ya ndoa. Aliniahidi kuwa atasilimu na kisha atanioa, kisha akayakwepa maamuzi yake na kukataa, naye hivi sasa anagharamia matumizi ya binti yangu, na sisi tunaamini kuwa anafanya hayo kwa kuwa anaogopa kufunguliwa kesi ya matumizi ya mtoto. Na binti yangu mpaka mwezi januari atatimiza miaka mitatu, na mimi naogopa siku moja baba yake anaweza kufungua kesi na kumchukua mtoto kimalezi, au akapata haki ya kushirikiana nami kwenye malezi. Na mimi sitaki itokee hivyo, kwa sababu yeye ni Mkristo na ni mbaguzi.
Mimi hivi sasa nimeolewa na Mwislamu mshika dini na mtu mwema, na yeye wala hafahamu jambo hili, isipokuwa anachojua ni kuwa mimi niliwahi kuolewa hapo kabla, na mume wangu anataka kumwandika mtoto wangu kwa jina lake yeye pamoja kumlea na kumuhudumia, na tumweleze huyu mtoto kwa wakati sahihi kuwa huyu baba mlezi sio baba yake wa kumzaa, na kwamba mimi niliwahi kuolewa na baba yake lakini hata hivyo tumeachana. Na alikuwa ameingia kwenye Uislamu lakini hata hivyo amerejea kwenye Ukristo, na yote hayo yafanyike kwa ajili ya kulinda na kutoumiza hisia za mtoto wao huyo.
Je inafaa kwa mume wangu kumwandika binti yangu kwa jina lake pamoja na kumweleza ukweli, ili aweze kupata utaifa wa Misri na baba yake mzazi asiwe na haki ya kumlea?
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Sheria hairuhusu kumwita mtoto anaelelewa kwa jina la mlezi wake, ambapo atashirikiana naye katika majina yake kamili, na sura hii yanapatikana makatazo ya sheria, Mola Mtukufu Amesema: {Waiteni kwa (ubini wa) baba zao, maana huo ndiyo uadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu}[AL AHZAAB, 5].
Na yafahamika kuwa Sahaba mtukufu; Zaid Ibn Haaritha alikuwa anaitwa (Zaid Ibn Muhammad) pale alipoitwa na Mtume Muhammad S.A.W. baada ya kuteremshwa amri ya uharamu, jina lake likarudi kama vile lilivyokuwa ambalo ni (Zaid Ibn Haritha).
Kinachofaa ni mtoto kupewa jina la familia ya mlezi wake, ambapo litaonesha kuwa yupo kwenye familia, lakini pasi na kumlaghai kuwa ni mtoto wake au binti yake wa damu, ili isije ingia kwenye wigo wa uharamu kisheria, ila ongezeko ambalo linakuwa mwishoni mwa jina la mtoto yatima au asiefahamika kizazi chake litakuwa ni kama mfano wa uhusiano wa utiifu uliokuwepo kati ya makabila ya zamani ya kiarabu, katika hilo hakuna chochote kinachojengeka na uharamu wa kisheria, kwa sababu mjengeko haramu ni kuongeza mtoto wa mwingine kwake katika mirathi na nasaba pamoja na kupatikana uhalali wa kukaa kwa siri na wanawake wa familia kwa kuzingatia kuwa ni katika walioharamu kwake kuoa, na yasiokuwa hayo, katika yale yaliyokuwa yameenea katika zama za ujinga na zama za mwanzo wa Uislamu, kisha Uislamu ukaharamisha ikiwa ni kuchunga kutochanganya kizazi.
Nasaba hii kwa sifa iliyotajwa ni yenye kuruhusiwa kisheria, na katika maneno ya wafasiri kuna ishara katika hili, mwanachuoni At-twaahir Ibnu A’ashuur ametaja kwenye tafasiri ya kauli Mola Mtukufu: {Waiteni kwa (ubini wa) baba zao, maana huo ndiyo uadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na kama hamuwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika dini na rafiki zenu. Wala si lawama juu yenu katika hayo mliyokosa, isipokuwa katika yale iliyoyafanya mioyo yenu kwa kusudi; na Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mrehemevu}[AL AHZAAB, 5].
Na kusudio la neno (marafiki) katika kauli yake Mwenyezi Mungu pale aliposema {na rafiki zenu} ni urafiki wa kuungana. Angalia kitabu cha: [At-tahrir wa At-Tanwiir, 21/263, chapa ya Tunisia.]
Na akasema mwanachuoni Al-aluusy kauli yake Mola: {Na rafiki zenu} kwa maana ni marafiki zenu – katika dini – waiteni kwa undugu na urafiki katika dini. Na kwa maana hii Saalim aliitwa – baada ya kuteremka aya hii – mtumishi wa Hudhaifa, na alikuwa anaitwa hivyo kabla ya aya.
Na pakasemwa: {Na rafiki zenu} kwa maana ya ndugu kwa baba wadogo, kana kwamba kuwaita hivyo kunapendezesha nyoyo zao, hivyo haikuamrishwa kuwaita kwa majina yao tu.
Na akasema pia: “Na uwazi wa aya unaonesha uharamu wa kukusudia kumwita mtu kwa jina lisilo la babaye, na hilo huenda ndivyo ilivyokuwa katika zama za ujinga, ama kama haikuwa hivyo kama mkubwa anavyomwita mdogo kwa njia ya upole: Ewe mtoto wangu – na wengi wanafanya hivyo – basi uhalisia si haramu kuita hivyo”.
Na katika kitabu cha: [Hawaashy Al-khufaashy tafasiri ya Al-baidhaawy]: mtoto hata kama maelezo yatafaa kuwa kama ndugu, lakini hata hivyo imekatazwa kufananisha na zama za ukafiri, na katazo hapa ni kwa lengo la kuepuka hali hiyo, na huenda halijapokelewa katazo linalomaanisha hivyo kwenye aya iliyotajwa, lakini kinacho katazwa na uharamu ni wito kwa sura ambayo ilikuwepo zama za ujinga” kitabu cha: [Ruuhu Al-Ma’any, 21/148,149, chapa ya Beirut].
Na amesema Imam Ibnu Kathiir katika tafasiri: “Ama kumwita mtu mwengine kuwa mtoto katika njia ya ukaribu na kumpendezesha, basi si katika yaliyokatazwa katika aya hii”, na akatoa dalili nyingi juu ya hilo, miongoni mwazo ni Hadithi iliyopokelewa na Imam Muslim kutoka kwa Anas Ibnu Maalik R.A. amesema: Aliniitaa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. “Ewe mwanangu” [ni tafsiri ya Ibnu Kathiir 6/377 – 378 chapa ya mwaka 1420H].
Na katika Hadithi za Mtume zipo zenye kuonesha hivyo, katika hadithi inayotokana na Anas R.A. amesema: Mtume S.A.W. aliwaita baadhi ya watu wa Madina na kuwauliza: “je kuna yeyote kati yenu asiyekuwa katika nyinyi? Wakasema: hapana, isipokuwa kuna mtoto wa dada yetu, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akasema: mtoto wa dada wa watu ni katika wao”.
Akasema Al-Munaawiy: kauli yake Mtume: “Mtoto wa dada wa watu ni katika wao” kwa sababu ananasibishwa na baadhi yao, naye ni mama yake, naye anaungana na ndugu wa karibu kwa kila kilicho lazima kuungana, kama utetezi, ushauri, upendo, kumfichia siri, msaada, wema, upole, ukarimu na mfano wa hayo”. [Angalia: Faidhu Al-Qadiir: 1/87,88 chapa ya Beirut ya mwaka 1391H].
Katika Hadithi hii, Mtume S.A.W. amebainisha kuwa: Hakika ya mtoto ananasibishwa na kabila la mama yake wakati ukweli hatokani na kabila hilo.
Katika Hadithi sahihi ndani ya kitabu cha Imam Bukhaar inasema kuwa: Hakika Haatwib – Ibnu Balta’at R.A. alimwambia Mtume S.A.W. kuwa: “Hakika yangu mimi nilikuwa mtu wa kikuraishi lakini sikuwa natokana na wao”.
Amesema Ibnu Hajar katika sharhu ya kitabu chake: juu ya kauli ya Haatib: “Nilikuwa mtu wa kikuraishi” maana yake ni kwa urafiki, kwa kauli yake baada ya hapo “Lakini sikuwa natokana na wao”, kauli yake: “Nilikuwa mtu wa kikuraishi lakini sikuwa natokana na wao” kauli hii si yenye kukinzana isipokuwa alitaka kusema kuwa yeye ni katika wao, kwa maana yeye ni rafiki yao, na imethibiti kwenye hadithi kuwa: “Rafiki wa watu ni katika wao”. [Angalia: kitabu cha: Fat-hul Baary: 8/634 chapa ya Beirut].
Na katika hadithi aliyoitaja Haatwib R.A. kuwa yeye ananasibishwa na kabila la mama yake kwa urafiki, lakini ukweli si katika kabila hilo, hatupaswi sisi kumpa mtu asiefahamika kizazi chake au nasaba yake jina la mlezi wake, inatofautiana sura hii na ambayo ipo kwenye sherehe ya aya na hadithi.
Na juu ya hili, yalifanyika hayo kwa waja wema wa zamani na wasomi wa hadithi pasi na kulipinga, ambapo nasaba kwao kwa ilifahamika kwa sababu ya tukio dogo na urafiki mdogo, lau hilo lingekuwa haramu au lenye kupelekea kutumika kwa jina linalozuiliwa basi wangefanya haraka kulipinga.
Anasema Al-haafidh As-suyuuty katika kitabu cha: [Tadriib Ar-Raawy]: “Huenda akanasibishwa mpokezi kwa jina la sehemu, au yaliyomtokea, au kabila, au alichofanya, na wala sio uwazi ambao unaonekana kwenye ufahamu wa nasaba ndio kusudio, isipokuwa ni kwa tukio lililotokea kutokana na kuwepo kwake katika sehemu hiyo, au kabila hilo na mfano wake”. [Angalia: kitabu cha: Tadriib Ar-Raawiy: 2/340].
Kitendo cha kunasibishwa kwa mlezi hakupelekei athari yeyote katika athari za uharamu wa kisheria, lakini hilo ni kama ilivyokuwa kwa wanachuoni na wapokezi wa hadithi walionasibishwa kinyume na makabila yao, zilitumika nasaba kwa kila mmoja wao ambapo inadhaniwa kuwa yeye kwa wale alionasibishwa nao ni mtu wa kizazi hiko, kwa maana: ni mtoto wa kuzaliwa na kabila hilo, basi kunasibishwa pindi kunapokuwa si asili ya mtu, basi ima itakuwa:
12- Kuacha huru mtumwa, nako ndio mara nyingi, mfano: Abiil Bakhtary At-twaaiy At-taabiy, jina lake ni Said Ibnu Fairuoz, naye ni mtumishi wa Twaiu, kwa sababu bwana wake alikuwa ni katika Twaiu kisha akamwacha huru.
13- Au kwa urafiki ambao asili yake ni mikataba na ahadi juu ya kuwa pamoja kusaidiana na kukubaliana katika mambo mbalimbali, mfano: Imam Maalik Ibnu Anas Al-asw-bahiy At-taymiy, naye ni Asw-bahiy kwa kuzaliwa, Taimiy ni kwa urafiki, na hilo kwa sababu watu wake walikuwa ni marafiki wa Taimiy Mkuraishi kwa ushirikiano uliopo.
Uislamu umeondoa urafiki uliokuwepo zama za ujinga wa fitina na mauaji kati ya makabila, au mashambulizi pasi na kushinda mwenye kudhulumiwa na wala kuunganisha undugu.
14- Au urafiki unaoendana na uajiri au kusoma, mfano: Miqsamu, aliitwa ni mtumishi wa Ibnu Abbas kwa kuwa naye sana karibu, au kama vile Malik Ibnu Anas, palisemwa kuwa: alinasibishwa na Taimi kwa kuwa babu yake Malik Ibnu Abi A’amir alikuwa ni mwenye kuajiriwa na Twalhat Ibnu Ubaidillah, pindi Twalhat alipokuwa akifanya biashara.
15- Au kwa kunyonya, kama vile swahaba Abdillah Ibnu As-sa’adiy, Ibnu Abdillah alisema kuwa: aliitwa jina la baba yake As-sa’ady kwa kuwa kwake alinyonyeshwa katika familia ya Baniy Sa’ad bin Bakri.
16- Kwa sababu za dini na kusilimu, mfano: Muhammad Ibn Ismail Al-bukhaary Al-ju’ufy, kwa sababu babu yake Al-mughiira alikuwa ni mpagani na akasilimu kupitia Al-yamaan Ibn Akhnas Al-ju’ufiy, basi akanasibishwa naye.
17- Au jengo la Idara, kwa maana ya kuwa jina lake limeandikwa katika moja ya majengo ya idara, basi akanasibishwa na watu wa ofisi hizi, kama vile Al-laithu Ibn Sa’ad Ibn Abdulrahman Al-fahmiy, basi akanasibishwa na jina la Fahmi, kwa sababu jina lake lipo kwenye ofisi ya Misri katika idara ya Kinana Ibnu Fahmi, na watu wake wanasema kuwa: Sisi ni watu kutoka Fursi ni watu wa Asbahaan, kwa maana: Asili yake ni kutoka Asbahaan lakini hata hivyo alinasibishwa na Fahmi, kwa sababu tu jina lake limo kwenye ofisi ya Fahmi. [Angalia: kitabu cha: Historia ya Damascus, 50/347 chapa ya Beirut mwaka 1419 H].
Kunasibishwa mwanadamu na kabila lisilo lake ni jambo lililoenea na lipo, vitabu mbalimbali vimeshuhudia, kwani ametaja Ibnu As-swalah katika utangulizi wake kuwa, kuna watu ambao wamenasibishwa na wasio baba zao, miongoni mwao wapo walionasibishwa upande wa mama zao, kama vile Sharahbiil Ibnu Hassana, ni jina la mama yake, na miongoni mwao wapo walionasibishwa na bibi zao, kama vile Ya’alaa Ibnu Mun’yat, miongoni mwao pia wapo walionasibishwa na babu zao, kama vile Abu Ubaidatu Ibnul Jar-raah, na miongoni mwao pia wapo walionasibishwa na asiekuwa baba yake kwa sababu, kama vile Mikidad Ibnu Al-as’wad, yeye ni Mikidad Ibnu Amru Ibnu Tha’alaba Al- kandiy, na alikuwa akiishi kwa Al-as’wed Ibnu Abduyaghuuth kisha akanasibishwa naye.
Na wapo walionasibishwa, undani wake kinyume na ufahamu anaoitiwa, kama vile Abu Mas’uud Al-badriy, kauli ya wengi inasema hakuwahi kushiriki vita vya badri, lakini alishuka kwenye viwanja vya badri basi akanasibishwa na jina hilo. (Kitabu cha utangulizi wa Ibnu As-swalaah ukurusa wa 629 na kurasa zinazofuata)
Hii ni mifano iliyotokea inayoonesha kunasibishwa mtu kwa jina ambalo si la baba yake wala kabila lake, madamu hili haliingii katika jambo linalokataliwa kisheria, nayo ni pamoja na athari zitokanazo na majina hayo, na zaidi ya hapo ni kule kunasibishwa mwanadamu na sehemu ambayo amefikia kwa kitendo cha kufikia tu sehemu hiyo, kwa mfano wa Abu Mas’uud Al-badriy.
Na huenda kunasibishwa kukapanuka zaidi, ambapo mtu huwa ananasibishwa na kabila la aliyekuwa bwana wake katika utumishi, mfano: Saidi Ibnu Yasaar Abil Hubbaab Al-haashimiy, kwa kuwa kwake ni mtumishi wa Shukraan mtumishi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alinasibishwa na ukoo wa Haashim. [Angalia kitabu cha: Fat’hul Mughiithu 3/393].
Kunasibishwa mtu kinyume na asili kama ilivyo kwenye mifano iliyopita, hakupelekei zuio la kisheria, kama vile hali ya kunasibishwa mtoto kwa mlezi wake, kwa sababu kusudio la kunasibishwa huku ni kiasi cha kuongeza tu jina na wala si katika uhalisia.
Na kutokana na hili: Kuitwa mtoto asiefahamika nasabu yake kwa jina la mlezi wake si jambo linalofaa kisheria kutokana na kuwepo kwa sura iliyoharamishwa kisheria. Ama kumpa mtoto anaelelewa jina la familia inayomlea ni jambo linalofaa kisheria, kwa dalili zilizotangulia kutajwa, kwa vile huonesha ukaribu wa mtoto kwa familia hiyo pasi na udanganyifu kwa kuitwa mtoto wa kuzaliwa na familia hiyo.
Kunasibishwa huku kunaleta maslahi kwa mtoto katika hatua zake mbalimbali za umri – haswa pale inapokuwa haifahamiki nasaba yake – kwa sababu hilo litaongeza mengi katika maisha yake ikiwa ni pamoja na amani, utulivu na matumaini, na pia kwenye hali hii atakuwa anaye katika hatua mbalimbali za umri wake anayeshika nafasi ya baba na mama mbele ya watu, pamoja na kulinda hukumu za kisheria za uharamu wa kunasibisha, kwa kile kinachopelekea athari mbaya. Kwa hiyo basi sisi katika hili tumechunga na kusimamia makusudio ya Sheria, na wala hatujaangukia kwenye kitu ambacho tumetahadharishwa nacho.
Kutokana na hilo: Uhusiano wenye dhambi ambao umekuwepo kati yako na yule wa kwanza ni mlango wa zinaa, ambao hauthibitishi nasaba, binti huyu si binti yake kisheria, na inafaa kwa huyu binti kuwa na jina la familia ya mumeo wa kisheria Mwislamu pasi na kutumia jina lake na jina la baba yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.


 

Share this:

Related Fatwas