Rangi ya Nguo za Kuombolezea Msiba...

Egypt's Dar Al-Ifta

Rangi ya Nguo za Kuombolezea Msiba.

Question

Je, Ni ipi hukumu ya kuvaa nguo nyeupe kwa mwanamke anayeomboleza? Na je, nguo hizo lazima ziwe na rangi ya nyeusi? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kuomboleza ni kuacha urembo kwa mwanamke aliyefiwa na mume wake anapokuwa katika eda ya kufiwa, kwa kuepuka nguo nzuri na manukato pamoja na mapambo ya vito na ya aina mbali mbali. [Isniy Al Matwaleb katika Sharh Raudhi Atwaleb 402/3, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy]
Uombolezaji kwa mwanamke ni halali, na ni wajibu wake kumhuzunikia mume wake kwa muda wa miezi minne na siku kumi, isipokuwa kama atakuwa mjamzito, eda yake itamalizika kwa kujifungua; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wenye mimba eda yao mpaka watakapozaa.} [ATWALAAQ 4]. Lakini uombolezaji juu ya mtu mwengine basi muda wa kuomboleza ni siku tatu tu bila ya kuongeza, na dalili yake ni maneno yaliyotajwa katika vitabu sahihi viwili vya Hadithi kwamba Zainab Bint Abi Salama amesema aliingia Umu Habibah mke wa Mtume S.A.W. alipokufa baba yake Abu Sufiyan basi Umu Habibah akajiepusha na manukato yenye unjano wa kupauka au kitu kingine chochote kinachofanana nayo, na akajipaka kwayo kijakazi kisha akajizuia na kusema: Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, mimi siyahitaji manukato haya, lakini nimesikia Mtume S.A.W. anasema juu ya mimbari: "Haiwi halali kwa mwanamke anayemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho aomboleze kwa kifo cha mtu aliyekufa zaidi ya siku tatu isipokuwa kwa kifo cha mume wake kwa miezo mine na siku kumi"
Kinachozuiwa katika nguo kwa mwanamke anayeomboleza: Ni vazi linalokusudiwa urembo, na dalili iliyoelezea hukumu hii ni: Nguo iliyopakwa rangi ya Osfori ambayo ni nyekundu na mfanowe. Osfori ni aina ya mmea utoao rangi nyekundu na hutumika kupaka kwenye hariri na mfanowe. [Al Muajam Al Waseet Uk. 405, Ch. Dar Adawa].
Inatajwa katika kitabu cha: [Al Eqnaa' fi Hal Alfaadh Abi Shujaa' kwa Al Khatweb Asherbiniy 56-57/4, Ch. Dar Al Fikr, kwa Hashiyat Al Bigirmiy] katika Fiqhi ya mabwana wa Kishafiy: Kuomboleza ni kujizuia na mapambo mwilini, kama vile dhahabu au nguo iliyopakwa rangi nzuri. Kwa Hadithi ya Abu Daudi kwa Isnadi ya Hassan: "Mwanamke aliyefiwa na mume wake haruhusiwi kuvaa nguo iliyotiwa rangi nyekundu au iliyopakwa udongo mwekundu, wala kuvaa vito, kupaka hina au wanja".
Neno la kiarabu "Mimshaqah" lina maana ya Udongo mwekundu. Au udongo unaofanana na rangi hiyo. Na ni ruhusa kuvaa nguo isiyotiwa rangi na iliyotengenezwa kwa pamba au sufi na katani hata kama itakuwa na thamani kubwa, na ya hariri kama haijatiwa mapambo. Inaruhusiwa nguo iliyotiwa rangi kwa kutokusudiwa urembo kama vile rangi nyeusi, ya buluu au ya kijani iliyokoza na kumili weusi, kwani hivyo haikusudiwi mapambo bali ni kwa ajili ya kubeba uchafu au kwa ajili ya msiba. Na iwapo mwanamke atababaika kati ya kuwa pambo na kinyume chake kama vile rangi ya kijani na ya buluu, kama itakuwa inang'aa au iliyokoza basi ni haramu. Kwani rangi hiyo inapendeza kwa kujirembea, au ikiwa kama na weusi uliyokoza basi hapana. Kwani rangi iliyokoza kwa kijani na bluu huwa inakaribia kuwa nyeusi."
Na kipimo kinachohusiana na Urembo ni mila na desturi. Sheikh Al Bagirimiy alisema katika kitabu chake [Hashiyat Al Bagirimiy Ala Al Eqinai] akielezea tamko lililotangulia la Al Khatweb: "Tamko lake: Pambo, lina maana ya kilichozoeleka kujipambia ili wanaume wakione hata kwa mujibu wa ukawaida wa watu wake au wanawake wenzake."
Na ni karibu kwa maana hiyo iliyotajwa na Imamu Aramliy Al Kabeer katika kitabu chake: Hashiyat [Isniy Al Matwaleb 204/3, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy] kutoka kwa baadhi ya wanavyuoni akasema: "Kauli nzuri ya Sheikh Ibraheem Al Marwaziy, katika maelezo yake mwishoni mwa mlango: Na Mfungamano wa Mlango huu ni kwamba kila chenye Urembo na kinawavutia wanaume kwake yeye mwanamke aliyefiwa na mumewe anatakiwa ajizuie nacho.
Kwa hivyo, hakuna rangi maalumu ya nguo inayozuiwa kwa mwanamke anaeomboleza msiba wa mume wake kisheria au kiutamaduni. Kinachokuwa hivyo huzuiwa na kisichokuwa hivyo hakizuiwi.
Ama kwa nguo nyeupe, mwanamke anaeomboleza hakatazwi kuzivaa ila kwa upande wa zingatio la utamaduni kuwa nguo hizo ni Urembo. Basi katika kitabu cha: [Hashiyat Adesuqiy al Asharh Al Kabeer kwa Sheik Adardeer 478/2, Ch. Dar Al Fikr]: Na mwanamke anayeomboleza atavaa nguo nyeupe kwa ujumla wake iwe nzito au nyepesi. Amesema katika Taudhwihi: wanazuoni kadhaa wameelekea katika kuzia nguo nyepesi iliyo nyeupe, na ukweli katika jambo hilo ni kinachofanyika katika mazoea ya kitamaduni. Na kwa jili hiyo, amesema katika kitabu cha: [Alkaafiy]: Usahihi wake ni kwamba mwanamke haruhusiwi kuvaa nguo anayojipambia kwayo iwe nyeupe au ya rangi nyingine yoyote.
Na katika kitabu cha [Sharh Al Muntaha kwa Al Bahutiy wa Kihambaliy 204/3, Ch. Dar Al Fikr]: "Mwanamke anaeomboleza hakatazwi kuvaa nguo nyeupe hata kama itakuwa nzuri."
Ama kuhusu nguo nyeusi, inaruhusiwa kuvaliwa na mwanamke anaeomboleza hata kama itapambwa bila ya kukusudiwa Urembo -kama yalivyotangulia maelezo yake katika kauli ya Sheikh Al Khatweeb Asherbini- na katika kitabu cha: [Sharhu Al Mahaliy ala Minhaj Anawawiy 53/4, Ch. Dar Al Fikr, Bairut, juu ya Hashiyat Qaliyubi na Umerah]: Inaruhusiwa nguo iliyotiwa rangi (bila ya kukusudiwa urembo) bali kwa kukusudiwa msiba au rangi yenye uwezekano wa kuwa kama uchafu kama vile nyeusi au bluu inayomili weusi.
Na iwapo atakusudia kujipamba kwa nguo hiyo basi itazuiliwa, Sheikh Al Qaliyubi katika kitabu chake [Al Hashiyah] akifafanua kauli aliyoieleza "kama nyeusi" ikiwa si kawaida yao kujipamba kwayo, na kama si hivyo kama ni waarabu basi inazuiwa."
Wanavyuoni wa Kimalikiy waliongeza: "Rangi nyeusi pia huzuiwa iwapo mwanamke ni mweupe sana kwani rangi hiyo humuongezea uzuri." Basi katika kitabu cha: [Asharh Al Kabeer kwa Sheikh Adardeer 478/2, Ch. Dar Al Fikr, katika Hashiyat Adesoqiy]: "(Na akaacha mwanamke aliyefiwa na mume wake kujipamba kwa nguo iliyotiwa rangi) (hata kama) imepauka, na ina rangi iliyokoza wekundu na haijafikia weusi kama atapata nguo nyingine, (isipokuwa nyeusi), ataacha vazi lake isipokuwa likiwa linang'aa kwa weupe wake au likawa ndio kipambo cha kitamaduni kwa watu wake, atalazimika kuliacha.
Na kwa hayo yaliyotangulia, inabainika kuwa hakuna rangi maalumu ya nguo inayovaliwa na mwanamke aliyefiwa na mume wake, isipokuwa kinachozingatiwa katika jambo hili ni urembo na kutokuwa urembo, vazi linalokusudiwa urembo limezuiwa, na vazi lisilokusudiwa urembo limeruhusiwa. Na kigezo katika urembo ni utamaduni na mazoea kama ilivyotangulia kuelezwa. Na iwapo itaamuliwa hivyo, kwa hiyo nguo nyekundu ikiwa pambo katika utamaduni wa nchi ya muulizaji basi itakuwa haramu kuvaliwa na mwanamke aliyefiwa na mumewe.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote

 

Share this:

Related Fatwas