Kuyatumia Majini Katika Shughuli Zi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuyatumia Majini Katika Shughuli Zinazoruhusiwa Kisheria.

Question

Ninihukumu ya kuyatumia Majini katika shughuli zinazoruhusiwa kisheria ambazo inajuzu kwazo Binadamu kuwatumia? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Majini ni tofauti na binadamu, na umoja wake ni jini. inasemekana kuwa: Wameitwa hivyo kwa kuwa wao wanaepukwa na hawaonekani. [Tazama: Mukhtaaru Aswahah Uk. 62 kidahizo cha J.N.N, Ch. Al Matwabah Al Asweriyah]
Ibn Madhuor alisema: J.A.N maana yake kimefichwa, na kila kilichofichwa kwako maana yake ni jini. Na kwa ajili hiyo wameitwa Majini kwa kufichika kwao machoni. Na Majini wana maumbile ya moto yenye nguvu za kubadilika kwa namna mbali mbali. [Lesaanu Al Arab 93/13, kidahizo cha J.N.N, Ch. Dar Swader]
Al Baidhawiy alisema: Majini wana maumbile mengi yenye akili na yaliyofichika, yaliyoelemea zaidi moto na hewa. [Tafseer Al Baidhawiy 224/4, Ch. Al Maktabah Atujariyah Al Kubra], na uwepo wao umethibiti katika Qur`ani na Sunna na Ijmai. Na anayekanusha uwepo wao ni kafiri kwa ukanushaji wake kwa yale yanayojulikana kidini kwa dharura.
Na wanazuoni wamekubaliana kuwa Majini wamekalifishwa na wanapokea ujumbe kama binadamu kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi} [ADH DHARIYAAT 56], Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka} [ARAHMAAN 33]. Na kwa ajili ya Hadithi iliyopokelewa na Al Bihaiqiy katika kitabu cha: [Asunnanu Al Kubra kutoka kwa Ibn Abaas alisema: Mtume S.A.W. Anasema: "Mtume alikuwa akitumwa kwa jamaa zake, lakini mimi nilitumwa kwa Majini na Binadamu".
Na kutumia maana yake ni kuomba msaada na kuwatumia Majini: Ni kuwataka wasaidie. Na kuwaomba wasaidie ni jambo ambalo akili hailipingi bali ni jambo lililopo katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Ametaja kuwadhalilisha Majini chini ya Nabii Suleimani A.S. na akataja kuwa wao waliileta Arshi ya Balkisi kutoka Yemeni. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasio yaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge. (37) Akasema: Enyi wahishimiwa! Ni nani kati yenu atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia nao wamekwisha salimu amri. (38) . Akasema: Afriti, katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako hapo. Na mimi kwa hakika nina nguvu na muaminifu. (39) Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika,anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru,kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu. (40) [AN NAML 37-40]
Na imetajwa kuwa yeye akawatumia katika kazi nyingine kama vili iliyotajwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na tulipo mhukumia kufa, hapana aliye wajulisha kufa kwake ila mnyama wa ardhi aliye kula fimbo yake.Na alipo anguka majini walitambua lau kuwa wangeli jua ya ghaibu wasingeli kaa katika adhabu hiyo ya kufedhehesha} [SEBAI 14] na hayo yanaashiria kuwa inajuzu kwa binadamu kuwatumia Majini. Lakini Kwa kuwa majini wako kama binadamu – wote hawako sawa bali katika wao kuna mwema na kafiri na mwovu - kinakuja kinachokera kwa kuchelea udanganyifu wa majini kwa binadamu. Kwa kuwa kwake haujui ukweli wake na hana yeye kutoka kwa Mwenyezi Mungu anaeweza kumsaidia. Kisha baada ya hapo tunaiangalia kazi inayokusudiwa kufanikishwa na uombaji wa msaada unachukua hukumu yake, kwa kuwa njia zina hukumu za makusudio.
Na Majini miongoni mwao kuna wema na waovu kama walivyo binadamu. Na inajulikana kuwa inajuzu kuwatumia binadamu katika mambo ya kisheria, kama vile kuondosha kitu kizito au kutafuta kitu kilichopotea na kadhalika. Si lazima sana ibada au unyenyekevu wao ukawajibika na amri zake bali inaweza kutimia kinyume na hivyo kwa kuwadhalilisha wao au si hivyo wala vile kwa kujitolea wao kwa kuwatumikia binadamu wema na kuwaongoza kwa masilahi yao maalumu, Na katika watu wa Mwenyezi Mungu, wapo wanaofungukiwa na pazia na wakawa wanatendeana na majini kama watendeanavyo na watu bali majini hujifunza kutoka kwao na hunufaika.
Na kwa kauli hiyo Sheikh Ibn Taimia akataja katika kitabu cha: [Majmou' Al Fatawa 307-308/11, Ch. Mujama'u Al Malik Fahd]: Na kinachokusudiwa hapa ni kwamba Majini pamoja na binadamu wana mazingira tofauti: Na anayekuwa miongoni mwa binadamu anawaamrisha Majini kwa kile Mwenyezi Mungu Mtukufu alichokiamrisha yeye na Mtume wake, kama kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake na kumtii Mtume wake, na akawaamrisha watu kwa hayo basi huyu atakuwa ni katika mawalii bora wa Mwenyezi Mungu Mtukufu naye kwa kazi hiyo ni katika makhalifa wa Mtume na wawakilishi wake.
Na atakaekuwa anawatumia Majini katika mambo ya halali kwake basi naye atakuwa kama yule anaewatumia watu katika mambo ya halali kwake, na hayo ni kama vile akawaamrisha kufanya yaliyo wajibu kwao na kuwakataza waliyoharamishiwa juu yao na akawatumia kwa yaliyo halali kwake basi yeye atakuwa kama Wafalme wafanyao hivyo. Na hiyo ni kama atajaaliwa kuwa miongoni mwa wa mawalii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi kwa hiyo lengo lake kuu ni kuwa miongoni mwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu Nabii Mfalme pamoja na Mja Mtume; kama vile Suleiman, Yusuf pamoja na Ibrahim, Musa, na Issa na Muhamad S.A.W. wote, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani iwe juu yao. Na atakaeyataumia Majini kwa yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake, yawe mambo hayo ni katika shirki au kuua mtu ambaye kisheria haruhusiwi kuuawa au kuwashambulia watu bila ya kuwaua, au kumsababishia ugonjwa, au kumsahaulisha elimu na mengineyo mengi katika dhuluma. Na ima katika vitendo vichafu kama vile kumleta anaetakiwa kufanyiwa uchafu huo, na huku ni kuwatumia katika madhambi na uadui, na kisha iwapo atawatumia wao katika kukufuru basi yeye ni kafiri, na akiwatumia wao katika maasi basi yeye ni asi, na ima atakuwa fasiki na ima atakuwa ni mwenye dhambi lakini sio fasiki.
Na kutokana na hayo; Basi inajuzu kuwatumia Majini katika matendo mema na mambo halali ya kisheria kwa sharti la kutoingia katika mambo yaliyoharamishwa katika sheria.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas