Kusoma Du'aa Ya Qunuti Katika Swala Ya Asubuhi.
Question
Ni ipi hukumu ya kudumisha kusoma Qunuti katika Swala ya asubuhi?
Answer
Kusoma dua ya Qunuti kwa kudumu katika Swala ya Asubuhi ndiyo waliyoshikamana nayo Wanachuoni wa Fiqhi wengi wa zamani na wa sasa. Kuna Hadithi ya Anas Ibn Malik, (R.A) kwamba: “Mtume (S.A.W), aliwaombea dua ya Qunuti kwa muda wa mwezi mmoja, kisha akaiacha, lakini katika Swala ya asubuhi akaendelea kusoma dua ya Qunuti mpaka akafariki dunia” na Hadithi hiyo imepokelewa na kundi la wahifadhi na wakaithibitisha, kama alivyosema Imamu Al-Nawawi na wengineo, na wanavyuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi na Maliki wakachukua rai hiyo. Kwa mujibu wao, inapendekezwa kabisa kusoma dua ya Qunuti wakati wa Alfajiri, na wanafasiri yale yaliyosimuliwa katika kuifuta Qunuti au kuiharamisha kuwa wanasema kilichoachwa ni dua kwa ajili ya watu fulani, si dua ya Qunuti yenyewe.
Yeyote anayesoma dua ya Qunuti wakati wa Alfajiri amefuata Madhehebu ya mmoja wa Maimamu wenye bidii waliofuatwa ambaye tumeamrishwa kuwafuata katika kauli yake Mwenyezi Mungu: “Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.” [An-Nahl: 43], na Maimamu lazima wazingatie yale ambayo yamethibiti na kufanyiwa kazi misikitini na nchini.