Uthibitisho wa Kutotoweka Moto
Question
Je, Ni sahihi kuwa kuna miongoni mwa wanazuoni waliosema kuwa moto utatoweka, na wakaenda mbali zaidi na kusema kuwa moto na watu wake hawatadumu milele ndani yake? Na nini maoni ya jamhuri ya wanazuoni katika jambo hili?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Basi kutoweka ni kinyume cha kubakia, na kutoweka kwa kitu ni kutokuwepo kwake Abu Ali Al Qaliy alisema: "Kutoweka kitu maana yake ni kumalizika kwake. [Taj El Arous 255/39, Ch. Serikali ya Kuwait]. Na kinachokusudiwa ni kutobakia kwa moto. Na wanaosemea kauli hiyo ni Imamu Ibn Taimiah katika kitabu chake: [Aradu Ala Man Qala Bi Fanaau Ajannatu Wanaar]. Na Ibnu Al Qaim katika kitabu chake: [Hadi Al Arwaah Fi Bilaadu Al Afraah].
Tofauti na Jamhuri ya wanazuoni wa kale na waliokuja baada yao kwamba Pepo na Moto vitaendelea kubakia milele na ataneemeka atakayekuwa peponi milele ya watakaokuwa milele na ataadhıbıwa wa kuadhibiwa motoni mpaka milele kwa watu wa milele.
Na Jamhuri ya wanazuoni wa umma imeleta dalili kwa kinachotamkwa na kinachofahamika kutoka katika Qur`ani na Hadithi, dalili ya kutotoweka kwa moto na miongoni mwa matamko hayo ni:
1- Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Isipo kuwa njia ya Jahannamu. Humo watadumu milele. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.} [AN NISAA 169]. Ashaukaniy alisema katika Tafsiri yake: "Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu {watadumu milele} (Kwa ajili ya kuondosha uwezekano kwamba umilele hapa unakusudiwa kukaa kwa muda mrefu) [Fathu Al Qadeer kwa Ashaukaniy 851/1, Ch. Dar Al Wafaa].
2- Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Watadumu humo milele. Hawampati mlinzi wala wakuwanusuru.} [AL AHZAAB 65].
3- Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele.} [AL JIN 23] katika aya hizo na kauli ya wazi ya kubakia kwa adhabu na kutajwa kudumu kwake, na usisitizaji huu wa kudumu milele kwa milele
- Na katika aya zifuatazo Mwenyezi Mungu Mtukufu amezungumzia kutotoka motoni akikazia hayo kwamba adhabu imekaa na itaendelea milele.
4- Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.} [AL BAQARAH 167]
5- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Watataka watoke Motoni, lakini hawatatoka humo, na watakuwa na adhabu inayo dumu.}[AL MAIDAH 37]
6- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannamu.74 Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa.75} [AZ ZUKHRUF 74-75]
7- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Hayo ndiyo malipo ya Maadui wa Mwenyezi Mungu -Moto! Humo watakuwa na maskani ya kudumu, ndiyo malipo yao kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara zetu.} [FUSSILAT 28]
8- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Nao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme: Hakika nyinyi mtakaa humo humo! [AZ ZUKHRUF 77]
9- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?{ [MUHAMAD 15]
10- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Hakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.} [AL BAINAH 6]
11- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo.} [AL HIJR 48]
12- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Hakika huo utafungiwa nao} [AL HUMUZAH 8]
13- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewataja watu wa moto basi anasema: {Na walio kufuru watakuwa na Moto wa Jahannamu, hawahukumiwi wakafa, wala hawatapunguziwa adhabu yake.Hivyo ndivyo tunavyo mlipa kila mwenye kuzidi ukafiri. {FAATER 36]
14- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Na ama wale walio tenda uovu, basi makaazi yao ni Motoni. Kila wakitaka kutoka humo watarudishwa humohumo. Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya Moto ambayo mliyo kuwa mkiikanusha.} [AS SAJDAH 20]
15- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Watasema: Lau Mwenyezi Mungu angelituongoa basi hapana shaka nasi tungelikuongoeni. Ni mamoja kwetu tukipapatika au tukisubiri; hatuna pa kukimbilia.} [IBRAHIMU 21]
16- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Hakika wale walio zikataa Ishara zetu tutawaingiza Motoni. Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishiangozi nyengine ili waionje hiyo adhabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.} [AN NISAA 56]
17- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Na walio zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana naye, hao ndio wenye kukata tamaa na rehema yangu, na hao ndio wenye kupata adhabu chungu.} [AL ANKABUT 23]
Licha ya aya nyingi nyingine kutoka Qur`ani takatifu, ambazo zimethibitisha wazi umilele wa Moto, au umilele wa watu wake ndani yake, na ambazo zinafika aya 37 miongoni mwa aya za Qur`ani, hizo kuna zingine ambazo zina maana ya umilele wa Moto au zinaufaidisha kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hao ndio walio nunua uhai wa dunia kwa (uhai wa) Akhera; kwa hivyo hawatapunguziwa adhabu wala hawatanusuriwa.} [AL BAQARAH 86] Na aya nyinginezo miongoni mwa aya takatifu katika Qurani Tukufu zina maana yenyewe. Na pia aya ambazo zinaashiria umilele watu wa peponi zimefika aya arubaini.
Hakika mambo yalivyo, tunausisitizia wingi huu wa aya zinazothibitisha kuendelea kubakia kwa moto na umilele wa watu wake ndani ya moto huo, kwani hiki ni kiwango cha juu cha wingi – kama anavyosema Sheik wa Uislamu Ataqiy Asubkiy – Inakatazwa kutegemea uwezekano wa ufasiri wa jitihada (Taawil) inawajibisha dalili ya mkato kwa jambo hilo, kama ambavyo aya zenye kutoa dalili ya ufufuo wa mwili kwa wingi wake, zinazuia ufasiri wa jitihada (Taawil) na kuanzia mwanzoni mwake tumetoa hukumu ya kukufuru kwake kwa elimu ya kiujumla, na japo kuwa sikutumia ulimi wangu kumkufurisha mtu maalumu. [Al Eitibaar Bibaqaau Ajanatu wa Anaar, uk. 46 kwa maelezo wangu, Chapa hasa kwa mhakiki Dkt. Twaha Disuqiy Heibeshiy].
Na Hadithi zimepokelewa zikionesha makafiri kukaa milele motoni;
1- Hadithi ya Anas ambayo wanaafikiana nayo na ambayo imepokelewa katika uombeaji wa Mtume S.A.W. Na katika Hadithi hiyo, Mtume S.A.W. amesema: "Basi akawatoa motoni na kuwaingiza peponi na hatabakia motoni isipokuwa aliyefungwa na Qur`ani." Na Qatadah alikuwa akisema katika hayo: "Yaani ukao wa milele umemwajibikia"
Basi Hadithi hiyo ina ishara kwamba miongoni mwa watu wa motoni wataishi humu milele katika moto, na hao ambao Qur`ani imesema kwamba wataishi humo motoni milele, kama vike katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wadumu milele humo}.
2- Yaliyopokelewa na Al Bukhariy na Muslim pia kutoka kwa Ibn Omar R.A ziwafikie wote wawili, kutoka kwa Mtume S.A.W. kwamba amesema: "Mwenyezi Mungu atawaingiza peponi watu wa peponi, na atawaingiza motoni watu wa motoni, kisha atasimama muadhini baina yao na atasema: Enyi watu wa peponi hakuna umauti humo, na enyi watu wa motoni hakuna umauti humo, wote mtaishi humo milele"
Al-Hafidh Bin Hajar alisema: "Al Qortubiy alisema: Na katika Hadithi hizo kumetajwa wazi kwamba hakika kudumu milele kwa watu wa motoni haiwi kuelekea upeo wa milele, na kuishi kwao ndani ya moto kwa kudumu bila ya kufa na wala maisha yenye manufaa au starehe kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na walio kufuru watakuwa na Moto wa Jahannamu, hawahukumiwi wakafa, wala hawatapunguziwa adhabu yake.Hivyo ndivyo tunavyo mlipa kila mwenye kuzidi ukafiri.} [FAATER 36]. Na Mwenyzi Mungu Mtukufu akasema: {Kila wakitaka kutoka humo watarudishwa humo humo.} [AS SAJDAH 20] Akasema: "Na atakaedhani kuwa watatolewa motoni, inaendelea kuwa bila kitu, au utatoweka na kushuka, basi mtu huyo atakuwa nje ya hali aliyokuja nayo Mtume na Watu wa Sunna kukubaliana kwayo". [Fatehu Al Bariy kwa Ibn Hajar Ak Asqlaaniy 221/11, Ch. Dar Al Maairifah].
3- Yaliyotolewa na Ahmad –na kitamko ni kwake- na Ibn Magah na Ibn Habaan kutoka Hadithi ya Abi Hurairah aliseama: Mtume S.A.W. amesema: "Mauti yataletwa siku ya Kisimamo na kusimamishwa katika Njia na kusemwa: Enyi watu wa peponi, watu watachungulia kwa woga wakiwa wanyenyekevu wa kutoka walipo, kisha inasemwa: Enyi watu wa motoni, watachungulia wakiwa na matumaini na furaha ya kutoka walipo, kisha patasemwa: Je mnayajua haya? Watasema: Ndio, hayo ni mauti. Atasema: Patatolewa amri kupasuka Njia, kisha pasemwe kwa watu wa peponi na motoni: Ndani humo kuna umilele na hamtakuta umauti ndani yake milele."
Basi katika Hadithi hiyo ni dalili ya upotofu wa madai ya kutoweka moto, kwani amejaalia moto kama pepo, endapo kuishi milele kwa watu wa pepo humu katika raha na burudisho, na kadhalika watu wa moto wataishi milele katika adhabu daima, basi kama kwamba pepo haitoweki kamwe, basi moto hautoweki kamwe.
4- Yaliyotolewa na Muslim Abi Saiyed Al Khudriy alisema: Mtume S.A.W. amesema: "Ama kwa watu wa motoni ambao wao ni watu wake hakika wao hawafi ndani ya moto wala hawaishi, lakini watu watafikwa na moto kwa madhambi yao, au amesema: Kwa makosa yao – na Mwenyezi Mungu Mtukufu akawafisha mauti mpaka wakawa kama makaa ataamuru Maombezi ya Mtume (Shafaa)"
Mwelekeo wa dalili kutokana na Hadithi hii ni kuwa amesema kwamba kafiri hafi motoni na wala haishi, na ikisemwa kuwa moto unakufa, inaweza kusemwa: Vinatoweka vilivyomo ndani yake kama itakiwavyo, au ukatoweka peke yake bila ya walio ndani yake, na vyote ni batili vinatofautiana na kauli wazi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Tena humo hatakufa wala hawi hai.} [AL AA'LA 13]. Na maana ya aya kama alivyosema Ibn Kathir; "Mtu mwovu ambaye ni kafiri hatakufa akastarehe, wala hataishi yakamnufaisha maisha hayo bali ni madhara tu kwake". [Tafsir Bin Katheer 323/ 14, kwa kueleza kwangu, Ch. Mu'sasat Qortubah]. Kwani kutoweka kwa Kafiri atakuwa amekufa na kustarehe, na akiwa hai kinyume cha hivyo atakuwa amestarehe ndani yake pia na yote hayo ni batili.
5- Na Ibn Abi Shaibah na Atwbaraniy wametoa kutoka kwa Abdullahi Bin Amro R.A. wote wawili, kwamba akasema: "Watu wa motoni wanamwita Malik, basi hawajibu muda wa miaka arobaini, kisha naye atasema: {Hakika nyinyi mtakaa humohumo!} [AZ ZUKHRUF 77]. Halafu watamwomba Mola wao wakisema: {Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kweli sisi ni wenye kudhulumu.} [AL MUU'MINUN 107]. Basi Mola wao hatawajibu kama alivyokuwa akiwajibu duniani, halafu atawaambia: {Tokomeeni humo, wala msinisemeze} [AL MUU'MINUN 108]. Kisha watu wanakata tamaa basi hauwi huo isipokuwa mlio wa muungurumo na mruzi unaofanana na sauti za punda, wa mwanzo wake ni mlio kama wa punda na mwingine ni kama mruzi.
Na amenukulu Ijmaa'i juu ya kutotoweka moto zaidi ya mmoja miongoni mwa wanazuoni; Al Imamu Al Qortubiy rehema ya Mwenyezi Mungu juu yake alisema: "Na wamekubaliana kwa ujumla Ahlu Sunna kwamba watu wa motoni ni wa milele ndani ya moto huo bila kutoka, kama vile Ibilisi, Farauni, Haman na Qaruun, Na kila atakayekufuru na kufanya kiburi na kupotoka basi ana moto ambapo hatakufa ndani yake wala hataishi, na Mwenyezi Mungu amewaahidi watu wa motoni adhabu kali. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje hiyo adhabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.} [AN NISAA 56]. Na wamekubalia kwa ujumla Ahlu Sunna pia kwamba hatabakia ndani ya moto huo au kuishi milele isipokuwa kafiri aliyeupiga vita uislamu, na utambue. Nilisema: -Msemaji ni Al Qortubiy- Na baadhi ya wanaoelemea upande wa elimu katika wanazuoni, wameteleza hapa na wakasema: Hakika kafiri, mwovu na mpiga vita dini watatoka motoni na kuiingia peponi.
Hakika yake inajuzu kiakili kukatika kwa sifa ya hasira, na akasema: Na vivyo hivyo inajuzu kiakili kukatika kwa sifa ya Upole na kuwajibisha Mitume na mawalii wakaingia motoni na kuadhibiwa ndani yake, na jambo hili ni baya lisilokubalika kutokana na ahadi yake Mwenyezi Mungu ya uhakika na tamko lake la kweli.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema katika haki ya watu wa peponi: {Hicho ni kipawa kisio na ukomo.} [HUUD 108]. Yaani kisichokatika, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo.} [AL HIJR 48]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Hakika wanao amini na wakatenda mema watakuwa na ujira usio na ukomo} [FUSSILAT 8]. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu.(21) Watadumu humo milele (22)} [Atawbah 21-22].
Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema katika haki ya makafiri: {wala hawataingia Peponi mpaka apite ngamia katika tundu ya sindano.} [AL AARAF 40]. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao.} [AL JATHIYAH 35]. Na hili liko wazi, na kwa ujumla, hakina upenyo kinachoingia akilini kwa kile kilicho katika asili yake kwa Ijmaai na Mtume. {Na ambaye Mwenyezi Mungu hakumjaalia kuwa na nuru hawi na nuru.} [AN NUUR 40]" [At Tazkarah kwa Al Qortubiy 920-921/1, Ch. Dar Al Minhaaj].
Na Al Imamu Abu Jaafar Atwahawiy Al Hanafiy akasema: "Na Pepo na Moto ni viumbe wawili, wasiotoweka milele au kuangamia" [Sharhu Al Akidah Atwahawiyah kwa Al Maidaniy, Uk. 119, Ch. Dar Al Fikr].
Na Ibn Hazm akasema: "Makundi ya Umma yamekubaliana yote juu ya kwamba Pepo haitatoweka na wala neema zake hazitatoweka, na Moto pia na adhabu zake havitatoweka, isipokuwa Watu katika wale Rawaafidha (Wapingaji)". [Al Faslu fiy Al Milal Wa Al Ahwaa Wa Anehal 69-70/4, Mktabat Al Khanngiy].
Na akasema katika kitabu chake: [Maratib Al Ijmaa'i] katika: "Mlango wa Ijmaa katika Itikadi ambazo mtu hukufurisha anayehitilifiana naye kwa Ijmaai" Na kwamba moto upo kweli na kwamba hiyo ni nyumba ya adhabu ya milele isiyotoweka na wala watu wake hawatoweki milele bila mwisho". [Uk. 193, Ch. Dar Al Afaaqu Ajadidah].
Na sheiku wa Uislamu Taqiyu Ediin Asubkily akasema -kama tulivyotangulia kunukulu-: "Na kwa hiyo, waislamu wamekubaliana juu ya Imani hiyo na wameipokea kutoka kwa waliowatangulia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, na hili linatambulika hivyo kimaumbile kwa waislamu, linajulikana kidini bila ubishi, bali na mila nyingine zote zisizokuwa za waislamu, na wanaamini hivyo. Na atakaye yarudia hayo basi yeye ni kafiri kama vile mtu aliyejitafsiria Aya zilizopatikana katika Ufufuliwaji wa miili, naye ni kafiri pia kwa mujibu wa Elimu, hata kama mimi siuachii ulimi wangu utamke hivyo. [Al I'tibaar Bibaqaa Al Janatu wa Alnaar Uk. 57-85]
Na Imamu Al Adhad Al Ejiy akasema: "Waislamu walikubaliana kwamba makafiri wataishi na kudumu milele motoni na adhabu yao haikatiki kamwe" [Al Mawaqif kwa Al Ejiy 499/3, Ch. Dar Ajeel].
Na Imamu Assa'd Ataftazaniy akasema: "Hakuna hitilafu katika umilele wa maisha ya watu wa peponi, na wala katika kukaa milele kafiri kwa ubishi au kwa itikadi motoni, na iwapo atafikia katika jitihada ya kuingia katika mambo ya jumla, na hakuwa na zingatio lolote kinyume na Aljaahidh na Al-Ambari. Waislamu wote wakakubaliana kwa kuishi milele kwa watu wa peponi, na kukaa milele kwa makafiri motoni." [Sharhu El Maqaswed kwa At Taftazaniy 131/5, Ch. Alam Al Kutuub].
Na Al Haafedh Ibn Hajar Al Asqalaniy akasema: "Al Qortubiy akasema: Atakayedhani kuwa wao hutokana naye au hubaki tupu au huteketea basi atakuwa ametoka nje ya yale aliyokuja nayo Mtume S.A.W. na Wanazuoni wa Sunna waliokubaliana nayo." [Fathu El Baariy kwa Ibn Hajar Al Asqalaniy 421/11].
Na Imamu As Safariniy wa Kihambali akasema: "Basi imethibitika katika aya wazi na habari sahihi tulizotaja umilele wa watu wa peponi na wa motoni ni wa kudumu, kila kilichomo ndani yake kama neema na adhabu kali, na kwa hali hii kuna makubaliano ya wanazuoni wa Sunna na ijmaa. Basi walikubaliana juu ya kwamba adhabu ya makafiri haikatiki na kama vile kwamba burudani ya watu wa peponi haikatiki. [Lawame' Al Nwaaru El Bahiyah 234/2, Ch. Mua'sasat na Makatabat Al Khafiqeen].
Na Mtalaamu mkuu Al Alusiy amesema: "Nawe unajua kuwa kuishi milele kwa makafiri ni jambo walilokubaliana waislamu wote, na wala hakuna zingatio lolote kwa mpingaji, na dalili za wazi ziko nyingi bila kikomo." [Roho Al Maaniy 164/12, Ch.Dar Ihiyaa At Turaath Al Arabiy].
Ama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua.} [AL NAAM 128], Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ama wale wa mashakani hao watakuwamo Motoni wakiyayatika na kukoroma. (106) Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hakika Mola wako Mlezi hutenda apendavyo. (107)} [HUUD 106- 107]. Basi siyo kusudio hapa kwa utenganishaji katika Aya mbili ni Utoaji, bali isipokuwa ni utengaji unaoambatana na utashi, basi labda Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Wamekaa motoni ukao wa milele kama Mwenyezi Mungu atataka hayo."; Kwani kila kitu kiko chini ya utashi wa Mwenyezi Mungu na kutaka kwake na inajuzu kiakili katika utashi wake akaamua kutowaadhibu, na akiwaadhibu hatawaweka milele kwenye adhabu hiyo.
Kinachokusudiwa kwa utenganishaji huu katika aya mbili ni mwongozo wa waja wa Mwenyezi Mungu kuelekea katika uwajibu wa kuyaachia mambo yao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na vile vile kutangaza kwao kwamba kila kitu kiko chini ya utashi wake na jinsi atakavyo yeye. Kwani yeye ndiye Mtendaji Mchaguaji asiyewajibika kwa kitu chochote na wala hakuna yeyote mwenye haki juu yake, na wala hakuna jambo la wajibu juu yake kulifanya isipokuwa kwa mazingira ya utashi wake atakavyo yeye aliyetukuka.
Na siyo kusudio kutoka utenganishaji na mifanano yao, kukanusha kwa kukaa kwao milele motoni, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Ametumbia katika kitabu chake kitukufu kwa kukaa milele kwa makafiri kudumu milele motoni.
Na Ibn Kathir ameashiria kwa hayo katika kauli yake: "Inamaana kuwa kudumu kwao sio jambo la wajibu kama lilivyo lenyewe, bali linauegemea utashi wake Mwenyezi Mungu Mtukufu." [Tafseer Ibn Katheer 474/7].
Na yanayokusudiwa kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi.} [HUUD 107], ya kusudio la Kudumu na kukanusha kukatika kwa njia hiyo ni kauli ya waarabu: "Mimi sitafanya hivi hata kama sayari zitadhihirika" au "au hata kama mwangaza wa Alfajiri utaangaza" na "Haukutofautiana mchana na usiku" na maneno mengine yanayomaanisha Umilele kwa waarabu. Kwani waarabu wanapotaka kukipa kitu wasifu wake wa kudumu milele husema: "Hiki ni cha kudumu milele ya mbingu na ardhi". Na kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasemesha kwa kile wakijuacho miongoni mwao, na wala haikusudiwi kusitisha maamuzi yao ndani yake kwa kudumu mbingu hizi na ardhi, kwani Maandiko yenye dalili za wazi yanathibitisha umilele wa maamuzi yao ndani yake.
Ama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wakae humo karne baada ya karne} [AN NABAI 23], Basi kauli yake: {Wakae humo karne baada ya karne} inaungana na yanayofuatia na hiyo ni Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji, (24) Ila maji ya moto sana na usaha, (25)} [AN NABAI 24-25]. Yaani Wakae humo karne baada ya karne katika hali ya huwa Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji. Ila maji ya moto sana na usaha. Basi kama zikiisha karne zile waliadhibiwa kwa aina nyingine za adhabu pasipo maji ya moto sana na usaha, na inaashiria hiyo kauli wazi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba ataadhibiwa kwa aina nyingine za adhabu pasipo maji ya moto sana na usaha, kauli yake katika Surat Swaad: {Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha! (57) Na adhabu nyinginezo za namna hii} [SWAAD 57-58] [Rejea Tafsiru Atwabariy 26-27/24]
Na katika Hadithi walioitumia kutoa dalili ni ile iliyotolewa na Atwabaraniy kutoka kwa Jafar Bin Azubeer kutoka kwa Al Qasim kutoka kwa Abi Umamah R.A kwamba amesema: "wataujia Moto wa Jahannamu siku moja utakuwa kama shamba linalowaka moto na lililo jekundu, milango yake inajigongagonga". Na wanajibiwa kwamba Hadithi hii ni Maudhui (ya kutungwa) na wala haisihi kuifanya kama dalili. Ibn Ajawz akasema katika kitabu chake: [Al Maudhuaat]: "Hadithi hii ni Maudhui (ya kutungwa) na muhali, na Jaafar naye ni "Ibn Azuber". Shu'bah akasema: Alikuwa akiongopa. Na Yahya akasema: Haikupokelewa na mwaminifu. Na Asaadiy akasema: Wameisema vibaya Hadithi yake. Al Bukhariy, An Nasaaiy na Ad Darqatwniy wakasema: Ni ya kuachwa. [Al Maudhua'at kwa Ibn Ajawzey 268/3, Ch. Adhwaau Essaaf na Al Maktabatu Et Tadmeriyah].
Na miongoni mwao pia ni yale yaliyopokewa na Abd Bin Humaid katika tafsiri yake kutoka kwa Hassan alisema: Omar Akasema: "Kama watu wa Motoni wangekaa Motoni kama kiasi cha muda wa idadi ya mchanga uliolundikana basi wangelikuwa na siku ya kutoka humo." Basi hiyo ni athari inayokatika; kwani Al Hassan hakuisikia kutoka kwa Omar, na inayokatika kwa wanazuoni wa Hadithi ni Hadithi dhaifu, na Hadithi dhaifu haifai kuchukuliwa kuwa hoja katika masuaa hayo.
Na ufupisho wa kauli ya jibu linalotokana na Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Maswahaba ni alichokisema Sheikh Swanani baada ya kuipokea yote, na akazungumza mwelekeo wa Dalili iliyomo ndani yake, na alitambua muradi sahihi uliyomo humo, kisha akasema: Na kwa hali hii unajua kuwa haisihi kuinasibisha kauli ya kutoweka kwa moto na kupotea kwake kwa Ibnu Asuudi na Abuu Huraira kama ilivyonasibishwa hii kauli iliyonukuliwa kutoka kwao mpaka kwa Omar, bali ni dalili ya kuendelea kubakia kwa moto baada ya kutoka kwa mwenye kutoka motoni humo miongoni mwa watu wa Tawhidi.
Basi vipi Sheikh wa Uislamu katika mwanzo wa suala hilo aseme: kwamba kauli ya kutoweka moto imenukuliwa kutoka kwa Ibn Masuod na Abi Hurairah; na hakika ya mambo ni kwamba sanadi yake katika unasibishaji wa hayo ni kwa wawili hawa ni hizi Hadithi mbili ambazo ni za hatua za dalili za kutoweka kwa moto na kuondoka kwake baada ya kusihi kwa Hadithi hizo, basi nimejua upotofu wa nasaba ya kauli hiyo kwa Ibn Masuod na Abi Hurairah, pia nimejua upotofu wa nasaba yake kwa Omar.
Na baada ya uhakiki wako kwa yale tuliotangulia kuyasema na kwa kujua kwako kule tulikoelekea utajua kuwa maswahaba hao wanne; ambao ni Omar, Ibn Masuod na Abi Hurairah na Abi Saiyed ambao Sheikh wa Uislamu akiyataja majina yao miongoni mwa maswahaba mwanzoni mwa suala, na akataja kuwa yeye aliwanukulu kauli yao ya kutoweka kwa moto na kupotea wao wako mbali na kauli hii pamoja na kuwanasibisha kwake kutoweka kwa moto, ni kama kutokuwa na hatia ya makosa kwa mtoto wa Yakobo, na akawatolea dalili kwa kile alichokidai kinanasibishwa kwao kwa namna isiyomgusa kwa madai yake kama nilivyoelewa mimi. Na kwa wakati huo atajua kuwa hana katika madai yake ya kutoweka kwa moto yeyote miongoni mwa maswahaba aliyewaainishia. [Rafu'o Al Astaar kwa Ibtwaal Adilat Al Qailiina Bifanaai An Nar kwa Al-Swana'aniy Uk. 77, Ch. Al Maktabu Al Islamiy]
Na kutokana na yaliyotangulia; basi Hakika kauli ya kutoweka kwa moto waliyoisema Maimamu wawili, Ibnu Taimia na Ibnu Lqiamu, inakwenda kinyume na inavyoamiwa na Watu wa Sunna na Jamaa, na wala haijuzu kuamini madhehebu kama haya.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.