Usahihishaji wa Baadhi ya Hadithi kuhusu Qur'ani
Question
Tumeona ombi linalotolewa na kukusanywa swali juu ya usahihishaji wa baadhi ya Hadithi, na kubainisha: Je, Hadithi hizi ni sahihi au la kama ifuatavyo:
1- “Fikisheni kwa niaba ya Allah, naye aliyepata Aya ya Kitabu cha Allah, hakika amepata amri ya Allah”.
2- “Jifunzeni Kitabu cha Allah, kimilikeni, kisomeni siku zote, na kisomeni kwa sauti nzuri”.
3- “Aliyeweka sunna nzuri katika Uislamu, na watu baada yake waliitekeleza, basi atapata thawabu ya hao walioifanya, bila ya kupotezwa cho chote cha ujira wao, na aliyeweka Sunna mbaya katika Uislamu na watu baada yake waliitekeleza, basi atapata dhambi ya hao walioifanya, bila ya kupotezwa cho chote cha dhambi zao”.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Kuhusu hadithi ya “Fikisheni kwa niaba ya Allah, naye aliyepata Aya ya Kitabu cha Allah, hakika amepata amri ya Allah”. Hadithi hii imepokelewa kwa njia ya Abdir-Razzaq, kutoka kwa Ma’mar, kutoka kwa Qatadah, katika kauli yake Mwenyezi Mungu: {ili kwa hiyo nikuonyeninyinyi na kila imfikiyayo}.Kuwa Mtume SAW, alisema: “Fikisheni kwa niaba ya Allah, naye aliyepata Aya ya Kitabu cha Allah, hakika amepata amri ya Allah”.
Na Abdur-Razzaq ameipokea katika tafsiri yake [2/205], na kwa njia yake, At-Twabariy [5/161], na Ibn Abi-Hatim [4/1272], na hii ni Mursal. Kuna ushahidi kwake, ilivyopokelewa na Bukhariy katika Kitabu chake kutoka kwa Abdillashi Ibn Amr RA, na Mtume SAW, kuwa yeye alisema: “Fikisheni kwa niaba yangu hata lau Aya moja”.
Kuhusu Hadithiya “Jifunzeni Kitabu cha Allah, kimilikeni, kisomeni siku zote, na kisomeni kwa sauti nzuri”. Kwa lafudhi hii ameipokea Imamu Ahmad katika Musnad yake [28/591] na An-Nasaiy katika Al-Kubra [7/226] na wengineo kutoka kwa Ukbah Ibn Amir Al-Juhaniy, na Mtume SAW, na Isnad yake ni nzuri.
Na kuhusu Hadithi ya: “Aliyeweka sunna nzuri katika Uislamu, na watu baada yake waliitekeleza, basi atapata thawabu ya hao walioifanya, bila ya kupotezwa cho chote cha ujira wao, na aliyeweka Sunna mbaya katika Uislamu na watu baada yake waliitekeleza, basi atapata dhambi ya hao walioifanya, bila ya kupotezwa cho chote cha dhambi zao”. Hadithi hii ni sahihi; ameipokea imamu Muslim katika kitabu chake [4/2058/Nambari: 1017] kutoka kwa Jariir ibn Abdillahi RA, na Mtume S.A.W.
Na Hadithi sahihi kama alivyosema Imamu Al-Hafidh Ibn As-Salaah katika Muqadima yake [Uk.: 11-12, Ch. Ya dar Al-Fikr]: ni: “Hadithi yenye Isnad inayoendelea kwa kauli ya mwenye uadilifu, na mwenye kudhibiti, kutoka kwa mfano wake, hadi ya mwishoni mwake, na haikuwa peke yake wala yenye kasoro. Na sifa hizi zinatambua aina nyingine kama vile: Mursal, Munqati’, Mua’adhal, Shadh, na yenye kasoro sana, na mpokeaji wake ana kukosoa”. [Mwisho].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.