Tafsiri ya Kiashiria ya Qur’ani

Egypt's Dar Al-Ifta

Tafsiri ya Kiashiria ya Qur’ani

Question

Nini tafsiri ya kiashiria? Na je, inahesabiwa kuwa miongoni mwa tafsiri zinazokubalika kwa Qur`ani? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Maana ya neno tafsiri katika lugha ya Kiarabu ni: kubainisha na kudhihirisha maana ya maneno au lafudhi kwa kutumia maneno mengine yaliyo wazi kwa upande wa mfasiri kwenda msikilizaji. Kisha Tha’lab na Ibn Al-Arabiy walisema kuwa: Tafsiir na Taawiil yana maana moja. [Taj Al-Arus: 13/323, Kidahizo: Fa Sa Ra; At-Tahriir Wat-Tanwiir: 1/10, Ch. Ya Ad-Dar At-Tunusiyah Lin-Nashr, Tunisia].
Na maana ya kiistilahi ya neno Tafsiri ni: Elimu inyochunguza kubainisha maana ya lafudhi za Qur`ani Tukufu na kifahiwa chake ama kwa muhtasari au upanuzi. [At-Tahriir Wat-Tanwiir: 1/11].
Tafsiri inatofautiana kutokana na njia za wafasiri wenyewe, na tafsiri ya kiashiria ni aina ya tafsiri ya Qur`ani tukufu, ambayo inaambatana na mfano maalum wa ufahamu, nayo ni kufahamu maana ambazo hazidhihiri moja kwa moja, lakini zinahitaji kuzingatia na kuchunguza, na maana hizi zinachukuliwa kwa viashiria vya Aya, na zinadhihiri kwa watawa na wenye elimu.
Sheikh Az-Zurqaniy aliifafanua kuwa: “kutafsiri Qur`ani kwa maana isiyo dhahiri, kutokana na ishara inayofichwa, lakini inadhihiri kwa watawa na wanasufi, kama inawezekana pia kuwiana kati ya dhahiri inayotakiwa na ya kufichwa”. [Manahel Al-Irfan: 2/56, Ch. Ya Isa Al-Halabiy].
Kuhusu maana ya tafsiri ya kiashiria, Ibn Al-Qaiym anasema: “Viashiria ni maana zinazoashiria hakika kwa umbali na nyuma ya bazia, nazo pengine ni kwa njia ya sikio, macho, akili, na pengine na hisia zote, kwa hiyo, viashiria ni miongoni mwa dalili na kufahamisha, na sababu yake ni: usafi kwa jumla unaoboresha hisi na akili ili iwe tayari kutambua mambo yasiyo dhahiri, ambapo hisi na akili ya mwingine haiwezi kuzitambua. Na mimi nilisikia Sheikh wa Uislamu Inb Taimiyah, Mwenyezi Mungu aitakase roho yake, akisema: Sahihi yake ni: inavyoonesha lafudhi kwa ishara yake, kwa mlango wa Qiyasi bora sana”. [Madarij As-Salikiin: 2/389, Ch. Ya Dar Al-Kitaab Al-Arabiy].
Wanachuoni walitaja masharti ya kukubaliwa tafsiri ya kiashiria, na maana ya kukubaliwa kuwa kutokataliwa, na si uwajibikaji wa kuichukua. Kuhusu kutokataliwa kwa sababu haipingi dhahiri na haifiki kiwango cha kosa, na haipingwi wala kukanushwa na dalili za kisheria; kuhusu si uwajibikaji wa kuichukuwa kwa sababu ni aina ya hisia ambazo haziambatani na dalili wala hoja, lakini ni jambo ambalo analikuta mwanasufi katika nafsi yake, na ni siri kati yake na Mola wake, kwa hiyo, ana haki ya kuichukua na kuitekeleza madhumuni yake, bila ya kumlazimisha mwingie aitekelezee.
Masharti haya kama yalivyotajwa katika kitabu cha: [Manahil Al-Irfan: 2/81] ni yafuatayo:
1- Isiyopinga na inavyodhihiri katika maana ya Qur’ani tukufu.
2- Asipojidai kuwa ni muradi pekee mbali na dhahiri.
3- Isiyokuwa Ta’wiil ya kigeni na mbaya, kwa mfano, tafsiri ya baadhi ya watu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na bila shaka Mwenyezi Mung Yu pamoja na wafanyao meme}. [Al ANKABUUT: 69] ambapo waliitafsiri Aya kwa njia isiyofaa.
4- Isiyokuwa na kinyume chake cha kisheria na kiakili.
5- Inakuwa na dalili ya kisheria inayotegemeza.
Lakini masharti haya yameingiliana, kwa hiyo, sharti la kwanza inaweza kulibadilishwa kwa sharti la kwanza, pia la nne kwa tano. Ni bora kuangalia masharti mawili ambayo ni mbadala wao:
Kwanza: kubainisha maana inayomaanisha lafudhi ya Qur’ani tukufu kwa sifa hasa.
Pili: Tasiri ya kiashiria isipelekea mchafuko kwa anyepokea tafsiri (mpokeaji). [Mwishokwa baadhi ya mabadiliko].
Kauli za wanachuoni kuhusu tafsiri ya kiashiria:
Al-Ghazaliy anasema: “Kila neno katika Qur`ani linahitaji uchunguzi katika maana yake, na maana haya yanabainika kwa wale waliotabahari katika elimu kwa kadiri ya wingi wa elimu yao, na usafi wa nyoyo zao, na kupatikana sababu za kuzingati, na ikhlasi ya kuomba elimu, na klia mmoja awe na mpaka unaompelekea kupanda ngazi ya juu… lakini kufika upeo wa elimu ya maana hakuwezekani, hata bahari ingekuwa wino na miti kalamu, siri za maneno ya Mwenyezi Mungu haziishi, na bahari zote zinaweza kuisha kabla ya maneno ya Mwenyezi Mungu hayajaisha… na siri za mambo haya ni nyingi, na tafsiri ya dhahiri haioneshimaana inayoficha, wala haipingi tafsiri ya dhahiri, bali ni ukamilifu wake, na kufikia kiini chake pamoja na dhahiri, na hayo tunayoyataja kwa kufahamu maana ya batini ambayo hayapingani na dhahiri, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi wa yote”. [Ihya’ Uluum Ad-Diin; 1/293 na baadala yake, kwa mabadiliko].
Sheikh Taj Ad-Diin Ibn Atwaa-Illahi As-Sakandariy katika kitabu cha: [Lataiful-Minan] anasema: “Jua kuwa tafsiri ya maneno kama hayo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake S.A.W., kwa maana ya kigeni… si kwa njia ya kubadilisha dhahiri yake, kwa sababu dhahiri ya Aya ni ilivyoletwa kwa ajili yake, na ilivyoonesha kwa kanuni ya lugha, lakini kuna maoni ya batini ya kufahamu Aya na Hadithi kwa yule Mwenyezi mungu afungue moyo wake. Imetajwa katika Hadithi: “Kila Aya ina dhahiri na batini na mpaka na upande”…usijizuie kupata maana hayo kutoka kwao wakati mwenye ubishi na upinzani anaposema:
Haya ni mabadiliko ya maneno ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na hakika haya si mabadiliko, lakini mabadiliko yapo wakati wanaposema: hakuna maana mengine kwa Aya isipokuwa haya, na wao hawakusema hivi, bali wakakiri dhahiri iwe dhahiri kutokana na muradi wa maudhui yake, na wakafahamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu alivyowafahamisha”. [Lataiful-Minan: Uk. 235-236, Ch. Ya Dar Al-Kitab Al-Masriy].
Viashiria vina aina kadhaa, vilivyotajwa na Imamu At-Tahir bin Ashuur katika tafsiri yake [At-Tahriir wat-Tanwiir: 1/35 na baada yake] aliposema: “Kwa maoni yangu kuwa viashiria hivi ni aina tatu:
Kwanza: maana inaonesha ulinganishi wa hali iliyotajwa katika Aya na hali inayolingana nayo, kwa mfano, walisema katika Aya ya: {Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayezuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kwamba humo lisitajwe jina lake na akajitahidi kuiharibu}. [AL BAQARAH: 114], kuwa hii ni ishara kwa nyoyo, kwani nazo ni mahali pa unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, na kwa njia yake anajuliwa, basi nyoyo zinamsujudia kwa unyenyekevu wa nafsi zote.
Na kuzuia utajo wake, maana yake ni kukataza nyoyo zifikie maarifa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na akajitahidi kuiharibu, maana yake kuzichafua nyoyo kwa maovu na matamanio. Na hii inafanana hali ya yule asiyetakasa nafsi yake kwa njia ya maarifa, na akakataza moyo wake usiingizwe na sifa nzuri kutokana nayo, na hali ya yule anayezuia misikiti lisitajwe jina la Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, kutaja Aya hapo hapo ni mfano wa ulinganishi.
Pili: Ilivyokuwa mfano wa Ta’wiil, ambapo neno lina maana isiyokuwa maana yake ya kawaida, hapo mtumiaji anachagua maana yenye umuhimu kwake, kutokana na moyoni mwake, mfano wa anayesema katika kauli ya mwenyezi Mungu: {Na nani huyo awezaye kuombea mbele Yake (Mungu)}. [AL BAQARAH: 255], ambapo, kutokana na lafudhi nyingine ya Kiarabu, maana yake: (aliyedhalilisha nafsi yake) basi awe miongoni mwa watawa wenye shafaa. Hapo mfasiri anachagua maana maalum iliyochukuliwa kwa lafudhi maalum, na akatumia Ta’wiil ya maana iliyopo ndani moyoni mwake. Na Sheikh Muhiy-Diin anaiita aina hii ya tafsiri (kilichosikilizwa), na yeye nibora zaidi.
Tatu: Ibra na mawaidha: kwa sababu watu wenye nafsi hai wanafaidika na kila kitu, wakachukua hekima katika kila mahali walipoikuta, unadhani nini wanapoisoma Qur`ani, wakaizingatia, wakapata mawaidha yake, na kama wakisoma kauli yake Mwenyezi Mungu: {Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamtesa mateso makubwa}. [AL MUZZAMMIL; 16] wakafahamu kuwa: moyo usiomuitikia mjumbe wa maaria ya juu, basi matokeo yake ni mabaya… na kila ishara isiyo ya aina hizi tatu basi inakaribia pole pole na kauli ya Wabatini, mpaka kufukia kauli yao yenyewe”.
Miongoni mwa vitabu vya tafsiri vinavyojadili suala la Tafsiri ya Kiashiria: Tafsiri ya An-Naisaburiy; Tafsiri ya Al-Aalusiy; Tafsiri ya At-Tasturiy; Tafsiri ya Muhiy-Diin Ibn Arabiy; Tafsiri ya Abi Abdi-Rahman As-Sulamiy (Haqaiqut-Tafsiir); Tafsiri ya Abil-Qasim Al-Qushairiy; Tafsiri ya Abi Muhammad Ash-Shiraziy (A’raisul-Bayan Fi Haqaiqil Qur`ani); Tafsiri ya Ibn A’jibah (Al-Bahrul Madiid); na Tafsiri ya Ismaiil Hqqiy (Rohol-Bayan).
Mwishoni: Tafsiri ya Kiashiria ya Qur`ani inakubalika kwa masharti yaliyotajwa hapo juu, ambayo yananukuliwa na wanachuoni.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas