Tahadhari ya udanganyifu na kuvunja ahadi
Question
Sharia ya Kiislamu Imetahadharisha vipi suala la udanganyifu na kuvunja ahadi?
Answer
Mtume S.A.W. ameeleza kuwa udanganyifu na kuvunja ahadi ni katika mambo ya wanafiki, na ni wajibu kwa muumini kujiepusha na hayo; Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Amr Allah R.A. yeye na baba yake amesema kwamba Mtume S.A.W. amesema: Mambo manne mwenye kuwa nayo anakuwa mnafiki moja kwa moja: Mtu ambaye akizungumza husema uongo, akiahidi hatimizi na akikubalina na mtu huvunja ahadi, na akigombana hufanya uovu, na mwenye kuwa na jambo Moja kati ya hayo anakuwa na jambo katika unafiki, mpaka atakapoacha"