Upinduaji Katika Kusoma Qur`ani

Egypt's Dar Al-Ifta

Upinduaji Katika Kusoma Qur`ani

Question

 Imamu wa msikiti katika sala ya Isha, na katika rakaa ya pili, amesoma, baada ya Surat –Al-Fatha, sura hutangulia sura aliyoisoma katika rakaa ya kwanza, kutokana na mpangilio wa msahafu, na baada ya kumaliza sala, baadhi ya wanasala walimkosoa, hata baadhi yao walisema kuwa: sala imevunjika, kwa mtazamo wa upinduaji wa kusoma, ambao kumekatazawa. Twaomba kutujulishwa, na ninyi mna thawabu zaidi.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Neno upinduaji katika lugha ya Kiarabu maana yake ni: kupindukia kitu kichwani mwake, kwa kukifanya juu ni chini na mwanzo ni mwisho. Katika Kamusi ya Al-Lisan na Ibn Mandhuur [kidahizo cha: Na Ka Sa: 6/241, Ch. ya Dar Sadir]: Upinduaji wa vitu, maana yake: kupindukia kitu kinyume chake, na kukifanya juu ni chini, na mwanzo ni mwisho”.
Na maana ya upinduaji katika istilahi hapa ni: kusoma mwisho kabla ya mwanzo kwenye Qur`ani tukufu, na upinduaji huu una aina nne: Upinduaji wa herufi, maneno, aya, na sura. Upinduaji wa herufi ni; kusoma herufi kinyume, kwa kusoma herufi ya mwisho ya neno kwanza, kisha iliyo kabla yake n.k., katika maneno yote, kuanzia herufi ya mwisho na ya mwanzo, kwa mfano: kusoma (BAR) badala ya (RAB). Upinduaji wa maneno ni: kusoma maneno kinyume chake; kusoma neno kisha lililo kabla yake n.k; kuanzia neno la mwisho na la mwanzo, kwa mfano kusoma: (Mmoja (tu), Mwenyezi Mungu, Yeye ni, sema), badala ya: {sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja (tu)}.
Upinduaji wa Aya una sura mbili:
Ya Kwanza: kusoma Aya kinyume chake; kusoma Aya kisha iliyo kabla yake n.k.; kuanzia Aya ya mwisho na ya mwanzo, kwa mfano kusoma: {(Ambaye ni) katika majini na watu}, kisha {Atiyaye wasiwasi nyoyoni mwa watu}, kisha {Na shari ya mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma} n.k.
Ya Pili: Kusoma jumla ya Aya kutoka kwa sura maalum, kisha kusoma jumla nyingine ya Aya kutoka kwa sura yenyewe, iliyoanzia alivyozisoma kwanza, kwa mfano: kusoma kwanza Aya mbili za mwisho kutoka kwa suratul-Baqarah, kisha kusoma Ayatul-Kursy (Aya ya Enzi) ndani ya rakaa moja au ya rakaa mbili.
Upinduaji wa Sura ni: kusoma sura kinyume cha mpangilio wake katika msahafu; kusoma sura kisha iliyo kabla yake n.k., kuanzia sura mwisho kimpangilio na ya mwanzo, kwa mfano: kusoma (Suratul-falaq) kabla ya (Suratul-Ikhlas).
Hukumu inaelekea katika upinduaji wa herufi, maneno, na sura ya kwanza ya upinduaji wa Aya ni; kwa sababu unavunja mfumo wa Qur`ani, hata inakuwa maneno ya kigeni.
Kuhusu upinduaji haramu wa maneno, Al-Bahutiy Al-hanbaliy katika kitabu cha: [Sharh Al-Muntaha 1/191, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “inaharamishwa upiduaji wa maneno ya Qur`ani kwa kuvunja mfumo wake , na (sala inanvunjika nao); kwa sababu unakuwa kama maneno ya kigeni, unaovunja sala ikiwa kwa makusudio au sahau”.
Kuhusu upinduaji wa herufi, unashirikiana na upiduaji wa maneno katika sababu ya uharamu, bali unazidi kuwa unabadilisha maneno peke yake bila ya maana hata kidogo.
Kuhusu upiduaji wa Aya, ni kinyume cha mpangilio wa Aya unaokubalika kwa pamoja, na pia hubadilisha maana, ikawa maneno ya kigeni na Qur`ani, na Ad-disuqi Al-Malikiy katika Hashiya yake ya Ash-Sharh Al-Kabiir na Sheikh Ad-dardiir [1/242, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “Inaharamishwa upiduaji wa Aya zinazoambatana katika rakaa moja, na kuvunja sala, kwa sababu ni kama maneno ya kigeni”.
Az-Zurqaniy katika kitabu cha: [Sharh ya Mukhtasar 1/203, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “inaharamishwa kuipindua Aya za sura moja katika rakaa moja au wakati mmoja, hata bila ya sala”.
An-Nafarawiy Al-Malikiy Katika kitabu cha: [Sharh Ar-Risalah 1/66, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: mpangilio wa Aya unaainishwa kwa kauli ya pamoja”.
As-Safariniy Al-Hanbaliy katika kitabu cha: [Sharh Mandhumat Al-Aadaab 1/414, Ch. ya Muassasat Qurtubah] anasema: “kuhusu mpangilio wa Aya unathibitishwa kwa matini, kwa kauli ya pamoja”. Kuhusu upinduaji wa sura katika aina yake ya pili: ni kinyume cha iliyo bora zaidi au makuruhu, kwa rai ya wengi wa wanachuoni, kwa sababu ya kupinga Sunna ya kusoma Qur`ani kwa utaratibu wake.
An-Nawawiy Ash-Shafiy katika kitabu cha: [Al-Majmuu’ Sharh Al-Muhadhab; 3/349, Ch. ya Al-Muniriyah] anasema: “Wanachuoni wanasema: Sunna ni kusoma sura kwa mpangilio wa msahafu siku zote, kama akisoma sura moja katika rakaa moja, atasoma katika rakaa ya pili sura inayofuata sura ya kwanza. Na Al-Mutawaliy anasema: kama akisoma katika rakaa ya kwanza: {Sema: Ninajikinga kwa Bwana Mwenye kuwalea}, atasoma katika rakaa ya pili: mwanzoni mwa Al-Baqarah. Na kama akisoma sura moja , kisha akasoma katika rakaa ya pili sura iliyo kabla yake, basi amepinga iliyo bora zaidi, na hana kosa, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi ya yote”.
Az-Zurqaniy Al-Malikiy katika kitabu cha: [Sharh ya Al-Mukhtasar 1/203, Ch. ya Dar Al-fikr] anasema: “Ilichukiwa upinduaji sura mbili au zaidi ndani au nje ya sala, akikusudia Qur`ani, lakini akikusudia kumtaja Mungu tu, basi ni kupinga iliyo bora zaidi tu, na iliyo bora zaidi ni kupangilia mfano wa Qur`ani, (Taz. Al-Wanshrisi). Na miongoni mwa upiduaji uliochukiwa ni kusoma nusu ya mwisho ya sura, kisha nusu yake ya mwanzo, ndani ya rakaa moja au mbili, na sala haivunjiki kutokana na upinduaji uliochukiwa”.
Al-Bahutiy Al-Hanbaliy katika kitabu cha: [Sharh ya AlIqnaa 1/344, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “inapendwa kusoma kama ilivyo ndani ya msahafu, kutokana na mpangilio wa sura), na Ahmad katika mapokezi ya Muhana: Napenda kusoma kutoka kwa Al-Baqarah mpaka chini; kwa sababu hii ndio iliyonukuliwa na Mtume S.A.W, (na inaharamishwa kupindua maneno) yaani maneno ya Qur`ani, kwa sababu ni kuvunja mfumo wake, (na sala inavunjika kwa upinduaji); kwani kuvunja mfumo kuyafanya maneno ya kigeni, kuvunja sala kwa kukusudia au kusahau. (Na inachukiwa upinduaji wa sura) kama kwamba kusoma: Suratu Alamnashrah, kisha kusoma: Suratu dh Dhuhaa, na ikiwa (ndani ya rakaa moja au rakaa mbili); na kwa mapokezi ya Ibn Masu’ud kuwa aliulizwa kwa anayesoma Qur`ani kiupinduaji, akasema: hivyo ni upinduaji wa moyo”.
Wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy walielekea kwenye kauli ya makuruhi yenye uharamu kwa sura mbili za upinduaji katika sala ya fardhi, isipokuwa hazivunji sala; na katika [Ad-Durul-Mukhtar na Al-Haskafiy], miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Hanafiy [na Hashiyat Ibn Abidiin: 1/546-547, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]: “inachukiwa kukata kwa sura fupi, na kusoma kiupiduaji, isipokuwa akihitimu, basi atasoma kutoka kwa Al-Baqarqh. Na katika Al-Qunyah: kusoma katika rakaa ya kwanza: Al-Kafirun, na rakaa ya pili: Alam Tara, au Tabbat, kisha alitaja: aendelee, na inasemwa: kukata akaanza, na haichukiwi hivi katika sala ya Sunna”.
Ibn Abidiin alieleza katika Hashiyah akisema: “(kauli yake: kusoma kiupinduaji) yaani anasoma katika rakaa ya pili sura iliyo kabla ya sura ya rakaa ya kwanza; kwani mpangilio wa sura katika kusoma ni wajibu, lakini inajuzu hivi kwa watoto kwa ajili ya kurahisisha elimu; kauli yake: (isipokuwa akihitimu… n.k.), katika sharh Al-Munyah: na katika Alwalwaljiyah: anayehitimu Qur`ani katika sala, akimaliza Al-Muawidhatein katika rakaa ya kwanza, arukuu, kisha asome katika rakaa ya pili Al-Fatiha na kitu cha Suratul Baqarah; kwa sababu Mtume S.A.W, alisema: “Aliye bora zaidi kuliko wote, ni mwenye kutua, na mwenye safari”, yaani: anayemaliza tena akaanza. [Mwisho];kauli yake: (katika rakaa ya pili) yaani akaanza rakaa ya pili; kauli yake: (Alam Tara) au (Tabbat), yaani akapindua au akakata kwa sura fupi; kauli yake: (kisha alitaja, aendelee) yaani upinduaji au kukata kwa sura fupi hakika inachukiwa katika hali ya kusudio, lakini katika hali ya kusahau, haidhuru, kama ilivyotajwa katika Sharh Al-Munyah”.
Fahamu maneno haya kuwa: hii ni makuruhi ya uharamu, lakini haivunja sala, na makuruhi ya uharamu ni aina ya uharamu, kwa maoni ya wengi wa wanachuoni, na madhehebu ya wanachuoni kuhusu suala hili ni: kuangalia mpangilio ni jambo linalotakiwa, na kauli ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy kuwa ni wajibu, haikuwa na dalili, na rai yenye nguvu zaidi ya wanachuoni kuwa: inatakiwa kuangalia mpangilio katika sura mbili, na upinduaji ni makuruhu kuhusu hizi mbili, au ni kupinga iliyo bora zaidi.
Kwa mujibu wa yaliyotangulia kuwa: inaharamishwa kuzipindua herufi, maneno, na sura ya kwanza ya upinduaji wa Aya; kwa sababu ni jambo linalovunja mfumo wa Qur`ani, na kuufanyia kama maneno ya kigeni, au kubadilisha maana. Kuhusu sura ya pili ya upinduaji wa Aya na Sura za Qurani, hizi ni kupinga iliyo bora zaidi, au makuruhu, kwa sababu ni kupinga Sunna ya kusoma Qur`ani na mpangilio wa utaratibu.
Kwa hiyo, na uhalisia wa Swali: alivyofanya Imamu huyu wa msikiti ni kinyume cha iliyo bora zaidi, au makuruhu, na sala yenyewe ni sahihi, kwa maoni ya wanachuoni wote.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaid.

 



 

Share this:

Related Fatwas