Mwanamke mwenye damu ya ugonjwa kusoma Qur`ani
Question
Ni ipi huku ya mwanamke mwenye damu ya ugonjwa kusoma Qur`ani?
Answer
Damu ya ugonjwa ni hali ya mwanamke ya kutokwa na damu nje ya Siku zake za mwezi, na nje ya wakati wa Nifasi, hukumu za hedhi hazimhusu mwanamke mwenye damu ya ugonjwa, kwani hiyo ni hadathi ndogo, kunajuzu kwake kusoma Qur`ani, na akitawadha kunajuzu kwake kuushika msahafu.