Swala na Saumu ya mgonjwa
Question
Je, ni ipi hukumu ya Swala na Saumu kwa mgonjwa mwenye ugonjwa unaoathiri uwezo na mwendo wake?
Answer
Wakati wa ugumu wa kuswali swala za Faradhi, Mwenyezi Mungu Mtukufu hamfanyii mgonjwa tabu ya kuzitekeleza kwa kadiri ya uwezo wake, kusimama, kukaa, au kulala ubavu au mgongo, na anaashiria kurukuu na kusujudu. akishindwa kufanya yote hayo, kiasi kwamba hawezi kuashiria isipokuwa kwa macho, au nyusi, au moyo, basi Swala huondolewa kwake kulingana na Madhehebu ya Hanafi, na rehema za Mwenyezi Mungu zina nafasi kwa ajili ya kila mtu.