Kushikwa na ugonjwa kunafuta dhambi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kushikwa na ugonjwa kunafuta dhambi

Question

Je, kupatwa na maradhi kunafuta dhambi na makosa?

Answer

 Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amewashukuru waja wake kwa kujaalia subira yao bila ya pingamizi kwa madhara yanayowapata kuwa ni njia ya kafara ya dhambi zao na makosa yao. Imepokelewa kutoka kwa Abu Huraira, (R.A) kutoka kwa Mtume (S.A.W), amesema: “Muislamu hatopatwa na tabu, wala maradhi wala mashaka wala huzuni wala udhia wala msononeko mpaka mwiba unaomchoma isipokuwa Allah Humfutia dhambi zake kwa sababu ya hayo”. Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari.

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Malik, (R.A), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), aliingia kwa Bedui mmoja akimtembelea huku Bedui yule ana homa, akasema: “(Ugonjwa wako ni) kafara na utakaso.” Imepokelewa kutoka kwa Ahmad katika “Musnad yake.”

Basi mgonjwa yuko chini ya uangalizi wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya subira yake kwa yale yaliyompata na kuridhika kwake na hukumu ya Mwenyezi Mungu juu yake.

Share this:

Related Fatwas