Kufa kwa sababu ya ugonjwa wa kansa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufa kwa sababu ya ugonjwa wa kansa

Question

Je, aliyekufa kwa sababu ya ugonjwa wa kansa huwa shahidi?

Answer

Kwa hakika anayekufa akiathirika kwa ugonjwa wa kansa hutarajiwa kupata malipo ya shahada katika Akhera, kwa rehma yake Mwenyezi Mungu, kwa kuwa amekusanya sababu ya shahada kwa kuumwa na kufariki kwa sababu ya nje, na sababu hizo haziainishwi, bali ni nyingi na tofauti moja yake huashiria nyinginezo miongoni mwa magonjwa ambayo yanaweza kuwapata watu, na kwa kuwa ugonjwa wa kansa ni mojawapo ya aina za magonjwa ambayo yana baadhi ya alama za pamoja na magonjwa mengine na huambatana na magonjwa mengineo kwa hatari na ubaya zaidi, lakini anayekufa akiathirika kwa ugonjwa huu yaani; kansa basi hukumu zake ni zile zile hukumu za maiti wa kawaida, kwa hiyo anaoshwa, kuwekwa ndani ya sanda, kusaliwa na kuzikwa.

Share this:

Related Fatwas