Kujitolea nyewele kwa watoto ambao ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kujitolea nyewele kwa watoto ambao ni wagonjwa wa kansa

Question

Je, inaruhusiwa kwa mtu kujitolea sehemu ya nyewele zake kwa hospitali ya kutibu kansa kwa watoto, kwa lengo la kuzitumia kutengeneza wigi kwa wale watoto? 

Answer

Inajuzu kwa mtu kujitolea sehemu ya nyewele zake kwa hospitali ya kutibu kansa kwa watoto kwa lengo la kutengeneza kinachoitwa "wigi" ili wale watoto waivae badala ya nyewele zao zilizoanguka kwa sababu ya dawa ya kemikali, kwani kufanya hivyo huhakikisha maslahi yao yaliyo thabiti kisharia, katika hali hii, anayetoa sehemu za nyewele zake huwa anastahili malipo mema makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwani anachangia kuwapunguzia watoto hawa madhara ya kisaikolojia, hasa ikikubukwa kuwa mgonjwa huyu ni mtoto anayehuzunika kwa kukosa nyewele zake, kwa hakika hukumu hiyo haifungamani na hukumu ya Wasl (kuunganisha nyewele za mtu kwa nyewele au wigi nyingine) ambayo ni marufuku kwa mujibu wa Sharia, zaidi ya hayo mtoto ambaye hajabaleghe bado haulizwi vitendo vyake.

Share this:

Related Fatwas