Kuapa kwa jina la Mtume S.A.W na kwa watu wa nyumbani kwake pamoja na Kaaba.
Question
Ni ipi hukumu ya mtu kuapa kwa jina la mtu mwingine ili kufikia mahitaji yake kwa njia ya kuapa kwa jina la Mtume S.A.W na watu wa nyumbani kwake pamoja na Kaaba?
Answer
Kuapa au kusisitiza maneno kwa jina la Mtume S.A.W au kwa mwingine kwa msemaji kusema kwa mfano: Naapa kwa jina la Mtume au Kaaba….nk miongoni mwa yasiyokusudiwa kiapo cha kweli ni jambo linalofaa Kisharia na wala hakuna ubaya ndani yake kwa kauli ya Jamhuri ya Wanachuoni, wala haifai kuzuia kwa dalili ambazo uwazi wake unaharamisha kuapa kinyume na jina la Mwenyezi Mungu, hilo si katika mlango huu, nalo limekuja katika maelezo ya Mtume S.A.W na maelezo ya Maswahaba Watukufu, kutoka kwa Abi Huraira R.A amesema: Siku moja kuna mtu alikuja kwa Mtume S.A.W na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni sadaka ipi yenye malipo makubwa zaidi? Mtume S.A.W akasema:
“Ninaapa kwa haki ya wazazi wako: Ni kutoa sadaka ukiwa na afya nzuri, una uwezo wa kufanya ubahili, kuhofia umasikini na matumaini ya kuwa na utajiri”….
Na Hadithi nyingine imepokewa na Masheikh wawili kuwa mke wa Abi Bakri Swiddik R.A alisema kumuambia mumewe:
“Naapa kwa utulivu wa jicho langu, yenyewe hivi sasa ni zaidi kabla ya hapo kwa mara tatu” akimaanisha kulisha wageni wake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mwenye kujua zaidi.