Usthamala wa Mtume S.A.W. na kuchun...

Egypt's Dar Al-Ifta

Usthamala wa Mtume S.A.W. na kuchunga hisia za watuwengine

Question

Vipi Mtume S.A.W. alikuwa akichunga   hisia za watu wengine?

Answer

Muamala wa Waislamu kwa wasiokuwa Waislamu umejengwa kwa usthamala, kuishi kwa pamoja na kuheshimiana, ambapo sharia imeamrisha kudhihirisha wema, huruma, uadilifu na ihsan katika kuamiliana na tunaotofautiana nao katika dini na akida; Mwenyezi Mungu Anasema: (Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu) [Al-Mumtahina: 8].

Wote wakaishi chini ya Uislamu na wakiheshimu akida zao, ada zao na tamaduni zao.

Ustahmala wa Mtume S.A.W. ukafikia kukataza kutukana maiti za wasiokuwa waislamu ili kuwa wakirimu watoto zao na kuungana nao, kama ilivyokuja katika kauli ya Mtume S.A.W. alipowaambia Masahaba zake:"Atawajia Akrama Mtoto wa Abou Jahly akiwa ameamini na kuhamia Madina Msimtukane baba yake, kwa sababu kutukana maiti kunamuudhi aliyehai na hayamfikii maiti" Hadithi hii imepokelewa na Aalwaqidy katika Maghazy".

Share this:

Related Fatwas