Kuapa kwa jina la Mtume S.A.W na wa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuapa kwa jina la Mtume S.A.W na watu wa nyumbani kwake pamoja na Kaaba.

Question

Ipi hukumu ya mtu kutegemea mtu mwingine ili kutimiza mahitaji yake kwa njia ya kuapa kwa jina la Mtume S.A.W na watu wa nyumbani kwake pamoja na Kaaba?

Answer

Kuapa au kusisitiza maneno kwa kutaja jina la Mtume S.A.W au kwa mwingine kwa msemaji kusema: Na Mtume – kwa mfano – au na Kaaba…..nk, ambapo haikusudiwi kiapo cha kweli kabisa, ni jambo linafaa Kisharia na wala hakuna ubaya wowote kwa mujibu wa Wanachuoni wa Fiqhi, wala haifai kuzuia hilo kwa kutumia dalili ambazo uwazi wake zinaharamisha kiapo kinyume na Mwenyezi Mungu, kwani hii si katika maswala hayo, imepokewa katika maneno ya Mtume S.A.W na maneno ya Maswahaba Watukufu, kutoka kwa Abi Huraira R.A amesema: Kuna mtu mmoja alikuja kwa Mtume S.A.W akauliza, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni sadaka gani yenye malipo makubwa zaidi? Mtume S.A.W akasema:

“Ninaapa kwa mama na baba yako: Ni mtu kutoa sadaka wakati akiwa mzima wa afya anahofia umasikini na anatumani utajiri”.

Share this:

Related Fatwas