Kuhiji kwa niaba ya wengine kwa pes...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhiji kwa niaba ya wengine kwa pesa sadaka

Question

Je, inajuzu kuhiji kwa niaba ya mwingine kwa pesa sadaka?

Answer

Asili ni kwamba Hijja ifanywe kwa niaba ya mtu aliyekufa kutokana na fedha zake mwenyewe ikiwa alitoa wasia na ndani ya ukomo wa theluthi moja (ya mali aliyoicha), na  inaweza kuwa kutokana na fedha za mtu ambaye atatekeleza Hijja kwa niaba yake, na inaweza pia kuwa kutoka kwenye pesa za wasiokuwa hao wawili, yaani: kwa pesa ambayo ni ngeni kwao, na kwa  kadiri ya juhudi, taabu, na gharama ya mtu anayewajibika, ndivyo kadri atapata thawabu kama neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mtume (S.A.W), alimwambia Aisha, (R.A) kuhusu malipo ya Umra yake: “Kwa kadiri ya taabu yako,” au akasema: “gharama yako. ” Imepokelewa kutoka kwa Mashekhe wawili.

Hakuna pingamizi la kuhiji kwa niaba ya mwingine kwa pesa sadaka.

Share this:

Related Fatwas