Kuwaozesha Vijana wasio na Uwezo kw...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwaozesha Vijana wasio na Uwezo kwa Mali ya Zaka

Question

Kamati ya Zaka ya Jumuiya hukusanya zaka, sadaka, na michango na kuwagawia wanaostahiki. Baadhi ya vijana wasio na uwezo wa gharama za ndoa, hufika kwa kamati ili kupata msaada wa ndoa zao, na jumuiya inatoa msaada wa mali na kifedha kwa ndoa zao. Je, inajuzu pesa hizo za zaka hutumika katika mambo hayo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Kutoa Zaka ili kusaidia anaetaka kuoa asiyeweza kumudu gharama zake ni jambo linalojuzu kwa Madhehebu ya Malik, na kama wasemavyo baadhi wafuasi wa Madhehebu ya Hanbal, wanasema kwamba katika kutimiza kutoshelezana ni kumpa masikini katika mali ya Zaka ili kufikia kupata kitakachomwezesha kuolea akiwa hana mke na akawa anahitaji kuoa([1]).

Imamu Al-Hattab Al-Maliky amesema: “kwamba yatima anapewa katika mali ya Zaka kiasi ambacho anakitumia katika mahitaji yake ya ndoa, na ni jambo ambalo amelipendekeza kadhi Hassan katika haki ya mtoto aliezuiwa kutumia mali zake, hivyo basi, yule ambaye hana vitu na mapambo ambavyo ni lazima kwa ajili yandoa atapewa katika ya Zaka, hii ni bora lizangtieni([2]).

Imepokewa kutoka Umar bin Abdula Aziz kwamba yeye alimwamrisha mpiga mbiu kwa watu: “Wakowapi masikini? Wakowapi wenye madeni? Wako wapi wanaotaka kuoa?” kwa maana ambao wanataka kuoa na hawana uwezo, amewaita ili awape katika pesa katika hazina ya Waislamu.

Zaka ni wajibu kwa Waislamu tu; kwa sababu inachukuliwa kutoka kwa matajiri Waislamu na hupewa masikini wao. Na Zaka ya mali asili yake ni kutolewa mali, ikiwa anaestahiki anahitaji kitu kitakachomsaidia, basi hakuna ubaya kuitoa katika hali ya kitu; kwa sababu kinachotakiwa ni kufikia masilahi yake.

Hivyo katika uhalisia wa swali kunajuzu kwa kamati kuotoa Zaka kwa lengo lililotajwa kwa Waislamu wanaohitaji katika njia ya msaada wa kifedha, ikiwa wanaofaidika na hilo wanahitaji kitu miongoni mwa mahitaji ya ndoa na kamati ikaweza kumpa, basi kunajuzu hilo pia.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

 

([1]) Hashiyat Al-Rawdha Al-Murabba, 1/400.

([2]) Mawahib Al-Jalil fi Sharh Mukhtasar Khalil, 2/347.

Share this:

Related Fatwas