Kumzawadia Maiti thawabu za Qur’ani...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumzawadia Maiti thawabu za Qur’ani kwa

Question

Je, inajuzu kwa mujibu wa Sharia ya Kiislamu Kumzawadia Maiti thawabu   za kisomo cha Qur’ani?

Answer

Imethibiti kuwa kusoma Qur’an na Kumzawadia Maiti thawabu za kisomo cha Qur'ani inajuzu, na malipo yatawafikia maiti na watanufaika nayo, Mungu akipenda. Kwa mujibu wa yale kauli ya Mtume (S.A.W) kumwambia Amr Ibn Al-Aas, (R.A): “Ikiwa alikuwa Muislamu na mkimuacha huru kwa niaba yake au mkitoa sadaka kwa niaba yake au kuhiji kwa niaba yake, hilo lingemfikia” (Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud). Hii inaashiria kuwa malipo ya kusoma Qur’ani yamemfikia maiti. Hakuna tofauti kati ya manufaa yake kutokana na kuacha huru, sadaka, na Hija kwa niaba yake, na manufaa yake kutokana na kusoma Qur’ani. Wanachuoni wa Fiqhi wamesema kwamba kafara yoyote anayoifanya na akaifanya malipo yake kwa ajili ya maiti itamfaa, Mwenyezi Mungu akipenda. Muislamu anaposoma Qur’ani, nia yake ya kuisoma iwe safi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aisome kwa unyenyekevu na kutafakari.

Share this:

Related Fatwas