.Uchafu
Question
Nini uchafu na unafahamika vipi kama ni sifa mbaya ambayo ni lazima kujiepusha nayo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1- Katika makamusi kuna maelezo mazuri yenye kuzungumzia kuhusu mdudu ambaye ametufundisha namna ya kuwa na subira pindi tunataka kujifunza, naye ni nzi, na ameitwa hivyo kwa sababu kila anapofurushwa na mtu basi huwa anamrudia tena, naye nzi huwa haelewi kuwa hapendwi na amekwishafukuzwa na pengine hata amefanyiwa jaribio la kutaka kuuliwa. Na kwa sifa hii ndio akawa mdudu mbaya. Na kwa mtu mwenye kusifika na uchafu huwa haelewi mahusiano yake na wengine, kama ambavyo haelewi udhaifu wake wala hisia za wengine kuwa hawamtaki, kwani huwa anafanya matendo yasiyokubalika, ambayo yaonesha kuwa hajali na wala hana hisia zozote zaidi ya ujinga.
2) Mwenyezi Mungu Mtukufu amezungumza kuhusu nzi ndani ya kitabu chake kitukufu kwa kupigia mfano kwa kusema kuna na sifa dhaifu za kung`anga`ania kurudia pale alipofukuzwa (kutojali wengine), na kama akifukuzwa sehemu iliyo na chakula au kinywaji au hata kwenye damu baada ya kuifonza basi huwa hatuna njia nyingine ya kuirudisha (haki yetu), sawa iwe ameofonza kisha akaruka au tukampata na kumuua.
Tatizo ni kuwa ametutawala na pia anatunyanganya kile awezacho kukipata. Na inasemekana kuwa baadhi ya marafiki walimuuliza imamu Shafie (amani zimshukie) “Ni kwa nini ameumbwa nzi?” akasema “ili awakere wafalme,” na wakati huo palikuwa na nzi aliyekuwa akimzonga, imamu Shafie akasema: “ ameniuliza na sikuwa na jibu kwa wakati huo lakini baada ya kumuona nzi (akinizonga) ndio nikapata jawabu.
3) Na Mwenyezi Mungu ameelezea kuhusu uwezo alipompa mdudu huyu juu ya mwanadamu, kwani pamoja na udhaifu wake na nguvu zake ndogo isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyemuumba na hakuna awezae kufanya hivyo. Ni kiumbe cha Mwenyezi Mungu, na yuko kila mahala ingawa kuna juhudi nyingi zifanyewazo na watu za kutaka kuwaangamiza na kuwatokomeza na ndio maana tunaona dawa za kuwaua ziko za kila aina zilizoenea ulimwenguni kote. Na katika kampeni mashuhuri ni ile iliyofanywa na Marekani ya kutaka kuwaua nzi wote kabla ya vita vya kwanza ya dunia, kwani walikuwa wakitenga dakika tano kila siku kwa ajili ya kuwaua nzi, na ilikuwa ifikapo saa saba kasoro dakika tano kengele ilikuwa ikipigwa kwa ajili ya kuacha kazi na kutoka nje kwenda kuua nzi kisha hurudi na kuendelea na shughuli zao, na hii ilikuwa ikujulikana katika taifa la Marekani kama siku ya kitaifa ya (kuua) nzi.
4) Mweneyzi Mungu Mtukufu anasema {Enyi watu! Unapigwa mfano, basi usikilizeni. Hakika wale mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, hawatuomba hata nzi ijapo kuwa watajumuika kwa hilo.Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata kwake.Amedhoofika kweli huyo mwenye kutaka na mwenye kutakiwa.} (AL HAJJ;73) Na ilivyokuwa kiumbe hiki Mwenyezi Mungu Mtukufu anakipigia mfano kwa watu ili wapate kufikiri na kwa kuwa kiumbe hiki kimeenea basi Mtume (rehma na amani zimshukie) ametupa hekima ambayo unajuulisha kuwa uisilamu ni dini ya kilimwengu na ni ya kila mahali na kwa nyakati zote na kwa watu wote na kwa hali zote na ni dini ya upendo na upole nani dini ya wepesi na utaratibu na ni dini ya yenye kuhuisha uhai. Na Mtume (rehma na amani zimshukie) anasema katika hadithi iliyotolewa na Bukhari katika kitabu chake, “Pindi akiingia nzi katika kinywaji cha mmoja wenu basi amzamishe (ndani) kisha amtoe, kwani moja ya ubawa wake kuna ugonjwa na (ubawa) mwengine ni dawa.” (Al-Bukhariy).
Na asili ni kuwa iwapo mfu (kiumbe kilichokufa) kikiingia katika chakula au kinywaji basi chakula huwa kimenajisika na hakuna budi isipokuwa kukitupa na kuacha kukila, kwani kula kitu najisi ni haramu, na hii ndio hukumu iwavyo, isipokuwa hukumu ya nzi ipo tofauti na hii. Na imekuja hukumu hii ili kuwaonea huruma mafakiri katika nchi zenye ukame au jangwani au wakati wa majanga na vita na njaa, kwani iwapo nzi ataingia katika chombo cha mmoja wao na ikawa hukumu yake ni kukitupa chakula hicho basi ingepelekea kupotea kwa chakula ambacho watu watakuwa wanakihitajia zaidi. Na ndio maana ikawa hadithi imewasaidia watu wengi kwa kuwapa hukumu yenye wepesi kwao, na hii ndio asili ya maelezo ya kisheria.
Katika hadithi hii kuna maelekezo yenye kuwepesha kwa yule atakaefikwa na hali hiyo, ama ikitokezea kwa mtu binafsi chakula chake au kinywaji chake kikaingia nzi basi ana hiari kwani hii si amri ya kisheria bali ni ruhusa iliyowekwa kwa ajili ya kuwawepesishia watu. Na watu wengi hawawezi kutafautisha kati ya hali mbili, hali ya ruhusa ambayo inanasibiana na uisilamu na hali ya ulazima au sunna ambayo inatakiwa kuwepo kwa ajili ya kuwepo maisha yenye furaha, na watu hawa wapo wa aina tatu: Wapo walioikubali hadithi hii na kusema ni katika sheria; na wapo walioipinga na kusema kuwa hii si katika hadithi na wengine wakakana kuwa uisilamu hauwezi kunena jambo kama hili.
Na kufahamu sheria ni jambo la muhimu sana hasa katika masuala kama haya, kwani haitopelekea kuwepo kwa mawazo hasi wakati wa kusikia kile ambacho nafsi inakidhania au kimependekezwa katika utamaduni, lakini jambo ambalo litashika nafasi ni ile hali ya kuzingatia, kufikiri na kujiuliza, ili afahamu yule anayepinga jambo hili ya kuwa hakutenda kosa kwa sababu ya kuuliza kwaze. Kwani Mtume (rehma na amani zimshukie) alikuwa akiacha kula baadhi ya vyakula na wala havipendi na kuwaachia wengine wa vile.
Alikataa kula kenge (aina ya mjusi), imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Niliingia mimi na Khalid bin Walid pamoja na Mtume (rehma na amani zimshukie) katika nyumba ya Maimuna, akatuletea kenge (aina ya mjusi) wa kuchoma akaunyoosha mkono wake kwenye chakula hicho, baadhi ya wanawake waliokuwemo ndani ya nyumba ya Maimuna wakasema, muulizeni Mtume (rehma na amani zimshukie) juu ya chakula anachokitaka. Mtume akaondoa mkono wake kwenye chakula hicho. Nikasema: je chakula hiki ni haramu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema “hapana, isipokuwa chakula hiki hakipo katika ardhi ya watu wangu (sehemu ninayoishi) na ndio maana sijakipenda.” Khalid akasema”, nikamvuta nikamla huku Mtume (rehma na amani zimshukie) anaangalia.” (Al-Bukhariy na Muslim).
Na alikataa kula sungura kwa kuwa imesemwa kuwa anaingia katika siku zake (anapata hedhi), imepokewa kutoka kwa Abdalla bin Amru: kuwa kuna kijana alikuja na sungura aliyemwinda, akasema: “Ewe Abdallah bin Amru, unasemaje? Akasema; aliletewa Mtume na mimi nilikuwa nimekaa, basi hakumla na wala hakukataza asiliwe na akahisi kuwa anapata hedhi.” (Abu Dawud, 3792). Na (kupitia haya) nzi wananikumbusha kuhusu makundi ya watu tunaoishi nao kuwa hawajaona mfano wa kuiga isipokuwa kwa nzi kwa kupitia sifa zilizojawa hapo juu. Na iwapo kuna mtu atajihisi kuwa ana sifa hizo basi namnasihi aiwahi nafsi yake na ajiepushe kuwa na sifa hizi mbaya, na ajirudishe katika hali ya utu (ubinadamu) na kuwa na sifa njema ili ajihisi kuwa na hisia nzuri na utulivu ambao utamzidishia upendo ndani ya moyo wake badala ya kuwa na chuki, kiburi na wasiwasi. Ingawa tabia za watu zilizo kama za nzi hawatopata uongofu isipokuwa ule utakao kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa tabia hizo ni za kijinga zisizo na hisia. Tunamuomba Mwenyezi Mungu asitujaalie kuwa miongoni mwao.
6) Na miongoni mwa sifa za nzi ni kuwa anatua katika kitu chochote, kwenye uchafu, vyakula, miili, vikavu na vibichi, na wala hajali ni wapi katua na wala kujali kachukua wapi na kabeba kitu gani, kwa mfano, tunamuona akiruka kwenye vitu visafi na kuruka pia kwenye vitu vichafu, na inawezekana kutokana na wingi wake (jamii ya nzi) tusiweze kujua ni wapi hasa anapotulia je katika vitu visafi au vichafu (kwenye taka)? Na kwa namna hiyo, kwa kulinganisha na ulimwengu wa watu, wingi wa watu haukisiwi kuwa ndipo ulipo ukweli, ni mara ngapi tumeshuhudia uongo ukizungukwa na watu wengi kama nzi anavyozunguka uchafu? Na mara ngapi tumeona ukweli unakaribia kutofuatwa na yeyote, Mwenyezi Mungu anasema {Sema: Haviwi sawa viovu na vyema ujapo kupendeza wingi wa viovu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, ili mpate kufanikiwa } (AL MAIDAH,100)
Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “Nilioneshwa umma nikaona Mtume yu pamoja na kundi la watu wachache, na Mtume mwengine ana mtu mmoja au watu wawili (hivi) na Mtume mwengine hana yeyote.” (Al-Bukhariy na Muslim 5752). Lakini ukweli utabaki kuwa ni ukweli hata kama haufuatwi na yeyote, na batili ni batili hata kama itafuatwa na wengi. Hii ni sheria (msingi) ambao umekuwa ni sehemu ya majadiliano kwa watu wengi pamoja na kuwa kuna hatari kubwa, na kuacha kuutekeleza basi kutasababisha madhara mengi.
7) Na kupitia nzi inanikumbusha ustaarabu wa kiisilamu na ustaarabu mwengine, kwani tunaona katika ustaarabu wetu na urithi wetu kuna vitu vyenye kutukinga na nzi vilivyotengenezwa kwa kutumia nywele za farasi, na kujiepusha nae mara nyingi huwa kwa mkono (kumfukuza nzi), au unaweza kumuua iwapo yu karibu. Ama zana za wenzetu zimetengenezwa kwa plastiki – na zimeenea kwa kuwa tumeacha utamaduni wetu wenye upole kwa watu na kwa viumbe wengine – na zana hizi huua moja kwa moja, na zana zetu huwa haziumizi hata kiungo, ama zao huwa zinaumiza viungo. Na nadhani jambo hili linatkiwa kuangaliwa tena kwa undani zaidi.
8) pia nzi ananikumbusha kupitia macho yake yenye kuchunguza – ambayo huona pande zote – kuwa muumini asiwe na tabia ya kuchunguza yasiyomuhusu na kuingilia mambo ya wengine, mwenyezi Mungu anasema, {Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za wanayo yafanya }(Anuur;30) na akasema {Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur'ani anayeliogopa onyo.}(QAAF;45). Na akaendelea kusema {Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao.}(AN NISAA;80)
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Chanzo : Kitaab Simaat Al Asri, Mufti wa Misri, Proesa Ali Juma