Wasia wa Wajibu.

Egypt's Dar Al-Ifta

Wasia wa Wajibu.

Question

Je, Kanuni ya wasia wa wajibu inaafikiana na sheria?
Na je, Utekelezaji wa wasia huo unategemea idhini ya warithi?
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Sheria imeweka wasia kuwa ni Sunna ili mtu aweze kuyawahi yaliyompita katika maisha yake yaliyotangulia na ayafikie kwa kuwasaidia wenye kuhitaji na wengine, kwa hiyo; wasia kwa ujumla ni Sunna kwa Jamhuri ya wanazuoni na sio wajibu wa kidini isipokuwa pakiwepo haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu au ya waja wake basi wasia huwajibika kwa lengo la kutekeleza wajibu huo.
Na wanazuoni wa sheria ya kanuni wamekuta kwamba zipo hali za kijamii zinahitajika kwa kutatuliwa kwa kikanuni kwa njia ya wasia wa wajibu, kwani katika hali nyingi anakufa mmoja wa watoto akimwacha baba yake au mama yake. Na lau yeye angelikuwa ameishi baada yao angelirithi fungu la mali yao analoliacha kwa watoto wake lakini yeye ametangulia kufariki dunia basi anakuwa peke yake kwa urithi wa baba, au Mama ndugu wa mtoto aliyefariki na watoto wa marehemu hawarithi chochote katika mali ya babu yao au bibi yao, kwani wao ama wawe wanawekewa kikwazo au wawe miongoni mwa wenye udugu wanayoahirishwa katika urithi kuliko zaidi wenye faradhi na ndugu wa karibu wa upande wa baba. Kwa hiyo, watoto hao wamekuwa katika ufakiri dhahiri ambapo wengine wamekuwa katika utajiri dhahiri kwa sababu ya urithi huo. Na uwiano wa ugawaji wa utajiri unakuwa na mgongano katika familia moja, pamoja na kwamba mali hii yote ambayo iliachwa na babu au bibi inaweza kuwa ni kazi ya mtoto huyo aliyekufa na ni matokeo ya juhudi zake, au inaweza kuwa kwa uchache yeye alishirika kwa fungu.
Familia ilikuwa ikitatua suala la wajukuu hawa kwa kuwawekea wasia kwa kile kinachorithiwa na baba au mama yao kama angelikuwa hai au kwa njia ya zawadi na mfano wake, wakati ambapo baadhi ya familia hazifanyi hivyo kwa kuathiriwa na viathiri vya mpito au kwa kuwa mauti yamemjia babu au bibi kwa kasi kabla ya kufanya hivyo.
Basi kanuni ya wasia nambari ya 71 kwa mwaka wa 1946, iliyotekelezwa kuanzia mwanzo wa mwezi wa Agusti, mwaka wa 1946, imekuja na imelitatua jambo hilo kutatua kwa kanuni yenye ulazimisho, imetegemea waliyoiafikiana baadhi ya wanazuoni wa kifikhi, kutoka ulazima wa wasia kwa wazazi wawili na ndugu wasiorithi kwa kuwapo kinachowazuia au kuwawekea kikwazo cha kurithi.
Kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mmeandikiwa -- mmoja wenu anapo fikwa na mauti, kama akiacha mali -- afanye wasia kwa wazazi wake na jamaa zake kwa namna nzuri inayo pendeza. Ni waajibu haya kwa wachamngu.} [AL BAQARAH 180]. Basi Imamu Atwabariy akasema katika tafsiri ya aya hiyo: "Na iwapo atasema msemaji: je ni faradhi kwa mtu mwenye mali ausie kwa ajili ya wazazi wake na jamaa zake ambao hawarithi? Itasemwa: Ndio. Na akisema: Na ikiwa yeye atapindukia katika jambo hilo akawa hajausia kuhusu wao je atakuwa mpotezaji wa faradhi ambayo anahisi ugumu wa kuipoteza? Ikasemwa ndiyo,
Basi iwapo atasema: Dalili gani juu ya hayo? Basi itasemwa ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mmeandikiwa -- mmoja wenu anapo fikwa na mauti, kama akiacha mali -- afanye wasia kwa wazazi wake na jamaa zake}. Basi ujue kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu akatufaradisha juu yenu kama alivyosema: {Mmeandikiwa -- mmoja wenu} [AL BAQARAH 183].
Na wala hakuna tofauti kati ya wote kwamba mwenye kuacha funga wakati ana uwezo wa kufanya hivyo anapoteza faradhi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kufanya kwake hivyo na vivyo hivyo kwake kwa kuacha wasia kwa ajili ya wazazi wake kwa hivyo ana yeye kwa anachokiusia kwa ajili yao upotevu wa faradhi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu." [Tafsiri ya Atwabariy 385/3, Ch. Mu'sasat Ar Resalah].
Imamu Ibn Hazm akasema: "Ni faradhi kwa kila mwislamu ausie kwa ajili ya ndugu zake ambao hawarithi ima kwa utumwa au kwa ukafiri au kwa kuwa kuna wanaowazuia wasirithi au kwa kuwa wao hawarithi, basi akausia kwa ajili yao kwa utashi wa nafsi yake mwenyewe hakuna adhabu katika hilo, na ikiwa hakufanya hivyo wao watatoa na hapana budi kwa kile walichokiona warithi au mwenye jukumu la kutekeleza wasia." Kitabu cha: [Al Mahaliy kwa Ibn Hazm 353/8, Ch. Dar Al Fikr].
Na Ibn Qudamah akataja katika kitabu cha: [Al Mughniy]: Nani aliyesema kwa uawajibu wa wasia? Akaseama: "Abu Bakr Bin Abdulaziz akaseam: wasia ni wajibu kwa ndugu ambao hawarithi, na hiyo ni kauli ya Dawud, na imesimuliwa hayo kutoka kwa Masruoq, Twaus, Iyaas, Qatadah na Ibn Jarer, walitegemea kwa aya na habari ya Ibn Omar, na wakasema kuwa: "Wasia umefutwa kwa wazazi wawili na ndugu wanaorithi na ukabakishwa kwa wale wasiorithi miongoni mwa ndugu." [Al Mughniy 137/6, Ch. Maktabat Al Qahirah]
Na Abu Bakr Al Jassass akasema: "Watu wanahitilafina katika wasia unaotajwa katika aya hiyo, je, ulikuwa ni wajibu ama sio? Basi baadhi yao wakasema: Hakika ya wasia haukuwa lazima isipokuwa ulikuwa Sunna yenye nguvu na ni mwongozo, na wengine wakasema: wasia ulikuwa faradhi kisha ukafutwa kwa mujibu wa tofauti zao wanazuoni kwa kile kinachofutwa." [Ahkaamu Al Quraan kwa Al Jassass 202/1. Ch. Dar Ihyaa At Turaath Al Arabiy]
Na Atwabariy akapinga kauli kwa kufuta kwa aya na akasema: "Kama akisema kwamba: umejua kuwa kundi kutoka wanazuoni wakasema: Je Wasia kwa wazazi na ndugu umefutwa kwa aya ya mirathi? Akaambiwa hivyo: na kundi jingine lisilokuwa wao likatofautiana nao na kusema: hiyo ni katika aya za hukumu na wala haijafutwa." [Tafsiri Atwabariy 385/3]
Sheria ikapelekea kujuzu kwa kuiga kwa kauli hizi ambazo zinazungumzia uwajibu wa wasia wa lazima, sheria ikaegemea pia katika madaraka ya uwajibishaji aliyonayo mlezi wa mtoto kwa mujibu wa msingi wa kisheria unaosema kuwa mlezi aamrishe kilicho halali kwa kuwa kwake na masilahi, na wakati wowote anapoamrisha hivyo ni lazima kumtii.
Na kauli yake kuwa wasia ni wajibu kwa mtoto wa mtoto aliyefariki ambaye amekufa katika maisha yake, iwe kihukumu au kiuhalisia, vyovyote atakavyokuwa mtoto huyo hata kama atakuwa ni katika watoto wa migongo, na kwa tabaka ya kwanza miongoni mwa watoto wa wasichana, yaani kuwa wasia unalazimika kwa wajukuu hata walikuwa wakishuka, lakini hawastahiki wasia huo isipokuwa watoto wa wasichana tu na sio wajukuu wao.
Kama ambavyo wasia unakuwa lazima kwa mtoto aliyefiwa na baba yake au mama yake kwa namna ambayo hajui aliyekufa miongoni mwao kama kufa kwa kuzama majini, au kufa kwa kuungua moto au kwa kuangukiwa na jengo kwani hawa hawarithiani.
Basi tawi halirithi asili yake katika hali hiyo, kwa hiyo hali yake inakuwa kama ya yule aliyekufa kabla ya baba yake au mama yake, na hawa ndio watu wa wasia ulio wajibu kisheria, na pindi mtu anapouusia basi lazima utekelezwe. Na hata kama hakuusia basi sheria itauanzisha wasia katika mali ya marehemu, na akiusia kwa baadhi ya wenye haki na kuwatenga wengine hivi punde, basi sheria itauanzisha wasia kwa wale ambao hawakupata wasia.
Na sheria imeweka kiwango cha wasia wa lazima ni fungu analolistahiki mtoto wa marehemu kama angelikuwa hai hadi mzazi wake akafa katika mipaka ya theluthi moja ya mirathi na sheria imefupisha uwajibu katika theluthi moja kwani uwanja wa utekelezaji wa wasia kisheria kwa kuwaunga warithi ni theluthi moja tu hakizidi kitu isipokuwa kwa utashi wao.
Na Inashurutiwa kuujuzisha wasia kwa yafuatayo:
Ya Kwanza: Basi wao lazima wasiwe warithi na ikiwa watastahiki mirathi iwe kidogo au kingi pasi hawana fungu katika wasia kwani wasia huwa ni kama mbadala wa kinachopita katika mirathi, na wasia katika hali hii utakuwa kwao ni chaguo lenye hukumu zake.
Ya Pili: Asiwe marehemu huyo alikuwa ameshawapa kiwango kinacholingana na cha wasia wa lazima bila ya mbadala kwa njia ya kutoa kama zawadi na mfanowe, na ikiwa aliwapa kiwango kilicho chini ya wasia basi wasia kwao ni lazima ili wakamilishe sehemu ya lazima iliyobaki, na ikiwa amewapa wenye kustahiki chini ya sehemu yake katika fungu lililobaki la theluthi moja na kinachokuwa nyongeza katika fungu la aliyeusiwa naye. [Al Ahkaam Al Asasiyah Lel Mawariith wa Al Wasia Al Wajibah fe Al Fiqh wal Qanun Lel Daktoor Zakariya Al Biriy, Uk. 234/235].
Na wasia wa lazima sio mirathi na wala ndani yake hauna mabadiliko ya hukumu za mirathi isipokuwa ni wasia unaokubalika na uliowajibishwa na sheria kwa kuwa kwake na masilahi, na ndani yake kuna sifa maalumu za wasia kwamba wasia huo ni utangulizi wa mirathi, na kwamba haupindukii theluthi moja. Na ni tofauti na mirathi na kwamba hautekelezwi ikiwa marehemu alimpa mwenye kustahiki bila ya kiwango mbadala wanachostahiki tofauti na mirathi katika haki hiyo na kwamba kila asili huzuia tawi na tawi la mwingine.
Na ikiwa sheria inaanzisha hata kama mtoa wasia hakuanzisha yeye, na atagawa kwa wenye kustahili, mwanaume atachukua mafungu mawili zaidi ya mwanamke na hizo ni baadhi ya hukumu za mirathi na kwa hali hiyo hakuna dalili inayoonesha kuwa hiyo ni mirathi kwa kuwepo tofauti kati yake. [Al Ahkaam Al Asasiyah Lel Mawareeth wa Al Wasia Al Wajibah fe Al Fiqh wal Qanun Lel Daktoor Zakariya Al Biriy, Uk. 233]
Na sheria imeeleza kuwa utekelezaji wa Wasia ni Lazima hata bila ya warithi kukubali. kwa mujibu wa hali hii, hakika sheria ya wasia ulio wajibu hakuna kwenda kinyume na sheria ndani yake bali ni kinyume chake, wasia unaenda sambamba na sheria ya Kiislamu na ni kutokana na kauli za Wanazuoni na wajuzi wa Fiqhi. Na hata kama haikuwa Ijmaa ya wanazuoni wa Fiqhi, isipokuwa kadhi au mtawala anaweza kuchagua miongoni mwa rai za wanazuoni wa Fiqhi ile inayoleta masilahi kwake na kwa kufanya hivyo ataondosha hitilafu iliyopo, kwani maamuzi ya kiongozi huondosha hitilafu na kwa hivyo Mahakama imewajibisha wasia kwa wajukuu hawa kuzipangilia hukumu zake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas