Hadithi ya Kuihifadhi Qur'ani

Egypt's Dar Al-Ifta

Hadithi ya Kuihifadhi Qur'ani

Question

Wengi wa wahubiri wa dini wanatangaza Hadithi ambayo wanaiita: Hadithi ya kuhifadhi, kwa anyetaka kuihifadhi Qur'ani, nayo ni Sala mahususi mwishoni mwa usiku wa siku ya Ijumaa, ambayo inakaririwa mara tatu, tano, au saba. Je, nini usahihi wa kuutekeleza usia huu? 

Answer

Sifa njema za Mwenyezi Munugu, na rehema na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, Aali zake, Masahaba zake na waliomfuata, na baada ya hayo:
At-Tirmidhiy na Al-Hakim wamepokea kutoka kwa Ibn Abbas kuwa alisema: Wakati tuko hapo na Mtume S.A.W., Ali Ibn Abi-talib akisema: Ewe mpendwa wangu mama baba na mama, hii Qur'ani imekwenda kutoka kwa kifua chanu, hata siwezi kuikumbuka, na Mtume S.A.W., alisema: “Ewe baba wa Al-Hasan, je, ninakufundisha maneno, Allah akunufaishia wewe na uliyemfundishia na kuthibitisha ulivyojifunza katika kifua chako? Akasema Ali: Ndiyo Mtume wa Allah nifundishe. Akasema Mtume: Ikiwa usiku wa Ijumaa, ukiweza kusimama kwa kusali katika theluthi ya mwisho wa usiku, ambapo hii ni saa inayoshuhudiwa, na dua ndani yake ikubalike, na ndugu yangu Yaaquubalisema kwa wanawe: Nitakuombeeni msamaha kwa Mola wangu; anasema:
Mpaka ukafika usiku wa ijumaa, na kama usipoweza, simama katikati ya usiku, au mwanzoni mwake, hapo Sali rakaa nne, unasoma Fatiha ya Kitabu katika rakaa ya kwanza na Surat Yasin, nakatika rakaa ya pili Fatiha ya Kiotabu na Haa Mym Ad-Dukhaan, na katika rakaa ya tatu Fatiha ya Kitabu na Alif Lam Mym Tanziil As-Sajdah, nakatika rakaa ya nne Fatiha ya Kitabu na Tabarak Al-Mufassal, na ukimaliza Tashahud shukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema zake, na nisifu sifa nzuri pamoja na Manabii wote, na omba msamaha wanaoamini wanaume na wanawake, na ndugu yako waliokutangulia katika imani, kisha sema mwishoni mwa hayo yote: Ewe Allah, nirehemu ili niache dhambi siku zote nikiishi, nirehemu ili nisitafute yasiyonihusu, niruzuku mtazamo mzuri kwa ajili ya radhi yako juu yangu; Ewe Mola Muumbaji wa mbingu na ardhi mwenye utukufu na ukarimu na enzi isiyo ya mfano, nakuuliza Ewe Allah, Ewe Rahman kwa utukufu wako na nuru ya uso wako uangaze macho yangu kwa Kitabu chako, na usemeze kwake ulimi wangu, na ufariji kwake moyo wangu, na upanulia kwake kifua changu, na uoshe kwake mwili wangu, kwa sababu hakuna ye yote asaidie haki isipokuwa Wewe na wala hatoe isipokuwa Wewe na hakuna nguvu wala uwezo ila kwa Allah aliye juu na aliye mkuu.
Ewe Abal-Hasan, fanya hivi muda wa jumaa tatu , tano, au saba, baadaye utapata jibu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, naapa kwa aliyenituma kwa haki jambo hilihalikumkosea muumini katu. Ibn Abbas alisema: Naapa kwa Allah, Ali hakungojea ila tano au saba, hata aje kwa Mtume S.A.W., katika kikao hico hicho, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, siku zilizopita nilikuwa sichukui isipokuwa Aya nne tu au mfano wake, kisha nikijaribu kuzisoma sikuzikumbuka, lakini sasa hivi najifunza Aya arobaini au mfano wake, na nikijaribu kuzisoma kama kwamba Kitabu cha Mwenyezi Mungu iko mbele ya macho yangu mawili, kadhalika nilikuwa nikisikia Hadithi na nikijaribu kuisoma tena ikaenda, lakini sasa hivi, Nasikia Hadithi na nikijaribu kuzisoma, sikusahau herufi moja.
Hapo mtume S.A.W., akasema: Naapa kwa Mola wa Kaaba wewe ni muumini, ewe Abal-Hasan”.
Hadithi hii ni dhaifu, na Al-Aqiliy aliitaja katika kitabu cha: [Ad-Dhua’afaa], na Ibn As-Sunniy katika kitabu cha: [A’mal Al-Yaum Wal-Lailah], na Al-Baihaqiy katika kitabu cha: [Al-Asmaa Was-Sifaat], na katika kitabu cha: [Ad-Daa’waat Al-Kabiir], na Ibn A’saakir katika kitabu cha: [Juzuu Akhbar Li-Hifdh Al-Quran Al-Kariim], na Ad-Diyaa Al-Maqdisiy katika kitabu cha: [Al-Ahadith Al-Mukhtarah], na Al-Mundhiriy katika kitabu cha: [At-Targhiib Wat-Tarhiib], na Ibn Kathiir katika [Fadhail Al-Quran], wote kutoka kwa njia ya Al-Waliid Ibn Muslim.
Hadithi pia ina Isnsd nyingine ya At-Twabaraniy katika kitabu cha: [Al-Mu’jam Al-Kabiir], na ina Isnad nyingine bila ya kutaja sala, kutoka kwa Abid-Dardaa katika Juzuu ya Ibn Asaakir, inayoitwa [Akhbar Hifdh Al-Quran], Ibn Al-Jawziy aliitaja katika kitabu cha: [Al-Madhua’at], na As-Sayutiy alieleza katika kitabu cha: [Al-Jamii’ As-Saghiir] akisema: “na Ibn Al-Jawziy aliitaja katika Al-Maudhua’at, lakini hakuwa na kweli”.
Ash-Shawkaniy katika kitabu cha: [Al-Fawaid Al-majmua’h] anasema: “Ameipokea Al-Hakim na kusema: Ni sahihi kwa masharti ya Bukhariy na Muslim, lakini kauli hii ya Al-Hakim haikubaliki, kwa sababu hadithi hii ni chini ya Hasan, na chini sana ya sahihi, pamoja na maneno yake si ya kawaida”. [Al-Fawaid Al-Majmua’ah Fil-Ahadith Al-Maudhua’ah; 1/42, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Al-Mundhiriy katika kitabu cha: [At-Targhiib Wat-Tarhiib] anasema: “At-Tirmidhiy ameipokea na kusema: Hadithi hasan gharib, hatuijui isipokuwa njia ya Al-Waliid Ibn Muslim, na Al-Hakim ameipokea na akasema: ni sahihi kwa masharti ya Wawili, lakini akasema: anasoma katika rakaa ya pili Al-Fatihah na Alif Lam Mym As-Sajdah, na katika rakaa ya tatu Al-Fatihah na Ad-Dukhaan, kinyume iliyoko katika At-Tirmidhiy, na alisema katika dua: ushughlike kwake mwili wangu, badala ya utumie, nayo ilitajwa hivi katika baadhi ya nakala za At-Tirmidhiy, na maana yake ni moja, na katika nakala nyingine: uoshe, kisha alisema: Njia ya Isnad ya Hadithi hii ni nzuri, lakini matini yake si ya kawaida kabisa, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi wa yote”.
Adh-Dhahabiy anasema: “Ingawa Isnad yake ni nzuri lakini matini yake inakanushwa sana, na nina wasiwasi juu yake, na yumkini Suleiman kuwa na hangaiko, kama alivyosema Abu-Hatim: Suleiman huyu akipokelewa kwa Hadithi maudhui hakuijua”. [Mizan Al-Ii’tidal, na Adh-Dhahabiy: 2/213, Ch. Ya dar Al-Maarifah].
Na Ibn Kathiir katika kitabu cha: [Fadhail Al-Quran] anasema: “Al-Hakim ameipokea katika kitabu cha: (Al-Mustadrak) kutoka kwa Al-Waliid, kisha akisema: kwa masharti ya Bukhariy na Muslim, na hapo hapana shaka kuwa Isnad yake na Al-Waliid inaambatana na masharti ya Wapokeaji wawili, ambapo Al-Waliid alieleza kuwa akisikia na Ibn Juraij, na ni dhahiri kuwa: si ya kawaida na kukanushwa, na mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa yote”. [Fadhail Al-Quran, na Ibn Kathiir: 1/292, Ch. Ya Maktabat Ibn Taimiyah].
Kwa hivyo, Hadithi dhaifu inatekelezwa nayo katika matendo mazuri, na Hadithi hii ya kuihifadhi Qur'ani haipingani na kanuni ya misingi ya Dini, bali inafuata Sheria kuhusu kuelekea Mwenyezi Mungu katika mambo yote, na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Na Mola wenu anasema: “Niombeni nitakujibuni}. [AL MUUMIN: 60], na At-Tirmidhy amepokea kutoka kwa Anas kuwa Mtume S.A.W., alisema: “Dua ni asili ya ibada”, na At-Tirmidhiy, Ibn Majah, Ibn Hibban, na Al-Hakim wamepokea kutoka kwa Abi-Hurairah RA, alisema: Mtume S.A.W., alisema: “Si kitu yenye karama sana kwa Mwenyezi Mungu kuliko dua”.
Na kujuzu kwa kuitekeleza Hadithi dhaifu kuhusu matendo mazuri ni kauli ya Jamaa kubwa ya wanachuoni, miongoni mwao: Imamu Ahmad, Abdur-Rahman Ibn Mahdiy, Ibn As-Salaah, Ibn Taimiyah, Az-Zarkashiy, An-Nawawiy, Al-A’allaniy, na Ibn Daqiq Ali’id, na hao wanafuatwa na wengi wa wanachuoni, kama vile, As-Sayutiy, Al-Haitamiy, na wengineo wengi.
Imamu Ibn As-swalaah anasema: “Inajuzu kwa wanachuoni wa Hadithi kurahisisha katika Isnad na isipokuwa Hadithi maudhui, miongoni mwa Hadithi dhaifu, na bila ya kujali kubainsha ngazi zake, na isipokuwa Hadithi zinazohusu Sifa za Allah Mtukufu, hukumu za Sheria, miongoni mwa Halali na Haramu na nyinginezo, kama vile; Mawaidha, Visa, fadhila za matendo, na aina zote za Targhiib na Tarhiib, na aina zote ambazo haziambatani na hukumu na imani, na miongoni mwa tuliopokelea nao urahisi katika mambo haya ni: Abdur-Rahman Ibn Mahdiy, na Ahmad Ibn Hanbal RA,”. [Muqadimat Ibn As-salaah: 1/103, Ch. Ya Dar Al-Fir].
Kuhusu wanachuoni wa madhehebu ya Hanafiy, nao waliitekeleza na wakaitaka dua hii katika usiku wa Ijumaa, na Ibn Abidiinanasema: “Inatakiwa usiku wa Ijumaa kwa mtu asali ndani yake Sala ya kuihifadhi Qur'ani”. [Tanqiih Al-Fatawa Al-hamidiyah, na Ibn Abidiin: 1/8, Ch. Ya Dar Al-Maarifah], kwa mtazamo wa kuwa: sala hii katika Hadithi mfumo wake haupingani na kusoma Qur'ani, kama ilivyo katika sala ya kawaida, isipokuwa kuainishwa kwa Sura maalum ya kusomwa, kama alivyofanya Mtume S.A.W., mara nyingi, kusoma Suratul Jumuaa na Al-Munafiquun katika Sala ya Ijumaa. [Ameipokea Imamu Muslim, kutoka kwa Abi-Hrairah], na kwa jumla, Sala hii ni kusimama usikuna Dua maalum.
Na kwa mujibu wa hayo: Ingawa Hadithi hii ingkuwa dhaifu, lakini itekelezwe nayo, kwa kauli ya wanachuoni kuwa inajuzu kuitekeleza Hadithi dhaifu katika matendo mazuri.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas