Ugaidi wa Kifikra
Question
Vipi tunafahamu kazi za ugaidi wa kifikra kwa vikundi vya ukufirishaji?
Answer
Mtu wa msimamo mkali hawezi kujenga mjadala wa kiuchambuzi kwa kadhia yeyote ambayo imejikita kwenye mifumo yao, kisha mara nyingi hukimbilia kwenye njia ya ugaidi wa kifikra na kuambatisha tuhuma zilizo tayari kwa wapinzani wa fikra zao, kwa mfano: Ikiwa mtu atapinga msimamo mkali na kumkinaisha kuwa kushirikiana na wengine wasio Waislamu jambo zuri ni katika wajibu wa Sharia ambayo imehimiza kwenye hilo, na akapingana naye katika mafundisho ya chuki na mfano wake, mara nyingi mwenye msimamo mkali hutumia na ugaidi wa kifikra katika huo mjadala, kwa kusema: Hawa ni makafiri, na kile unachojaribu kukithibitisha ni kupingana na hukumu ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Amesema:
{Je, hawajui ya kwamba anaye shindana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi huyo atapata Moto wa Jahannamu adumu humo? Hiyo ndiyo fedheha kubwa} Attawba: 63.
Mwenye msimamo mkali wa kigaidi anajaribu kumbebesha tuhuma mpingaji wa nadhari zake kwa hivyo.
Kutumia alama na ibara zilizochezewa:
Kwa sababu hiyo changamoto za kifikra ambazo anakutana nazo huyo mwenye msimamo mkali zilikuwa ni kubwa sana, maswali kuhusu malengo ya matendo yao na matokeo ya hali wanayoitafuta mara nyingi hawapati jibu la kweli katika akili zao, hivyo ufumbuzi unakuwa ni katika kutumia alama na ibara zilizochezewa na ambazo husaidia msimamo wao na mielekeo ya vikundi vyao.