Uzazi wa mpango

Egypt's Dar Al-Ifta

Uzazi wa mpango

Question

Ni ipi hukumu ya kisharia katika kupanga uzazi

Answer

Kupanga uzazi kwa maana ya kuweka umbali kipindi cha kubeba mimba kwa ajili ya kulinda afya ya mama na kumlinda na madhara kutokana na kubeba ujauzito  na kuzaa  mfululizo, au kuwa na muda wa kulea watoto alionaoa , ni halali kisharia, nalo  linahimizwa na matini za Hadithi tukufu; kwa kulinganisha na kutoa (kumwaga mbegu za kiume nje ya uke) nayo ni moja ya njia ambazo wanandoa walikuwa wakizifanya kwa makubaliano ili kuzuia ujauzito na kupanga uzazi, kama ilivyokuja katika riwaya ya Imamu Muslim katika sahihi yake kutoka kwa Jabir Allah R.A. "Kwamba Masahaba R.A. walikuwa wanatoa (Wanamwaga mbegu za kiume nje ya uke) kwa wake zao na vijakazi wao zama za Mtume S.A.W. na taarifa hiyo ikamfikia Mtume S.A.W. na hakutukataza".

Share this:

Related Fatwas