Uzazi wa mpango.

Egypt's Dar Al-Ifta

Uzazi wa mpango.

Question

Ipi hukumu ya uzazi wa mpango?

Answer

Uzazi wa mpango ni katika mambo muhimu sana ya maisha na Kisharia, kukubaliana kwa wanandoa wawili juu ya kuachanisha vipindi vya ujauzito ili kujenga mustakabali wa familia au kusimamisha kwa muda maalumu kwa lengo hilo hilo limekuwa ni jambo muhimu sana ili kukubaliana kati ya mapato na watoto kwa upande mmoja na wito wa maandiko ya Sharia na makusudio yake kwa upande mwengine, kwani Sharia imelingania swala la kulinda kizazi na ubora wake, na ikahalalisha kujitenga pale inahitajika kufanya hivyo, hilo halipingani na wito wa baadhi ya Hadithi wa kuzaa watoto wengi ndani ya wakati fulani, ambapo makusudio ni kizazi ambacho kitapelekea kufikiwa fahari ya kweli kwa kuelimika kwake wema wa afya yake na wala si kuwa wengi tu.

Share this:

Related Fatwas