Ugumu wa Mateso.

Egypt's Dar Al-Ifta

Ugumu wa Mateso.

Question

Ni namna gani ugumu wa mateso na fikra ya adhabu ya Mungu vimeathiri fikra za vikundi vya misimamo mikali?

Answer

Ugumu wa mateso sifa muhimu ya mtu wa msimamo mkali ili kufikia hali ya kukubaliana kisaikolojia kwake, hilo ni kwa sababu tabia za mtu wa msimamo mkali na fikra zake zinapingwa na kukataliwa sana kwenye mazingira yake yanayomzunguka, hisia hizo mbaya zinafika kwenye mzunguko wa karibu zaidi wa kijamii yake kama vile familia, ili mtu wa msimamo mkali aweze kupata sababu ya hali ya kutengwa na jamii na kwa tabia yake hukimbilia kuamini kuwa mwenye mateso, na hali hiyo ni mwenendo kwa sababu ni mwenye kushikamana na dini yake, na mwenye kushikamana na dini yake ni “Kama kushika makaa ya moto” na kwa kuwa kwake mshika dini basi jamii yake “Yenye ujinga” lazima wamfanyie uadui na kumtesa kila anapopata nafasi.

Hivyo mtu wa msimamo mkali siku zote anahitaji dalili ya Mungu juu ya usahihi wa mwenendo ambao anautumia, na upotofu wa mwenendo ambao unafuatwa na wengine, ni sawa sawa wamekwenda kinyume na yeye katika dini au wamekubaliana, hivyo watu wa msimamo mkali katika kujenga fikra ya adhabu ya Mungu na kuilingania katika hali zote wanakuta dalili nzuri ya ukweli wa maneno yao na mifumo yao, kwa mfano mtandao wa “isis” mwanzoni mwa kuenea kwa virusi vya corona nchini China, kisha ndani ya baadhi ya nchi Barani Ulaya kama vile Italia na Uhispania walitoa maelezo yaliyosema kuwa janga hili ni adhabu kali itokayo kwa Mungu kwa “Mataifa ya kimsalaba” hilo kwa kawaida kabla ya janga kupiga ulimwenguni kote na kuenea katika nchi zote za Kiislamu.

Share this:

Related Fatwas