Bima ya Maisha
Question
Ni nini Hukumu ya Sharia katika Bima ya Maisha?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ofisi ya Fatwa ya Misri imewahi kujibu jambo hilo katika Fatwa yake namba ya 520, tarehe 20 Mfuguo nne, Mwaka 1417H., sawa na 27 Mei; 1997, kama ifuatayo:
Bima kwa aina zake zote ni miongoni mwa matendeano ya kisasa, ambayo hakuna maandiko yeyote ya kisharia yapokelewa kuhusu uhalali au uharamu wake, jinsi ilivyo inafanana na miamala ya mabenki, kwa mujibu wa hayo matendeano yake yanaasisiwa kwa jitihada za Wanachuoni na tafiti zao zinazochukuliwa na matini za Qu`ani Tukufu na Sunna kwa jumla, kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu}. [AL MAIDAH; 2]; na kauli yake Mtume S.A.W: “Mfano wa waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kusaidiana kwao, ni mfano wa mwili, kiungo kimoja kikiumwa, mwili mzima hushirikiana kwa kukesha na homa”. [Ameipokea Bukhariy]. Na Maandiko mengineyo yaliyopokewa katika mlango huu.
Bima ina aina tatu:
Kwanza: Bima ya kupeana:
Inatekelezwa na fungu la watu, au vyama kwa ajili ya kufidia majanga yanayowapata watu.
Pili: Bima ya Kijamii:
Inahusu watu wanaotegemea mapato yao katika kuendesha maisha, dhidi ya majanga yanayowapata, kwa madhumuni ya kudhaminiana kijamii, na mfumo huu ni kwa madaraka ya dola.
Tatu: Bima ya kibiashara:
Inatekelezwa na mashirika ya hisa, yanayoanzishwa kwa lengo hili.
Kuhusu aina ya kwanza na ya pili, zinakaribiana na kauli ya pamoja (Ijmaa) kuhusu mapatano yao kwa Sharia ya kiislamu, kwa sababu hii ni michango ya asili, na kushirikiana katika wema na uchamungu, na kuleta kanuni ya Kudhaminiana kijamii, na kushirikiana kati ya waislamu bila ya kuikusudia faida; na pia hazivurugwi kwa ujinga wala kutoelewa, na ziada iliyopo kati ya malipo ya Bima na hisa haihesabiwi riba, kwa sababu hisa hizi si kwa ajili ya muda maalumu, lakini ni mchango kwa kufidia majanga ya hatari.
Kuhusu aina ya tatu, nayo ni Bima ya kibiashara, pia Bima ya watu, kuna tofauti kubwa kati ya Wanachuoni:
Upande mmoja kati yao unaona kuwa: Aina hii ya muamala ni haramu, kutokana na udanganyifu unaokatazwa, pia huenda iwe na kamari, kuweka dau na riba; upande mwingine unaona kuwa Bima ya kibiashara inajuzu na hakuna linalopinga Sharia ndani yake, kwa sababu hii ni aina ya udhamini wa kijamii, na kushirikiana kwa wema na kimsingi ni mchango, na pia haihesabiwi kama thamani ya kitu.
Upande wa mwisho umetoa dalili yao kwa maandiko ya Qur`ni Tukufu na Sunna kwa ujumla, na pia dalili za kiakili.
Kuhusu Qur`ani Tukufu, kauli yake Mwenyezi Mungu: {Enyi mlio amini! Timizeni ahadi} [AL MAIDAH: 1] Walisema kuwa; neno (Ahadi) linakusanya ahadi zote, miongoni mwake ni Bima na nyinginezo, kama ahadi hiyo ya Bima ingekatazwa, basi Mtume S.A.W angeibainisha, na hali Mtume S.A.W hakuibanisha, basi ujumla wake ndio onaokusudiwa, na ahadi ya bima inaingia ndani ya ujumla huo.
Kuhusu Sunna, imepokelewa na Umar bin Yathribiy amesema: “Nilishuhudia hotuba ya Mtume S.A.W. Minaa, na miongoni mwa hotuba yake: “Si halali kwa Muislamu kuchukua mali ya mwenziwe isipokuwa kwa ridhaa yake”, hivyo basi Mtume S.A.W, amejaalia uhalali wa kupata mali ya mwingine ni njia ya ridhaa, na Bima ni ahadi wanayoridhia pande mbili kwa kuchukua mali kwa njia mahsusi, kwa hiyo ni halali.
Na dalili ya akili kuwa: Bima ni ahadi ya mchango kwa pande mbili, nazo ni: Mtu anayeshiriki kwa kulipa fungu la mali maluumu, na shirika la Bima linalogharimia kiasi cha Bima, na hayo yote kwa kusudio la kugawana hatari, na kusaidia mewenye janga, kwa hiyo hakuna linalokatazwa kisheria.
Pia wametoa dalili ya mila na desturi kwa sababu watu wamezoea kutendeana kwa aina hii ya ahadi, na mila na desturi ni miongoni mwa machimbuko ya Sharia kama ijulikanavyo, na mfano wake pia masilahi ya kawaida. Zaidi ya hayo, kuna mahusiano mbali mbali kati ya Bima ya kibiashara na aina mbili nyingine nazo ni ya kupeana na ya kijamii, na mahusiano yanayohusisha na hukumu ile ile, kwa hiyo inakuwa halali.
Mkataba wa Bima ya maisha, ni moja ya mikataba ya kibiashara, si miongoni mwa mikataba yenye kasoro iliyoharamishwa, kwa sababu ni mchango na si thamani ya kitu; na kasoro ndani yake haipelekei ugomvi kati ya pande zake, kwa wingi wa kutendeana nayo na kuenea kwake katika nyanja zote za kazi za kiuchumi, na kile walichokizoea watu na kukiridhia watu bila ya kuwepo ugomvi kinakuwa hakikatazwi. Kanuni za kisheria zimekubali kuwa mikataba ya michango haidhuriki na kasoro nyingi, kinyume na mikataba ya thamani ya kitu ambayo inaweza kukubali kasoro chache, [1].
Kasoro inaweza kuwepo ikiwa mkataba ni kati ya mtu binafsi na shirika la bima, lakini kwa sasa Bima imeingia katika nyanja zote za kiuchumi, na mashirika ya Bima yamekuwa na madaraka ya kuweka bima ya pamoja kwa wafanya kazi wake, na kila mwenye hisa anajua tangu mwanzo kiasi atakacholipa, na pia atakachopata, kwa hiyo haifikiriwi kuwepo kasoro ya jeuri inayokatazwa. Pia katika mkataba wa Bima ya kibiashara kosa la Shubha ya kamari, kwa sababu kamari inategemea bahati, lakini Bima inaanzishwa kwa misingi iliyodhibiti na hesabu madhubuti, licha ya kuwepo mkataba wa kujiandikisha.
Kupitia uchunguzi wa hati za Bima ya kibiashara katika aina zote zinazotolewa na Shirika la Bima la Sharq na mashirika mengine mengi, imedhihirika kuwa kanuni zake nyingi ni misingi ya nidhamu iliyopitishwa na mashirika ya Bima, ikiwa mteja atakubali, basi analazimika kuitekeleza, na misingi hii kwa jumla haipingani na Sharia ya kiislamu. Lakini kuna baadhi ya kanuni lazima zitenguliwe au zirekibishwe ili ziende sambamba na hukumu za Sharia, na maamuzi ya viongozi wa Bima katika taarifa ya mkutano wao chini ya uongozi wa Mufti wa Jamhuri, ndani ya Ofisi ya Fatwa ya Misri, tarehe 25/3/1997, Na hii katika vipengele vifuatavyo:
Kipengele kinaambatana na:
(kurudisha hisa za Bima kamili, akiwa mteja angali hai, mwisho wa muda wa Bima), kipengele hiki lazima kirekibishwe kuwa:
(kurudisha hisa za Bima kamili, akiwa mteja angali hai, mwisho wa muda wa Bima, pamoja na faida zake za uwekezaji, baada ya kupunguza asilimia maaluum kama ada za kazi za kiidara za shirika la Bima).
Kifungu cha kumi inayoambatana na:
(Mteja akipokea barua iliyosajiliwa na Shirika, ya kwamba hakulipa hisa zake katika muda maluum, na hali ya kuwa hisa za miaka mitatu ya kwanza hazikulipwa kabisa, basi mkataba wa Bima huvunjika bila ya onyo, na hisa zilizokwisha lipwa zinakuwa haki ya shirika).
Lazima mada hii irekibishwe na kuwa:
(… makato yanayolipwa yarudishwe kwa mteja, baada ya kumega kiwango kisichozidi asilimia kumi kama malipo ya kazi zilizofanwa na Shirika). ili shirika lisije likachukua mali za wateja bila haki.
Kifungu cha kumi na tatu, kipengele cha kwanza kinachoambatana na:
(Haki ya kudai kiasi cha mali kutokana na mkataba wa Bima itaanguka, kama wenyewe hawakudai, au hawakupeleka shirikani nyaraka zinazothibitisha kifo).
Kipengele hiki lazima kifutwe, kwa sababu haki haiwezi kufutika kamwe, hata wenyewe wasipoiomba. Lakini baada ya miaka kumi ikabidhiwe kwa nyumba ya mali ya waislamu (Akiba ya kusaidia Waislamu).
Kipengele cha pili cha Kifungu cha kile kile:
(… Haki ya wanaofaidika inaaguka kwa kupita muda kwa kufungua kesi mahakamani dhidi ya Shirika la Bima, kwa ajili ya kuziomba haki zinazoambatana na mkataba huu, baada ya miaka mitatu ya kifo).
Kipengele hiki irekibishwe kuwa:
(… Haki inaanguka baada kupita miaka thelathini na mitatu), nao ni muda wa muhula wa kupeleka kesi mahakamani kuhusu haki za kiraia, kwa mtazamo wa Wanazuoni wa sharia ya kiislamu.
Na katika uhalisia wa swali na kwa mujibu wa yaliyotangulia:
Miamala yaliyotajwa pamoja na Bima ya maisha yanajuzu kisheria; kwa sababu Bima katika aina zake zote imekuwa na ulazima wa kijamii na inayoambatana na hali ya maisha, na haiwezekani kuiacha, kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wafanyakazi viwandani na mashirika ya kiuchumi, ikiwa ni binafsi au ya umma. Hivyo mashirika yatakuwa yanalinda mtaji, ili kufanya kazi yake katika kulinda uchumi, nao ni uti wa maisha, na kulinda wafanyakazi kwa madhumuni ya kutuliza maisha yao kwa sasa na siku zijazo, na si kwa kusudio la faida au mapato yasiyo ya kisharia, lakini ni kushikamana, kudhaminiana na kushirikiana katika kuepusha madhara ya ajali na majanga. Kwa hiyo Bima siyo kodi inayolipwa kwa nguvu, lakini ni kushirikiana katika wema na upendeleo, na mambo kama hayo ni miongomi mwa maamrisho ya Uislamu, pamoja na kuangalia vipengele vivyotangulia.
Nchi mbali mbali ulimwenguni zimeutumia mfumo wa Bima kwa ajili ya kukuza mataifa yake na maendeleo ya rai wake, na Uislamu haujaufunga mlango kwa wafuasi wake kuhusu mfumo wa Bima, kwa sababu ni dini ya maendeleno, ustaarabu na nidhamu, hivyo Wanachuoni wa Waislamu tangu zamani na sasa katika mataifa yote ya ulimwengu wa kiislamu waliijuzisha na kuhalalisha, na wana dalili zao ambazo baadhi yake tumezitaja.
Na Ofisi ya Fatwa ya Misri inaona kuwa: Hakuna katazo la kisharia kuitekeleza mfumo wa Bima kwa aina zake zote, na tunatumaini kuipanua zaidi iwezekanavyo, ili iwafikie watu wote wasiokuwa na Bima. Na iwe kwa makato ya kila mwezi au mwaka kwa kiasi cha fedha kinachokubalika, na iwe ni lazima ili watu wote wazoee kuweka akiba na kusaidia, kwa lengo la kurejea kwao faida zao walizoziwekeza zikiwa na vitegauchumi vyake vyenye kuwanufaisha wao na nchi zao. Mataifa yaliyoendelea na jamii zenye nzuri zinafundisha vijana wake kupenda kuweka akiba na kufanyia kazi yanayowanufaisha wao katika dini yao na kwa maisha yao ya baadaye.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
[1] . Al-Furuuq na Al-Qarafiy, Ch., ya Dar Ihyaa’ Al-Kutub Al-Arabiya, Mwaka 344H., Vol.1, Uk. 151; tu Hashiyat Ibn Abidiin, Vol. 5, Uk. 416-429; Al-Qawaid Al-Fiqhiya, na Ibn Rajab (Msingi wa tano baada ya mia); Al-mausua’ Al-fiqhiyah; Herufi /gh/, Kidahizo: /gharar/, vol.31, Uk. 160].
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
