Ndoa ya Misyaar
Question
Je, Ndoa ya Misyar ni halali au Haramu?
Answer
Ndoa ya Misyar inaruhusiwa na halali ndoa itakapofungwa na kutimiza nguzo na masharti yanayozingatiwa na Sharia, kama vile ijaabu (makubaliano ya kuoana), kuwepo kwa walii, mashahidi na mke na mume kusalimika na vizuizi vya kisharia. Na kuacha baadhi ya haki zake kwa mwanamke hakuathiri uhalali wa mkataba wa ndoa, kwa sababu anamiliki haki hiyo, kwa hivyo inaruhusiwa kwake kuiacha, zaidi ya hayo, hakuna udhalilishaji wa mwanamke au mwanamume katika ndoa ya Misyar, bali inaonyesha kiwango cha upana wa Sharia na uwezo wake wa kukidhi mahitaji ya roho ya mwanadamu, na hilo kupitia tatuzi mbalimbali zinzozuia kuanguka katika dhiki ya kisaikolojia au kuingia katika yaliyoharamishwa na sharia.
Maelezo
Katika ndoa ya misyaar, ndoa inafungwa, ikitmiza masharti na nguzo zake za kisharia kama tamko la ndoa, kuwepo walii na mashahidi na wanando kutokuwa na vizuizi vya kisharia, ila mwanamke anaafikiana na mumewe kusamehe haki yake ya makazi na kupata matumizi au moja yao na mwanamke anatosheka mume kuwa anakuja kwake badhi ya siku.
Fatwa iliyotolewa na Ofisi ya kutoa Fatwa ya Misiri inasema kwamba ndoa hiyo inajuzu na ni halali mradi tu ndoa inafungwa, ikitmiza masharti na nguzo zake za kisharia zilizotajwa hapo juu. Kwa hivyo, haki zote zinazotokana na mkataba wa ndoa zinastahiki kwa mkataba huu kwa upande wa nasaba, urithi, Eda[1], talaka, na haki zingine, mwanamke kusamehe baadhi ya haki zake hakuathiri uhalali wa mkataba. Bali, mkataba ni halali, na sharti batili ni batili, kama walivyosema wanazuoni[2].
Ndoa ya misyaar siyo mpya katika Fiqhi ya Kiislamu lakini jina lake ndilo jipya na aina hiyo ni ya zamani ambayo ilikuwa inajulikana kwa jina la ndoa ya “NAHARIYAT AU LAYLIYAT (Mchana mchana au Usiku usiku”)”, na ndoa hiyo ni halali kwa rai za baadhi ya Wanazuoni[3].
Swali linakuja: Je. Inajuzu kwa mwanamke kusamehe baadhi ya haki zake katika mkataba wa Ndoa?
Jibu ni Ndiyo, inajuzu kwa mwanamke kusamehe baadhi ya haki zake, kwani yeye ndie anayemilikia haki hizo, na dalili ya kujuzu huko ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mwanamke akichelea kutupwa na kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekwa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamchamungu basi hakika Mwenyezi Mungu Anazo khabari za yote mnayoyatenda} {AN-NISAA, 128}.
Imepokewa Hadithi kutoka kwa Mama wa Waumini Bi. Aisha R.A ya kwamba sababu ya kushuka kwa Aya hiyo ni: “Mume anakuwa na mke hali ya kuwa amemchukia hamtaki anataka kuachana naye, na mkewe amwambie: “nakupa uhuru wa kuniacha”, basi ikashuka Aya hiyo katika suala hilo[4]”
Na kutoka kwa Ibn Abass R.A. amesema: “Bi. Sauda alihofia kuachwa na Mtume s.a.w. akamwambia: usinipe talaka niache niishi nawe na siku yangu mpe Bi. Aisha, basi Mtume (S.A.W) akafanya na hivyo ikashuka Aya: (basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora)[5]”
Haikuwa sahihi kudai kwamba aina hii ya ndoa ni batili kwa sababu inapingana na malengo ya sharia ya Kiislamu kuhusu ndoa, kama vile kupata utulivu, mapenzi, na utunzaji wa watoto. Hii ni kwa sababu hatusemi kwamba aina hii ya ndoa ndiyo ndoa bora, lakini kushindwa kufikia malengo yote yanayotarajiwa ya ndoa hakubatilishi mkataba au kubatilisha ndoa.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kwamba Ndoa ya Misyar inaruhusiwa ikiwa mkataba umekamilika kwa mujibu wa nguzo na masharti yanayozingatiwa na Sharia, na hakuna kizuizi cha kisharia kwa mwanamke kusamehe baadhi ya haki zake ili mwanamume kuja nyumbani kwake wakati wowote anaotaka, mchana au usiku.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
[1] - “Eda": Kipindi cha muda ambacho mwanamke husubiri na kukaa katika nyumba ya ndoa baada ya kutengana na mumewe kutokana na talaka au kifo.
[2] Al Mughniy” Ibn Qudamah, 94/7].
[3] - Fat-hu Al Qadiir, cha Alkamal Bin Al Hamam, 249/3
[4] Imepokolewa na Al Bukhariy
[5] Imepokelewa na Al Bukhariy
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
