Kuchukua Maoni ya Madhehebu ya Dhahiriya.
Question
Kwa wanazuoni wa fiqhi wa Dhahiriya wana maoni yao katika masuala ya kifiqhi ambayo huafikiana na madhehebu moja miongoni mwa madhehebu manne, na pengine hukhitalifiana nao katika maoni mbali mbali. Na Dhahiriya huwa na maoni yao peke yao ambayo hayakutanguliwa na wengine. Je, inawezekana kufuata maoni yao katika hali hizi au hapana?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Sharti la kuzingatia kauli za wanazuoni au kutozingatia, sharti ni kuchukuliwa kauli yenye nguvu na maana yake ni dalili yenye nguvu, na ikiwa dalili hiyo ni dhaifu basi isichukuliwe kwani ni bora pasiwepo na dalili kabisa. As-Seyuty alisema katika sharti hili: (Ni lazima iwe na nguvu na iwe wazi na isiwe dhaifu). [Al-Ashbaha wa Al-Nadhair uk, 137, chapa ya Dar Al-kutub Al-Elmiah]. Na miongoni mwa udhaifu wa dalili ni uendaji kinyume na matini ya Qur`ani Tukufu au kinyume na makubaliano ya wanazuoni kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume}: [AN NISAA: 59]. Na kauli Yake: {Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu}[SURAT AL MAIDA]. Na kauli yake: {Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu.} [ASHSHURA: 10]. Na kauli ya Mtume S.A.W.
(Atakayezua kitu kisichokuwemo katika jambo letu hili kitakataliwa). Na miongoni mwa udhaifu wa dalili pia ni hitilafu kwa kiasi cha wazi na hali ya kuwa kuna kasoro (ila) ndani ya matini au kuna maafikiano katika tafauti baina ya asili na maandiko, na mfano wake ni: uharamishaji wa kuwapiga wazazi kutokana na uharamishaji wa kuwaambia wazazi hao neno lolote la kuwapinga ili kuyazuia maudhi juu yao, na pia kwa Kiasi (Kipimo) cha uwalii wa ndoa juu ya uwalii wa usimamizi wa mali katika uthibitishaji wa uwalii juu ya mtoto kwa sababu ya udogo wake katika hali mbili .
Na wengi wa wanazuoni wa Elimu ya Mizizi ya Elimu waliafikiana kwamba hitilafu katika maoni ya wanazuoni wa Fiqhi kwa Kiasi kilicho wazi ni dalili juu ya udhaifu wa maoni ya Dhahiriya, na hii ni sababu ya kuweza kusimama hukumu ya kadhi akipitisha maamuzi kinyume cha Kiasi kilicho wazi kwani dalili ya Kiasi ni yenye nguvu na ni msingi wa kila hukumu. Na Alzarkashiy alinakili katika kitabu cha: [Al-Bahru] kutoka kwa Abi Is-Haq Al-Isfarayiniy kwamba rai hii ni ya wanazuoni wote. [Al-Bahr Al-Muhit 4\271, Ch. Dar Al-Kutub]. Na kadhalika Abul Abbas Al-Qurtwubiy alitaja katika maelezo yake, katika kitabu cha: [Sahihi Muslim] kwamba wengi wa wanazuoni wa Usuul na wanazuoni wa Fiqhi, wanaafikiana na rai hii. [Rejelea kitabu cha: [Al-Mufham Lima Ushkalu Min Talkisw Kitab Muslim 1\543, Ch. Dar Ibn Kathir wa Dar Al-Qalam At-Twayeb]. Na hii iko wazi kutokana na maneno yao juu ya hitilafu ya wanazuoni wa Madhehebu ya Dhahiriya kwa Makubaliano ya wanazuoni wote, ni kutokuchukuliwa maoni ya Dhahiriya. Na sababu ya hayo ni ugeni wa maoni yao kutokana na maoni ya wanazuoni wote wengine.
Na miongoni mwa dalili ya hitilafu yao ni kiasi kilicho wazi kinachokanushwa kwa msisitizo na Ibn Hazm, na katika sababu hii kadhi Abu Bakr Al-Baqalaniy na Abu Is-Haq Al-Isfirayiniy na Imamu Ag-Gwiniy na mwanafunzi wake Al-Ghazaliy, waliafikiana juu ya kukanusha Kiasi kilicho wazi [Al-Burhan 2\819, kwa Uhakiki wa Daktariy Abdulazim Ad-Dib, na Al-Bahr Al-Muhitw 4\471, 472]. Kwa hivyo inawezekana kabisa kusema kwamba Jamhuri ya wanazuoni wa Usuul walisema kutochukua kila dalili isipokuwa Kiasi kilichowazi.
Na kinachotajwa na AL-Isfirayiny na Al-Qurtwubiy ni kwamba wengi wa wanazuoni wanaendelea kuukana msimamo wa madhehebu ya Dhahiria, na miongoni mwao ni baadhi ya wafuasi wa Madhehebu ya Shafiy kama vile: Al-Nawawiy, Ibn Daqiq Al-Eid, Ibn Abi Hurairah, Abu Al-Hassan Al-Marwiy, Imam Al-Haramin, Abu Hamid Al-Ghazaliy na Ibn Al-Salah. [Tazama: Maelezo ya Al-Nawawiy juu ya Sahihi Muslim 1\142, Ch, Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy na Al-Bahr Al-Muhitw 4\472-474, na 6\291, na Sharhu Al-Imam kwa Ibn Daqiq Al-Eid 1\413, Ch. Dar Atwlas kwa Uchapishaji na Kueneza, na Al-Burhan 2\819, na Fatwa za Ibn As-Swalah Uk. 69, cha Maktabat Al-Ulum wa Al-Hekam na Dar Aalam Al-Kutub]. Na miongoni mwa wanazuoni wa Kimalikiy kadhi Abu Bakr Al-Baqalaniy, Ibn Betwal, Ibn Al-Arabiy na Ad-Darder, [Al-Mufahem 1\543, na maelezo ya Sahihi Muslim kwa Ibn Betwal 1\352, Ch. Maktabat Ar-Rushdiy na Aaredhat Al-Ahwaziy 10\111, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah, na Bughayat As-Salik 2\389]. NA maneno ya Al-Shawkaniy yanasisitiza hivyo: [Rejea: Irshad Al-Fuhul 1\215 Ch, Dar Al-Kitab Al-Arabiy].
Ama kwa Kiasi kilichofichika, wengi wa wasiyofuata Madhehebu ya Dhahiriya katika Kiasi kilichowazi pia wanawakanusha katika Kiasi kilichofichika, na miongoni mwa wanaohitalifiana nao katika mitazamo yake ni Ibn Al-Salah, katika fatwa zake. [1\207] (Alizozichagua ustadh Abuu Mansour katika jambo hilo na alitaja kuwa ni sahihi katika madhehebu hayo kinyume na Abu Sulayman Dawud Al-Asbahaniy – katika fiqhi, iliyothibiti baina ya Maimamu wengi waliochaguliwa hapo baadaye waliyataja madhehebu ya Dawud ili kuthibitisha vitabu vyao maarufu katika Maandiko yaliyoendana na wafuasi wao, na miongoni mwao ni Sheikh Abu Hamed Al-Isfe-irayiniy na rafiki yake Al-Mahamiliy na wengine wengi, (Mwenyezi Mungu awawie radhi). Kwa hakika kama wangekiri hitilafu yake wasingeleta maoni ya madhehebu yake miongoni mwa vitabu vyao hivi kwani maudhui yake ni kinyume cha fikira zao,kwa hivyo nilijibu kwa msaada wa Mwenyezi Mungu kufuata aliyoweka Dawud kutoka madhehebu yake kutokana na asili yake kwa kukanusha kiasi kilicho wazi ambacho kimekubaliwa na wanaofuata kiasi na namna zake au juu ya kiasi kingine kinachotokana na asili yake iliyosimamisha dalili isiyo na shaka, kwani kuwaafiki wengine katika jambo kama hili kwa kinyume chake kinakuwa ni Ijimai\kuafikiana kwa pamoja, na kauli yake (Katika mfano wake unakwenda tofauti na wote..Na maneno ya Ibn As-Subkiy yalipatikana kutokana na yale yanayosemwa na Ibn As-Swalah aliposema katika kitabu chake Al-Twabaqat 2/290, Ch. Dar Hagr]: “Kwa madhehebu ya Dhahiriya kuna baadhi ya masuala ambayo hayachukuliwi kama hitilafu ya Abu Dawud siyo kwa sababu ya asiyeikubali rai yake bali kwa sababu hafuati rai ya Jamhuri ya Wanazuoni, na udhuru wake haujulikani – au kwa sababu ya dalili iliyo wazi sana”. Na dalili yake ni kauli yake hii: “Au dalili iliyo wazi sana”, na siyo kwa sababu ya Kiasi kilichofichika bila mjadala. Na dalili kutoka katika maneno ya Ibn As-Swalah aliposema: “Wanaofuata Kiasi wameafikiana na namna ya Kiasi hicho”, na kiasi kilichofichika siyo miongoni mwa hayo kwa sababu ya hitilafu ya wanazuoni wa Fiqhi katika kila aina miongoni mwa aina za kiasi kilichofichika katika udhaifu mmoja uliopo kwenye asili na ambao umejengewa kiasi, kwa mfano, kuchukua kipimo cha Muuaji wa kukusudia kwa muuaji wa bahati mbaya hakutofautishi kati yao haukataliwi kwa kufuta tafauti hata isemwa kulipa kisasi kwa namna mbili za mauaji, kwa hivyo Al-Imam Abu Hanifia hajakubali uwepo wa kisasi katika mauaji yasiyokusudiwa [Badae’ As-Swanae’ 7/234, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Na maneno ya Ibn Al-Swalah ni afadhali zaidi kuliko yale yaliyotajwa na Jamhuri ya Wanazuoni: kuhusu Kiasi kilichojengwa juu ya udhaifu wa asili, kwani pasingekuwapo kukiri katika matini au kwa yale yanayosemwa na wanazuoni wote kutokana na kauli sahihi inayotokana na dhana, na yanayojengwa kwa dhana ni dhana. Na hakuna haja ya kukikanusha kilichojengwa kwa dhana, kwani hakiwezi kupingana na dalili sahihi, na kwa hivyo As-Shatwbiy anasema katika kitabu chake cha: [Al-Muwafaqat]: “Jambo la kidhana halitoi ushahidi wa asili isiyo na shaka na halipingani na asili isiyo na shak na wala hakuna haja ya kulizingatia”. kwa maana kwamba hakuna haja ya kulitazama kwa lengo la kulifanyia kazi, kwani hakuna dalili ya kidhana kuwa sawa na dalili sahihi .Na haiwezekana kusema kwamba asili ya kiasi haina faida isipokuwa dhana; kwani maneno yanasemwa kwamba Kiasi kilicho wazi ni kutoka namna ya kiasi. na yasiyo miongoni mwa madhumuni ya maneno kwa maana kiasi kiasi kilicho wazi kinathibitisha kutokuwa na shaka, na ni kinyume cha kiasi kilichofichika, kwani kiasi kilichofichika ndani yake kuna dhana.
Na ni lazima kuzindua kwamba yanayotajwa na Dawud katika maneno ya Ibn As-Swalah na Ibn As-Subkiy ni kama mfano tu, na lau mwanafiqhi mwengine angesema kinyume cha anayosema Ibn As-Swalah na Ibn As-Subkiy katika ibara zao mawili, bila shaka isichukuliwe kauli yake na yasichukuliwe kwa kauli hii, kwani yasichukuliwe maneno ya msemaji yakiwa na nguvu au dhaifu; kwani hakuna utukufu kwa watu, wala kuwatazama kwa sifa zao bali kauli yao na elimu yao ni muhimu zaidi, na anayejua zaidi anazingatiwa kwa tofauti yake na lau daraja yake katika ijtihadi ni chini ya anayetofautiana naye, na anayekuwa dhaifu katika elimu yake isichukuliwe kwa tofauti yake na lau daraja yake ya kielimu ni juu, na labda mmoja wao ana elimu zaidi katika baadhi ya masuala zaidi kuliko mwingine bali utukufu wa jambo ni haki ya mtu yeyote.
Na kutokana na misingi iliyotangulia kuelezwa, tunaweza kusema kwamba: Kwa hakika kauli ya wanazuoni wa Fiqhi wa Madhehebu ya Dhahiriya na wengine ikiwa inaitegemea dalili yenye nguvu itakuwa sahihi na kuingia upande wa kuchaguliwa zaidi kuliko mwingine kutokana na nguvu yake, na ikiwa ni dhaifu kwa sababu yoyote hauchukuliwi kuwa ni sahihi. Na wanazuoni wanasema kwamba udhaifu wa kauli si sababu tosha ya kukanusha uchukuaji wa maoni hhaya, kwa hivyo wanajuzisha kuichukua kauli dhaifu katika hali ya dharura au kwa ajili ya masilahi au hata kwa lengo la kuondosha ufisadi, kama anavyosema Ibn Abdiin katika mashairi ya [Ukud Rasm Al-Muftiy 1/43, Ch. Markaz Twawiyat Al-Fiqh Al-Islamiy India]: Haijuzu kuichukua dalili dhaifu ila kwa dharura tu.
Ibn Abdiin amenakili katika maelezo yake, kauli za maimamu kwa kuifanyia kazi iliyo dhaifu, kwa sharti ya kuwa kauli hiyo isiwe dhaifu sana, kwa hivyo anasema kwa kumzungumzia mnywaji wa pombe anadhibiwa kisheria na ni kinyume cha kauli ya Imam Abu Hanifah; kwani dalili za kuharamisha kuadhibiwa mnywaji wa pombe kwa Abu Hanifah hazina nguvu. [Rejea: Mughniy Al-Muhtaj 6/11, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah
Na maoni ya wafuasi wa Madhehebu ya Dhahiriya katika masuala yajayo kwa kiasi kilicho wazi na wanayotegemea juu ya dhahiri kwa kilicho achwa, na mengi miongoni mwa masuala yanayokuwa na maoni yao pekee mbali na wanazuoni wa fiqhi wa madhehebu manne katika kinachotegemewa juu ya kiasi kilicho wazi na hawafuatilii wengine katika masuala haya, kama katika kauli yao ya kujuzu kukidhi haja katika maji yaliyotulia na kauli yao: Hakuna riba ila kwa aina zilizotajwa tu. [Tazama: Al-Mehmaliy 11\124, na 1\145, na 7\401, Ch. Dar Al-Fikr].
Na kwa upande mwingine, labda wafuasi wa Madhehebu ya Dhahiriya katika baadhi ya masuala wanayohitalifiana na wanachuoni wa Fiqhi miongoni mwa madhehebu manne, wanawafikiana na wengine, na wakati huo huo kuichukua kauli yao haimaanishi kuwa ni maoni ya Wafuasi wa madhehebu ya Dhahiriya tu bali ni kwa wengine pia. Lakini inazingatiwa hitilafu yao kwa kiasi kilichojificha; kwani hitilafu hiyo inajengwa juu ya dhana. Ad-Dhahabiy As-Shafiy anasema katika kitabu chake cha: [Sira ya Dawud Ibn Aly Imam Ad-Dhahiriyah]: “Bila shaka katika kila suala ana maoni pekee na anayeukataa ubatili wa kauli yake katika suala hili ni bure, na tunalisimulia kama ni mfano wa kushangaza tu, lakini kila suala lina msingi wake katika matini na kama lilitanguliwa na mfuasi basi litakuwa miongoni mwa masuala ya hitilafu. Na kwa ujumla Dawud Ibn Aly ni mjuzi wa fiqhi, mjuzi wa Qur`ani, amehifadhi Hadithi, kiongozi wa maarifa ya hitilafu, miongoni mwa waalimu, ana uwerevu wa hali ya juu, na ni mtu wa dini. Na kadhalika miongoni mwa wanafiqhi wa dhahiriya kuna kundi lenye elimu na lililoelimika kwa kiwango kikubwa, kwani ukamilifu ni nadra, na Mwenyezi Mungu Amwafikishe. Na anasema kwamba “Na kwa kila hali wao wana vitu vizuri miongoni mwa vitu vyao, na wana masuala yasiyokubaliwa” [Seyar Aamal Al-Nublaa 13\106, 107, Ch. Muasaset Ar-Resalah].
Kwa hivyo tunaweza kusema kuwa kuna uwezekano wa kuyachukua maoni ya wafuasi wa Madhehebu ya Dhahiriya kama yatakuwa na nguvu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.