Kuchukua Msahafu Msikitini
Question
Ipi hukumu ya kuchukua Msahafu kutoka Msikitini?
Answer
Kila kilichowekwa Waqfu kwa ajili ya Msikiti haifai kukichukuwa ni sawa sawa imetolewa ruhusa ya kuchukuwa na anayehusika au haijatolewa ruhusa, na mwenye kuchukuwa Msahafu uliowekwa Waqfu kwa ajili ya Msikiti basi anapaswa kuurejesha, na kama utakuwa umechanika au kuharibika kwa namna yeyote au umepotea basi atalazimika kulipa Msahafu mwingine kama huo na kuuleta Msikitini kisha na atubie kwa Mwenyezi Mungu kwa alichofanya.