Kukata Swala ya Faradhi kwa Udhuru.
Question
Nilikuwa nikiswali swala ya faradhi nyumbani peke yangu, na mtoto wangu mchanga alaikuwa anacheza, akawa anachezea umeme, hivyo mimi nikaamua kukata swala yangu kwa kuhofia madhara yake. Je, nini hukumu ya Sheria kwa niliyoyafanya? Je, Mimi nimepata dhambi kwa kitendo hicho?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huo:
Kukatwa kwa ibada ya faradhi baada ya kuianza bila udhuru halali ni haramu, kwani hali hii ni kuiharibu ibada, na katazo la kufanya hivyo limetajwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika aya ifuatayo: {wala msiviharibu vitendo vyenu [MUHAMMAD: 33].
Imamu An-Nawawi anasema katika kitabu cha: [Al-Majmuu' 2 / 315.317: Dar Al-Fikr]: “Kama Muislamu alianza swala ya faradhi katika mwanzo wa wakati wake hairuhusiwi kuikata pasipo na udhuru, hata ikiwa wakati wake bado, kwa mujibu wa madhehebu yaliyochaguliwa... Dalili ya kukataza kuikata swala ni kauli ya Mwenyezi Mungu: {na wala msiviharibu vitendo yako} [MUHAMMAD 33], dalili hii ni ya ujumla isipokuwa kile kitakachoondoshwa kwa dalili.”
Imetajwa katika kitabu cha Ar-Rawdh pamoja na maelezo yake kwa Ibn Qasim Al-Hanbaliy [3/465, bila ya toleo]: “(Ni haramu kukata faradhi bila ya udhuru). Al-Majd na wengine walisema: Hatujui tofauti katika suala hili. Na alisema katika kitabu cha Al-Fruu: anayeanza wajibu ambayo wakati wake bado, kama vile; kufunga Ramadhani, swala ya faradhi katika mwanzo wa wakati wake, na vinginevyo, kama nadhiri isiyoainishwa, na kafara -kama tukisema inaruhusiwa kuahirishwa- basi ni haramu kuikata bila ya udhuru”.
Inaruhusiwa kuikata swala ya faradhi kwa sababu ya udhuru wa kisheria, kisha hukumu ya udhuru huu ni kati ya kuruhusiwa na kupendekeza na wajibu.
Wanavyuoni wamehesabu sababu zinazoruhusisha kuikata swala ya faradhi: kuua nyoka nk., kuogopa kupoteza yenye thamani kwake mwenyewe au kwa watu wengine, kutoa msaada kwa anayehitaji msaada, kuwatahadharisha mwenye kughafilika au mwenye kulala na kuna hatari isiyoepukika, na haiwezekani kumzindua kwa tasbini, kumwokoa mwenye kuzama, na kumhofia mtoto au nafsi yake mwenyewe, nk.
Kwa mujibu wa kitabu cha: [Ad-Durr Al-Mukhtar kwa Al-Hskafy pamoja na maelezo ya Ibn Abidin 1 / 654.655 Dar Al-Fikr]: “(na inaruhusiwa kuikata) yaani kama swala ikiwa ni faradhi (kwa ajili ya kuua nyoka) yaani kumwua kwa vitendo vingi, (na kutoroka kwa mnyama) vile vile kwa ajili ya kuhofia mbwa mwitu ili asimle kondoo (na kuchemka kwa chungu) inaonekana kwamba jambo hili linategemea kiasi cha hasara inayotokea baadaye, ikiwa yaliyomo kwenye chungu ni yakwake au kwa mwingine (na kupoteza chenye thamani ya dirhamu) alisema katika Mujma Ar-Riwayat: kwa sababu iliyo chini ya dirhamu ni chache sana na hairuhusiwi kuikata swala kwa ajili yake. (Na inapendekeza kuikata swala kwa sababu ya kuizuia haja mbili (kubwa au ndogo)) aidha katika kitabu cha Mawahib Ar-Rahman na Nurul Idhah, lakini suala hili ni kinyume na kile tulichokitoa katika vitabu vya Al-Khazain na Sharhul Maniyah, alisema kuwa kama hali hii inaweka moyo wake mbali na unyenyekevu katika swala, akamaliza swala, basi atapata dhambi kwa ajili ya utendaji wake pamoja na kuchukiza sana, na maana ya hivyo ni kwamba kuikata swala katika hali hii ni wajibu usio pendekezwa ... (na ni lazima) yaani ni faradhi kuikata swala (kwa ajili ya kutoa misaada kwa anayehitaji misaada hii) kama akihitaji misaada hii kutoka kwa asaliye au hakumuamini yeyote. Vile vile, kama kuhofia kuanguka kwa kipofu kwenye kisima, kwa mfano, kama akidhani kuwa bila shaka ataanguka (siyo kwa ajili ya kuita mmoja wa wazazi wake ... n.k) pia inakusudiwa babu au bibi, na dhahiri ya maneno yake ni kwamba alikanusha kwa uwajibu wa kujibu, basi inaruhusiwa kuikata sala. Al-Tahawi alisema kuwa kuhusu swala ya Sunna kama mmoja wa wazazi wake akijua kwamba anaswali na akamwita hakuna vibaya kutomjibu, na kama hakujua inaruhusiwa kumjibu.”
Katika kitabu cha: [Sharhul Manhaj kwa Sheikh Zakaria Al-Ansari maelezo ya Bujayrami 1/246, Al-Halabi.]: “Ni wajibu kumtahadharisha kipofu, kama haiwezekani kumwonya isipokuwa kwa maneno tu au kwa vitendo vianvyobatilisha swala, basi ni wajibu kufanya hivyo. Na swala inabatilishwa kwa vitendo hivi kufuatana na rai iliyochaguliwa”.
Katika kitabu cha: [Al-Mughni kwa Ibn Qudaamah (2/183, Maktabat Al-Qahira.]: “Ahmad alisema: Kama akiona wavulana wawili wanapigana, na ana wasiwasi kwamba mmoja wao ataanguka kwenye kisima, anaruhusiwa kwenda kwao ili kuwatenganisha, na anarudia swala yake. Na alisema: kama mtu aliona moto na alitaka kuuzima, au mwenye kuzama anataka kumwokoa, anaruhusiwa kutoka kwake, na kuanza swala yake baadaye. Kama moto umemfikia, au mafuriko, huko alikuwa akiswali, kama akikimbia, anaruhusiwa kukamilisha swala yake, kama katika hali ya swala ya hofu; kama tulivyotaja hapo awali. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi.
Asili ya suala hili inategemea msingi wa kulinganisha kati ya maslahi na hasara, bila shaka kumwokoa mtu yeyote ambaye maisha yake yana heshima ni muhimu zaidi kuliko swala, pia inawezekana kuchanganya kati ya maslahi mawili kuiokoa roho, kisha kuswali.
Imetajwa katika kitabu cha: [Qawaid Al-Ahkaam Fi Masalih Al-Anaam kwa Imam Ezz Ibn Abdul Salam 1/66, Maktabat Al-Kuliayat Al-Azhariyah] katika mifano ya msingi: kulinganisha kati ya maslahi na hasara ni pamoja na ifuatayo: “Mfano wa Nane: kuokoa maisha ya wenye kuzama ni muhimu zaidi kuliko swala; kwa sababu kuokoa maisha yao ni bora kuliko kuswali, na inawezekana kuchanganya kati ya maslahi mawili yaani kumwokoa mtu mwenye kuzama katika maji, halafu anaswali, na inafahamika kwamba kumwokoa Mwislamu kutokana na kifo ni muhimu zaidi kuliko kuswali”.
Hivyo, kutokana na yaliyotangulia hapo juu, unachofanya na kuikata swala kwa ajili ya kuzuia madhara ya mtoto wako ni wajibu ulio muhimu zaidi kuliko swala, na baada ya hivyo, unaweza kuswali swala yako kama wakati wake bado upo, au unaweza kuiswali baadaye kama wakati wake umemalizika, na hakuna dhambi wala hakuna kitu kibaya.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.