Kuiharibu Saumu kwa Kumwingilia Mke Mchana wa Ramadhani.
Question
Ni ipi hukumu ya mtu aliyeiharibu Saumu yake kwa kumwingilia mke wake katika mchana wa mwezi mtukufu wa Ramadhani? Na je, kuna tofauti baina ya anayeiharibu saumu yake kwa kumwingilia mwanamke na yule anayeiharibu saumu yake kwa kula na kunywa bila udhuru wowote na baadaye kumwingilia mke wake?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Maana ya Saumu Katika Lugha: Ni kujizuia na kujiepusha kufanya jambo fulani. Inasemwa katika kiarabu kwamba saumu ina maana ya kunyamaza au kusimama, ni kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu juu ya ulimi wa mtoto wa Mariam A.S.: {Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu.} [MARIYAM 26].
Ama Saumu inavyotambulika Kisharia:
Ni kufanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa kujizuia na kula, kunywa na kufanya tendo la ndoa kuanzia kuchomoza kwa alfajiri hadi kuzama kwa Jua. [Badaea As-Swanaea Fi Tartib Ash-Sharaea 2\75, Ch., Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Wanazuoni wa Fiqhi waliitaja misingi ya Saumu na kwamba mtu asiyeifuata misingi hiyo, Saumu yake itakuwa imeharibika. Na katika vinavyoiharibu saumu ni tendo la ndoa nyakati za mchana wa Ramadhani. Na Jamhuru ya Wanazuoni wa Fiqhi imesema kwamba muislamu anayeiharibu Saumu yake kwa kuingiliana na mke wake mchana wa Ramadhani bila ya udhuru – na makusudi ya tendo la ndoa ni kuingiliana kwa sura kamili kati ya mume na mke ikiwa ni kwa kutokwa na manii au la – jambo hili linawajibisha kulipa kafara.
Na kulipa kafara huko ni: kuzilipa kwa kuzifunga siku alizoziacha, na kafara hapa ni: ile kafara kubwa “Na kafara kubwa ni kumwacha uhuru mtumwa muumini, na hakuna utumwa kwa sasa baada ya uhuru wa watumwa kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa”, na kwa hivyo basi anafunga siku hiyo na baadaye atafunga siku sitini mfululizo bila ya kula hata siku moja ila kwa udhuru wa kisharia: kama Idi mbili, au kwa udhuru wa kimwili: kama maradhi, na kama hataweza kufunga siku hizo sitini, basi analisha masikini au mafukara sitini ambapo kila masikini atampa kiasi cha Muddu, na hii muddu ni kiasi cha Sadaka ya Idi Al-fitri, na kama hataweza kuyafanya hayo yote basi kafara yake litakuwa deni atakalotakiwa kulilipa pale atakapokuwa na uwezo wa moja kati ya njia zilizotajwa hapo kabla, akiweza hapo baadaye ni lazima kwake kulipa wakati huo kwa kuwa na uwezo, na atalazimika kutubu toba ya kweli na kutorudia tena maishani mwake kwa dhambi hiyo aliyoifanya.
Na dalili ya hayo Hadithi ya Mashekhe wawili kutoka kwa Abu-Hurairah R.A. amesema kwamba: Tulipokuwa sisi tumekaa kitako kwa Mtume S.A.W. alimjia mtu akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mimi nimeangamia. Akasema: Nimemuingilia mke wangu nikiwa katika swaumu. Akasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu S.A.W.” Unaye mtumwa ili umwache huru?” Akasema: Laa. Akasema: "Je unaweza kufunga miezi miwili mfululizo? "Akasema: Laa. Akaacha Mtume S.A.W. kuzungumza naye na akasubiri kiasi. Huku na sisi tumo katika hali hiyo, akaletewa na Mtume S.A.W. kipakacha ambacho ndani yake mna tende. Akasema: "Yuko wapi muulizaji?” Akasema: ni Mimi hapa. Akasema: "Chukua tende hizi na uzitoe sadaka" Akasema Yule mtu: Nimpe aliye fakiri kuliko mimi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Basi Wallahi, baina ya majabali mawili haya (Yaani Madinah yote) hapana nyumba iliyo na ufukara kuishinda nyumba yangu mimi. Mtume S.A.W., akacheka mpaka yakaonekana magego yake, kisha akamwambia: "Walishe watu wako”.
Na Hadithi hii ni dalili ya wazi sana juu ya kwamba kafara ya tendo la ndoa lililofanyika mchana wa Ramadhani inaufuata utaratibu uliyotajwa hapo juu, nao ni: kumwacha huru mtumwa, kama mtu hakuweza basi atafunga miezi miwili mfululizo, na akishindwa kufanya hivyo basi anawalisha masikini sitini kwa chakula cha wastani anachowalisha watu wake.
Ikisemwa anayeilazimika kutoa kafara halazimiki kuifunga tena siku hiyo aliyoiharibu kutokana na msimamo wa Mtume S.A.W. pamoja na Al-Aarabiy aliyemwambia Mtume S.A.W. alimwingilia mke wake mchana wa mwezi wa Ramadhni na Mtume S.A.W. hakumwamuru kufunga badala ya siku hiyo, tutasema kuwa Hadithi ya Abu Dawud na Ibn Majah inairudia rai hii kwamba Mtume S.A.W. alimwambia mtu yule aliyemwingilia mke wake mchana wa mwezi wa Ramadhani “Na uilipe siku hiyo kwa kuifunga”; na kwa kuwa uharibifu wa saumu ya siku hiyo ya mwezi wa Ramadhani hautokani na uharibifu wowote kama vile kula au kunywa kunawajibika kuilipa kwa kuifunga siku hii iliyoharibiwa, na kwa hivyo basi kitendo cha mke kufanya tendo la ndoa na mume wake vile vile kunamwajibisha kuilipa kwa kuifunga siku aliyoiharibu.
Na kwa mtu asiyekuwa na mali, je, kafara ya kumwingilia mke wake inafutika? Al-nawawiyy alisema katika maelezo yake kwa Hadithi hii ilyotajwa hapo juu: “Kauli sahihi ya wanazuoni, na ndio inayopendelewa, kauli hii yasema kwamba Kafara haifutiki juu yake, bali ni kama deni juu yake mpaka atakapoweza kuilipa, kwa kiasi cha deni na haki zote na kadhalika. Ama maana ya Hadithi inamlazimika mtu kulipa kafara pale anapoweza, na hii ni dalili ya wazi ya kwamba kafara katika hali kama hii ni kama deni ambalo ni lazima kulilipa pale mtu anapoweza, kwani yule mtu alimwambia Mtume S.A.W. katika suala la kafara kwamba yeye hawezi kulipa au kuyatekeleza yale mambo yote matatu, kisha akaja Mtume S.A.W. kwa maji ya tende, basi Mtume S.A.W. alimwamuru kuyatoa, na hii dalili ya kumlazimu mtu kulipa kafara yake hata akiwa masikini au hana pesa wakati ho mpaka atakapoweza, na kwa sababu ya umasikini wake wakati ule Mtume S.A.W. alimwamuru mtu yule kuilisha familia yake; kwani alikuwa masikini wakati ule, na kafara inaweza kuchelewa, kwa hivyo Mtume alimwamuru mtu yule kuwalisha watu wake, na kafara ilikuwa deni juu yake mpaka alipoweza kuilipa, na hii ni sahihi kwa mujibu wa maana ya Hadithi”. [Sharhu Al-Nawawiy Juu ya Sahih Muslim 7\225, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Ama kwa upande wa mwanamke ayelitenda tendo la ndoa na mume wake mchana wa Ramadhani, Saumu yake imeharibika, na analazimika kuilipa siku hiyo aliyoiharibu tu na hana kafara yoyote; kwani Mtume S.AW. alimwamuru aliyemwingilia mke wake mchana wa Ramadhani atoe kafara yeye peke yake, na hakuamwmuru amwambie mke wake alipe kafara, na kuchelewa kwa ufafanuzi kutolewa kwa wakati wa haja hakujuzu, na kwa hivyo basi inajulikana kutokana na hayo kwamba mwanamke analazimika kuilipa siku hiyo moja tu pamoja na toba ya kweli.
Na rai sahihi hapa ni kwamba hakuna kafara yoyote kwa mtu aliyeiharibu saumu yake bila ya kumwingilia mke wake mchana wa Ramadhani kama vile kwa njia ya kula na kunywa, kwani kuna maandiko yanayohusu tendo la ndoa baina ya mume na mke tu.
Al-sheikh Zakariya Al-Answariy alisema katika kitabu cha [Athna Al-Matwalib 1\425, Ch, Dar Ak-Kitab Al-Islamiy] “anayeiharibu saumu yake pasina kumwingilia mke”, kama vile kwa kula au kujaribu kuyatoa maji ya manii (hana kafara) kwani matini iliitaja kafara katika tendo la ndoa la mchana wa Ramadhani tu, na hii ni dhambi kubwa zaidi kuliko nyingine yoyote (na haimlazimu mtu anayeingilia na mke wake na hali ya kuwa yeye ni mwenye kusahau) au hali ya kuwa yeye hajui hukumu hii ya kumwingilia mke wake mchana wa Ramadhani, au anayechukizwa kwa kumwingilia mke wake wakati wa saumu au anayemwingilia wakati wa safari, kwani mtu huyu hana dhambi yoyote, au anayekuwa mgonjwa na kuiharibu saumu ya mke wake, pia hana kafara ya aina yoyote ikiwa saumu hiyo sio ya Ramadhani, kwani saumu ya Ramadhani ina fadhila yake mahususi, na kwa hivyo kafara ni wajibu tu katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani tu. Na kauli yetu kwa sababu ya tendo la ndoa, mchana wa Ramadhani ili kujiepusha nalo mpaka mtu atakapofuturu kwanza, na baadaye akamwingilia mke wake, kwa hivyo basi yeye hana kafara yoyote) kama tulivyobainisha hapo juu”.
Na Ibn Qudamah alisema katika kitabu cha [Al-Mughniy 3\130, Ch. Maktabat Al-Qaherah] “Na tunaungana na rai hii kwani mtu huyu alifuturu bila ya kumwingiliana mke wake, na kwa hivyo hana kafara yoyote, na ni kama kumeza kitu au udongo, au ni kama kuwarudi wafuasi wa Imam Malik; na kwani wao hawana dalili ya matini au Ijimaa. Na haisihi kuchukuwa Kiasi (Kigezo) juu ya kumwingilia mke; lakini jambo hili likiwa katika Hija basi litaiharibu Hija hiyo na litamlazimu mtu anayehiji kuchinja ng`ombe; kwani jambo hili likitokea ndani ya mwezi wa Ramadhni basi litaiharibu saumu ya wote wawili, mume na mke wake)”.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia: mtu yeyote kuiharibu saumu yake ni jambo la haramu na halijuzu kisharia. Na anayeiharibu saumu yake kwa kumwingilia mke wake anafanya dhambi kubwa, na atalazimika kuilipa swaumu ya siku hiyo aliyoiharibu pamoja na kulipa kafara. Na anayeiharibu saumu yake bila ya kumwingilia mke wake, atalazimika kuilipa siku hiyo aliyoiharibu tu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.