Je, Baba Ndiye Hasa Anayetakiwa Kumfanyia Akika Mwanaye?
Question
Je baba ndiye hasa anayetakiwa kumfanyia Akika mwanae? Na je inajuzu kwa mama kumfanyia mwanae Akika kwa kuwepo baba mwenye kulazimika kufanya hivyo na ndiye anaelazimika kwa matumizi ya mwanae aliyezaliwa?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Akika maana yake ni nyewele ambazo mtoto anazaliwa nazo. Mtu alimfanyia Akika mwanae, anamfanyia akika hiyo mwanae, anapomnyoa nywele zake, na akamchinjia mbuzi. Na Akika: ni nywele anazozaliwa nazo mtoto nazo ndizo zinazosababisha kuchinjwa mnyama wakati wa kuzikata nywele hizo za mtoto aliyezaliwa; [Mu’jam Maqayeyes Al-Lugha kwa Ibn Faris Madahat Aq 3-4/4, Ch. Dar Al Fikr]
Na Akika katika sharia ni mnyama ambaye anachinjwa wanaponyoa nyewele za mtoto anayezaliwa, kukiita kitu kwa jina la sababu yake. [Mughniy Al-Muhtaj 138/6, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Na Akika ni Sunna iliyotiliwa mkazo, kwa Hadithi iliyopokelewa na Abu Dawud katika Sunna zake, kutoka kwa Amru Bin Shuaib kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, alisema: Mtume S.A.W, anasema:“"Atakaejaaliwa mtoto na akataka kumfanyia ibada hii basi na amfanyie, kwa mtoto wa kiume mbuzi wawili, na kwa mtoto wa kike mbuzi mmoja”, kwani ibada hiyo ni kumwaga damu bila ya kuwepo kosa lolote wala nadhiri na kwa hiyo sio lazima kama ilivyo katika uchinjanji wa kichinjo, na maana iliyomo ndani yake: ni kudhihirisha furaha kwa neema ya kizazi na kueneza nasaba".
Na Akika inatakiwa ifanywe na baba mzazi wa mtoto, baba ambaye analazimika kutoa matumizi ya mtoto huyo kwa makadirio ya ufakiri wake kwa maana ya ufakiri wa mtoto huyo, na hakika mambo yalivyo, sisi tumesema hivyo kwa sababu Akika ni jukumu la anayegharamia matumizi ya mtoto hata kama mtoto aliyezaliwa atakuwa tajiri kwa kurithi au kwa njia nyingine yoyote, kwa hiyo mzazi atawajibika kuitekeleza kwa mali yake mwenyewe na wala sio kwa mali ya mtoto, na mtu asiowajibika hapaswi kuifanya hiyo Akika isipokuwa kwa idhini ya mwenye kulazimika kuifanya Akika hiyo.
Na hii haipingani na alivyofanya Mtume S.A.W, alipofanya Akika kwa Al-Hassan na Al-Hussein kama ilivyopokelewa na Abu Dawud katika Sunna zake, kutoka katika Hadithi ya Ibn Abbas R.A. wote wawili, Pamoja na kwamba yule ambaye anawajibika kuwatolea matumizi wote wawili ni baba yao; kwani inategemewa kuwa matumizi yao yalikuwa juu ya Mtume S.A.W, kutokana na mzazi kushindwa kuyatekeleza - kwa hivyo Mtume aliwafanyia Akika kwa idhini ya wazazi wao.
Al-Khatweb As-Sherbiniy alisema katika kitabu cha [Sharhu Al-Mihaaj]: “Inasuniwa kwa yule mwenye kuwajibika kwa matumizi kumtolea mtoto wake kwa mujibu wa ufakiri wake (ni kwamba amfanyie Akika) mtoto aliyezaliwa (wa kiume kwa mbuzi au kondoo wawili) wanaolingana, na kwa (mtoto wa kike mbuzi au kondoo mmoja)” [Mughniy Al-Muhtaj 138/6, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Na As-Shams Ar-Ramliy akasema: “Na mfanya Akika ni yule anaewajibika kutoa matumizi yake kwa kiwango cha ufakiri wake katika mali yake bila ya mwanaye, kwa sharti la kuwa mwenye kufanya Akika hiyo ana hali nzuri: kwa maana kwamba wepesi huo wa kitabia kwa yanayodhihirika kabla ya kupita muda mwingi wa nifasi wala usipite muda huo kwa kuchelewa, na iwapo mtoto atafikia umri wa kubaleghe bila ya Akika basi umri wa akika utaondoka kwa mwingine, na yeye atakuwa na chaguo la kujifanyia Akika yeye mwenyewe.
Na Mtume S.A.W, alimfanyia Akika Hassan na nduguye Hussein kwa kuwa wao walikuwa chini yake kimatumizi kutokana na mzazi wao kutoweza kufanya hivyo au ilikuwa ni kwa idhini ya baba yao. Na jukumu la mtoto wa zinaa liko kwa mama yake. Inasuniwa kwa mama huyo kumfanyia Akika mwanae na wala haiwajibishi kudhihirisha kwake kunakopelekea kuonekana kwa aibu, na mwelekeo ni kama alivyoutaja Balqeniy ni kutokuwa sunna ya Akika kwa mzazi aliye huru kwa mwanae aliye mtumwa kwani hamuwajibikii kwa matumizi yake. [Nehayat Al Muhtaaj 138/8, Ch. Muswtafa Al-Halabiy].
Na ambaye analazimika kwa matumizi sio baba tu, na imekuja katika kitabu cha: [Sharhu Al-Menhaaj] kwa Al-Khatweb As-Sherbiny, katika Mlango wa Matumizi; “Sura katika matumizi ya ndugu, na mwenye kuwajibika ana undugu angalau sehemu ndogo tu (anawajibika) yaani mtu huyo awe mwanaume au mwanamke (kwa matumizi ya mzazi wake) aliyehuru (na akiendelea juu) kwa mwanaume na kwa Mwanamke (na mtoto) aliye huru (na akiendelea chini) kwa wajukuu na watukuu na kuendelea chini”. [Mughniy Al-Muhtaj 138/5, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Na imeeleweka kwa yaliyotangulia kuwa hakika matumizi ya mtoto sio wajibu wa baba tu bali ni wajibu pia kwa ndugu wa Kiumeni kwake kama vile babu na mama, iwapo baba atashindwa au akakosekana.
Na kutokana na maelezo hayo yaliyotangulia, ni kwamba hakika ya Akika huswihi kwa kila anayewajibika na matumizi ya mtoto aliyezaliwa miongoni mwa ndugu wa Kiumeni, na huswihi pia kwa wengine wasio kuwa hao wa Kiumeni lakini kwa idhini ya mzazi, na ikawa inaswihi kwa mama pindi anapolazimika kwa matumizi ya mtoto aliyezaliwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.