1- Kutumia Sabuni Yenye Harufu Nzur...

Egypt's Dar Al-Ifta

1- Kutumia Sabuni Yenye Harufu Nzuri kwa Mwenye Kuhirimia Ibada ya Hija na Umra.

Question

 Je, ni ipi hukumu ya kutumia sabuni yenye harufu nzuri kwa mwenye kuhirimia?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Wanazuoni wa Fiqhi walikubaliana kuwa kujipaka manukato wakati wa kuitekeleza ibada ya kuhirimia ikiwa ni katika mwili au katika nguo imekatazwa; kwa sababu mwenye kuhirimia anatakiwa asiwe mwenye kujipamba, na kujipaka manukato katika hali hii ni kwenda kinyume. Ama kujipaka manukato kabla ya kuitekeleza ibada ya kuhirimia ni Sunna, kwa maoni ya Wanazuoni wengi, kwa ajili ya kujiandaa na ibada ya kuhirimia, imepokewa kutoka kwa Aisha R.A., akisema: “Nilikuwa nikimpaka Mtume S.A.W., manukato kwa ajili ya kuhirimia kwake, kabla ya kutekeleza, na wakati wa kutoambatana na kuhirimia kabla ya kutufu”. Na akasema: “Mimi kama kwamba ninatazama mmeremeto wa manukato katika paji la Mtume S.A.W, wakati akihirimia”. [Muttafaq]
Wafauasi wa madhehebu ya Shafi na Hanbal walijuzisha kuwa mwenye kuhirimia aoshe nywele na mwili wake kwa kutumia kila kinachoondosha uchafu na kisicho na manukato, kama vile majani maalumu ya miti yenye harufu nzuri yanayochanganywa na maji kwa ajili ya kujisafisha, na walielekeza hivyo kuwa matumizi ya majani haya hayazingatiwi kwa uzuri wala manukato isipokuwa kujisafisha tu.
Inaeleweka kuwa wafuasi wa madhehebu ya Shafi na Hanbal hawakatazi matumizi ya kila chenye manukato kwa mwenye kuhirimia kwa uwazi, lakini sharti la kukataza ni matumizi kwa ajili ya uzuri, kwa sababu hiyo hawakukataza kula matunda kama vile tufaha na mengineyo, kwa sababu matumizi yake ni kwa ajili ya kula, na karafuu ni kwa ajili ya kupata dawa, kwa hivyo kila mimea asili ya matumizi yake si kujipaka manukato haihitaji fidia, hata ikiwa na harufu nzuri iweje isitumia kwa ajili ya kujippaka manukato, lakini kwa hivyo walisema kuwa kuacha ni bora zaidi.
Na wafuasi wa madhehebu ya Malik walijuzisha matumizi ya kila kinachoondosha uchafu na ubaya kisicho na manukato, kinyume na kilicho na manukato ambapo matumizi yake inawajibika kutoa fidia. Na wafuasi wa madhehebu ya Hanafi walikataza yote yaliyotajwa.
Al-Kasaniy mfuasi wa madhehebu ya Hanafi katika kitabu cha: [Al-Badai’: 2/190-191, Ch. Ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] anasema: “Kama akitibu jeraha lake kwa kutumia mafuta au ufa wa miguu yake, halazimiki kutoa kafara; kwa sababu haya si manukato, ingawa ni asili ya manukato lakini matumizi yake si kwa ajili ya kujipaka manukato, kwa hiyo halazimiki kutoa kafara; kinyume na matumizi ya manukato kwa ajili ya kutibu si kwa ajili ya kujipaka manukato, ambapo analazimika kutoa kafara, kwa sababu ni manukato, basi si kitu kuwa kwa ajili ya uzuri au kwa jambo jingine”.
Akasema: “Akiosha kichwa na ndevu zake kwa majani yenye harufu basi analazimika kuchinja mnyana kwa kauli ya Abu Hanifa, na analazimika kutoa sadaka kwa kauli ya Abu Yusuf na Muhammad, ambapo wanaona kuwa majani haya si manukato, na matumizi yake kwa ajili ya kuondosha uchau, mfano wa kila aina hii, na hailazimiki kuchinja mnyama, lakini inalazimika kutoa sadaka; kwa sababu majani haya yanawaua wadudu na si manukato kwa asili. Na Abu Hanifa anasema kuwa; majani haya ni manukato, kwa sababu harufu yake nzuri, basi inalazimika kuchinja mnyama mfano wa kila aina ya manukato, na kwa sababu yanaondosha uchafu na kuwaua wadudu”.
Katika kitabu cha: [Ad-Durul Mukhtar na Al-Haskafiy]: “Wajibu ni kuchinja mnyama kwa Mwenye kuhirimia, mwenye kubaleghe akikipaka manukao kiungo… au akipaka mafuta, au mafuta ya ufuta kwa sababu ni asili ya manukato, lakini akila, akiiweka puani, akipoozea jeraha, au nyufa za miguu, au akiiweka masikioni, halazimiki kuchinja mnyama wala sadaka, kwa makubaliano ya wanazuoni”.
Ibn Abidiin anasema: “Kauli yake (kwa makubaliano ya wanazuoni) kwa sababu haya si manukato kwa uwazi, na kama isipotumiwa iwe manukato, basi haina hukumu ya manukato ndani yake”. [2/543, Ch. Ya dar Al-Fikr]
Al-Khirshiy mfuasi wa madhehebu ya Malik katika Shaehe yake ya Mukhtasar Khalil anasema: “akiiosha mikono yake kwa mada ya kusafisha bila ya kuitumia kama manukato kama vile majani yasiyo na harufu na sabuni na kila kinachoodosha uchafu, na kujiepusha na vitu vyenye harufu na matunda yanayoacha harufu katika mikono, kwa sababu yana maana ya kujipaka manukato, lakini akikichanganya kitu chenye harufu, na kama kitu hiki kikikitumiwa peke yake, basi halazimiki kutoa fidia, na jambo lile lile asipokichanganya. [Mwisho].
Ad-Dardir mfuasi wa madhehebu ya Malik katika Ash-Sharehe Al-Kabiir anasema: “Akiiosha mikono yake iliyo na uchafu kwa mada ya kusafishia basi haiwi haramu ikiwa mada hii si ya harufu”.
Ad-Disuqiy katika Hashiya yake ya As-Sharh Al-Kabiir anasema: “Kauli yake: mada ya kusafisha isipokuwa yenye harufu: mfano wake sabuni, maana yake: ikiwa mada ya kusafisha yenye harufu ni haramu kuiosha mikono kwake, na inalazimika kutoa fidia, kwa mfano majani yenye harufu yakikaushwa na kusagwa kwa ajili ya kuioshea mikono yake”. [2/60, Ch. Ya Dar Al-Fikr]
Ibn Hajar Al-Haitamiy mfuasi wa madhehebu ya Shafi anasema katika [Tuhfat Al-Muhtaj]: “Mwenye kuhirimia hakatazwi kuosha kichwa na mwili wake kwa majani ya kusafisha, kwa sababu ni kuuondosha uchafu, kinyume na mafuta ambayo yanafanana na manukato. Hakika ni bora kuacha kutumia hivyo hata katika nguo yake, isipokuwa uchafu ni wazi, kama inavyobainika”. [4/169, Ch. Ya Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy]
Ash-Sharwaniy anasema akieleza: “Mfano wa majani ni sabuni isiyo ya harufu”.
Ar-Ramliy katika [Nihayat Al-Muhtaj] anasema: “Hakuna kujipaka manukato kwa matunda kama vile: tufaha, chenza, nk, kwa sababu ni vyakula; vile vile dawa, kama vile karafuu, sandarusi, na aina zote za miti shamba, kwa sababu matumizi yake ni kwa ajili ya kutibu; vile vile maua yenye harufu ambapo hayatumiwi kama manukato”. [3/334, Ch. Ya dar Al-Fikr]
Katika [Al-Wadhih na Ibn Aqiil mfuasi wa madhehebu ya Hanbal kuna mapokezi ya kuwa: hakuna kutoa fidia kwa kupaka mafuta ya manukato, kwa sababu si makusudio yake [ Rejea; Al-Furuu’ na Ibn Muflih; 5/436, Ch. Ya Muassasat Ar-Risalah]. Kwa hivyo inawezekana kuelekea kuwa maelezo ya mapokezi haya ni kuwa; mwenye kuhirimia inaruhusiwa kwake kutumia mada za kusafisha hata zikichanganywa kwa manukato, kwa sababu ya kutopatikana makusudio.
Na kwa mujibu wa maelezo yaliyotajwa, hakuna kizuizi chochote cha kutumia sabuni yenye harufu nzuri kwa mwenye kuhirimia, kwa kuwa haitumiwi kwa lengo la kujipaka manukato, lakini ni bora zaidi kutoitumia, kwa ajili ya kujiepusha na hitilafu.
Na Mwenyezui Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas