Kubadilisha Pesa

Egypt's Dar Al-Ifta

Kubadilisha Pesa

Question

 Je, inajuzu kubadilisha sarafu za madini kwa sarafu za karatasi na kwa ujazo unaolingana?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Baadhi ya watu hususan wafanyabiashara wanabadilisha sarafu ndogo ndogo kwa sarafu za karatasi, na pengine hukamilisha mauziano haya kwa mizani; yaani kwa kuzipima sarafu hizo na kuziuza kama bidhaa zozote kwa bei maalumu kilo kwa mfano kiasi kadhaa. Na labda kutimiza mauziano kati ya sarafu za madini kwa sarafu za karatasi kwa kiasi maalumu cha pesa, na aghalabu sarafu za karatasi zinakuwa na thamani ya juu zaidi kuliko sarafu za madini, na katika hali nyingine sarafu za madini zinakuwa ghali zaidi kuliko sarafu za karatasi, kama katika hali ya kutumia sarafu katika simu ya kawaida inayotumia sarafu za madini.
Na sura hii imetajwa katika Fiqhi ya kiislamu katika mlango wa riba, au katika mlango wa matumizi; kwani mazungumzo yanakuwa juu ya mbadala wa mali kwa mali, na zinakuwa zenye sura mbali mbali kati ya kuruhusiwa na kutoruhusiwa.
Na hukumu katika suala hili kwa sura yake yote iliyotajwa katika mfano wa suala hili lote ni ruhusa.
Na dalili ya hayo ni kwamba sababu ya kuiharimisha riba katika dhahabu na fedha aghalabu kwa sababu ya namna ya thamani yake, na uharamu huu ni katika dhahabu na fedha tu; kwani uharamu wa riba hapa siyo kwa maana ya ndani inayopitisha pesa nyingine; kwani lau kuwa inapitisha pesa nyingine zisingeruhusiwa katika pesa nyingine; kwani kila vitu viwili vinakusanywa na kasoro moja katika riba haijuzu katika kukizuia kimoja na huruhusu kingine kama katika dhahabu na fedha, na hii ni dalili juu ya kuwa maana ya hayo ni kuhusu madini hizo mbili tu na siyo namna nyingine. Na alipotaja lafudhi ya ((aghalabu)) katika maelezo ya kuiharamisha riba katika dhahabu na fedha ili kuziepusha namna nyingine za pesa, na zinaingia katika riba vitu vinavyotengenezwa kutoka dhahabu na fedha.
Na kama tulivyosema kuna baadhi ya makundi ya Wanachuoni walitoa baadhi ya maoni juu ya jambo hili:
Sheikh Zakaria Al-Ansary alisema: "kuiharamisha riba katika dhahabu na fedha hata lau kuwa ni vito vya dhahabu vya wanawake au vitu vya jiko kama sahani vilivyotengenezwa kutokana na dhahabu au fedha na siyo katika pesa". [Asna al-Matwaleb Sharh Rodh Al-Twaleb 2\22, Ch. Dar Al-Kitaab Al-Islamiy].
Na Al-Khatweb As-Sherbiny alisema: "Na fedha kwa fedha", na maana ya hayo ni dhahabu na fedha zikiwa ni kwa mfumo wa pesa au la (kama chakula kwa chakula) hukumu yake ni kama katika kila masuala yaliyotangulia, ikiuzwa kwa namna ileile kama dhahabu kwa dhahabu itakuwa ni lazima kuuzwa kwa mithili yake, ama lau ikiuzwa kwa namna nyingine siyo kutoka namna moja kama kwamba kuuza dhahabu kwa fedha hapa yaweza kuifadhilishwa baina ya namna hizi mbili. Ikisemwa kulazimisha kutangulia pesa juu ya chakula kwa mujibu wa mwafaka wa Hadithi ya Mtume S.A.W., itasemwa kwamba maneno katika chakula yalikuwa mengi zaidi kuliko katika pesa. Na haisemwi: ikitangulia iliyokuwa na maneno machache ni afadhali; kwani hayo kwa mujibu wa makusudio, na kasoro ya riba katika dhahabu na fedha, aghalabu ni kwa sababu ya uhalisia wa thamani zake. Kwa hivyo dhahabu na fedha katika pesa na vitu vya nyumbani vya dhahabu kwani vitu hivi vinaweza kufanya ndani yake njia ya riba kama tulivyosema hapo juu, na siyo miongoni mwa kutathimini vitu vingine". [Mughny Al-Muhtaj Sharh Menhaj At-Twalebeen 2\25, Ch. Dar Al-Fekr].
Na Al-Bahuty alisema: "(na ikiwa moja yake) kwa maana moja ya namna mbili za mauzo ( zikiwa ni pesa taslimu, basi, la) hairuhusiwi kwa wanawake na wala kuubatilisha mkataba kwa sababu ya kuchelewa kuchukuwa pesa hata lau kuwa ya pili ni kupimiwa kama kwamba kuziuza chuma au shaba au vitu vingine kwa dhahabu au fedha, alisema katika kitabu cha: [Al-Mubdea]: Bila ya hitilafu kwani mwanasharia aliruhusu katika mbadala. Na asili katika jumla ya mali yake: Lau zingeharamisha dhahabu na fedha juu ya wanawake zingezuia mlango wa mbadala, aghalabu katika mambo yanayopimwa kwa uzito (na lau katika matumizi ya pesa) yaani kwa pesa taslimu, basi inaruhusiwa kwa wanawake (na imechaguliwa na sheikh na wengine) kama Ibn Akil na Sheikh alitaja riwaya juu ya jambo hili, alisema katika kitabu cha: [Ar-Reayah] (jambo hili ni kinyume cha lililotajwa katika kitabu cha Al-Tanqeh) na sharti la kuruhusu ni kupita mwaka kamili na kukabidhi katika matumizi ya pesa za dhahabu kwa pesa za kawaida. Na yaliyotajwa katika Al-Tanqeh yalitajwa katika kitabu cha: [Al-Mubdea] na yalitajwa katika kitabu cha: [Al-Inswaf]: Kwa kweli rai hii ni sahihi miongoni mwa madhehebu yote,na aghalabu ya Masahaba waliafikiana na rai hii, na yalitajwa pia katika kitabu cha: [Al-Muharrar na Al-Furua na Al-Raaytheen na Al-Hawayen na Al-Faeq]. Na kuithibitishia katika kitabu cha: [Al-Muntaha]. [Kashshaf Al-Qenaa 3\264, Ch. Dar Al-Fekr].
Al-Desouqy alisema: "Uuzaji wa pesa za kawaida zinazotumika nazo kwa pesa za dhahabu na fedha za kiserikali, basi anayetegemea juu ya kuwa pesa si riba, ili zikawa ni halali basi ni lazima ziwe zimefanana hata lau asijue idadi yake, na lau ikazidisha moja yake mbali na biashara basi ni halali, na lau kinyume cha hayo, hairuhusiwi, ama lau alizingatia pesa ni pesa za riba basi hairuhusiwi kuuza isipokuwa pesa mbili ni mfano katika uzito wake au katika idadi zake". [Hashiyat Al-Desouqy juu ya maelezo makubwa 3\61, Ch. Dar Al-Fekr]
Ikisemwa: Baadhi ya wanazuoni hawaoni ruhusa katika jambo hili, na dalili ya sababu zao kwamba jambo hili ni miongoni mwa mlango wa uuzaji wa mali kwa mali bila ya kuzichukuwa pesa taslimu, na jambo hili limekataliwa katika Hadithi sahihi kama katika Hadithi ya Abu Bakr R.A alisema: Mtume S.A.W., alisema "Msiuze dhahabu kwa dhahabu ila kuwa uzito sawa, na fedha kwa fedha ila kuwa uzito sawa, na Uzeni dhahabu kwa fedha, na fedha kwa dhahabu mnvyotaka".
Na kujibu juu ya haya ni: kwamba upingaji huu katika asili yake ni sahihi.lakini upingaji huu haikuwa sawa katika suala hili, na tofauti hapa ni kwamba wanazuoni wa fiqhi walipozungumzia walizungumza juu ya dhahabu na fedha, ama pesa nyingine hazikuchukuliwa hukumu ile ile ya dhahabu na fedha.
Al-Suyuty alisema: "Hakuna riba katika pesa zinazotengenezwa kutokana na madini mengine, yasiyokuwa dhahabu au fedha". [Al-Ashbah na Al-Nadhaer Uk.370]
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia inajuzu kisheria kubadilisha pesa za madini kwa pesa za karatasi, au kinyume chake, na jambo hili si miongoni mwa riba.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


Share this:

Related Fatwas