Kilemba Kati ya Mazoea na Ibada.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kilemba Kati ya Mazoea na Ibada.

Question

Je, kuvaa kilemba chochote kichwani ni ibada, na kuacha kufanya hivyo ni jambo linalochukiza au jambo baya? 

Answer

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa Njema za Mwenyezi Mungu, na Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake, na Masahaba wake, na waliomfuata. Na baada ya hayo:
Kilemba ni kifuniko cha kichwa, ambacho ni kipande cha kitambaa kinachozunguka kichwa, peke yake au pamoja na kofia.
Kilemba kilikuwa miongoni mwa ada za waarabu wa zamani, na kazi yake ilikuwa kuwakinga kwa joto la Jua, na Imamu Malik anasema: “kilemba, kukaa kwa kuishika miguu yake kwa mikono miwili, na kuvaa viatu ni mazoeo ya waarabu”. [Al-Muntaqaa Sharh Al-Muwataa’ na Al-Bajiy: 7/219, Ch. ya As-Saa’adah].
Abul-Aswad Ad-Dualiy anasema kuhusu kilemba kuwa ni: “Kinga katika vita, mwavuli dhidi ya joto, kinachotia joto dhidi ya baridi, heba katika mikutano, kinga dhidi ya ajali, ziada ya urefu, na ni miongoni mwa ada za waarabu”. [Buluugh Al-Arab Fi Maarifat Ahwaal Al-A’arab, na Mahmuud Shukriy Al-Aalusiy: 3/410, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Mtume S.A.W., amevaa kilemba, kutokana na ada na mazoeo ya watu wake, na mengi ya yaliyopokelewa naye kuhusu kilemba ndiyo ni masimulizi na maelezo ya hali yake; na An-Nasaiy katika Sunnan yake, kutoka kwa Al-Mughirah Ibn Shuu’bah kuwa: “Mtume S.A.W, ametawadha, akafuta utosi wake, kilemba, na viatu vyake”.
Na Mtume S.A.W., alikuwa na kilemba, na alikuwa akikizungusha katika kichwa chake kitukufu, ambacho kinaitwa As-Sahaab, akamvalisha Ali R.A.; na Mtume S.A.W., alipovaa kilemba akaacha ncha yake kati ya mabega yake, au alikuwa akikiunga chini ya kidevu chake; na alikuwa akimnasihi Umar R.A, ili afanye hivyo wakati wa vita kwa ajili ya kukiunga. [Tazama: Zaad Al-Maa’ad, na Ibn Al-Qaiym; 1/130, na ilivyo baada yake, Ch. ya Ar-Risalah].
Na ilivyokuwa sahihi kutoka kwa Mtume S.A.W., kuwa amesema kuhusu mwenye Ihramu kuwa: “Havai kanzu wala kilemba”. [Muttafaq, kutoka kwa mapokezi ya Abdullahi Ibn Umar R.A.].
Na hii ni dalili kuwa kilemba kilkuwa ada, na ipo amri ya kukiepusha katika hali ya ihramu, na kutofunika kichwa kwa ajili ya kumtukuza Mwenye Utukufu. [Faidh Al-Qadiir, na Al-Manawiy: 4/429, Ch. ya Al-Maktabah At-Tijariyah Al-Kubra].
Wanazuoni wengi zaidi walizingatia kuwa kumfuata Mtume S.A.W., kuhusu kuvaa kilemba na kofia na vinginevyomiongoni mwa vifuniko vya kichwa viwe halali; kwa sababu tendo hili la Mtume S.A.W., halikuonesha maana ya ibada, bali linaonesha maana ya ada na tabia, kama vile chakula na kunywa, vile vile haikupokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W., kupendezesha wala kuhofisha kuhusu kifuniko cha kichwa. Na rai mashuhuri kwa wana Usuul wa Fiqhi kuwa hakuna kufuata katika mambo kama haya, lakini akitaka mtu kufanya afanye, na akitaka kuliacha aache, bila ya tofauti kati ya kufanya na kuacha kuhusu thawabu n.k., na bila ya kuwepo kusemwa vibaya kisheria kuhusu kuacha. [Afa’alur-Rasul, na Al-Ashqar: 1/225, kwa maelezo machache, Ch. ya Ar-Risalah].
Kilemba na kofia ingelikuwa mavazi yanayopendekezwa, basi mavazi kama nguo ya juu, nguo ya chini, kanzu, na kila kilichopokelewa kuwa ni mavazi ya Mtume S.A.W., ingelikuwa pia ni mavazi yaliyopenekezwa.
Kuhusu kauli zilizopokelewa juu ya kuvaa kilembe na kofia siku zote, kauli hizi nyingi hazifai kuwa hoja ya kuleta hukumu, kwa sababu hizi zote ni Hadithi dhaifu. [Kashful-Khafaa’, na Al-A’jluniy: 2/94, Ch. ya Al-Maktabah Al-A’sriyah].
As-Sakhawiy anasema: “Hizi zote ni dhaifu… na baadhi yake ni dhaifu sana kuliko nyingine”. [Al-Maqasid Al-Hasanah: Uk. 466, Ch. ya Dar Al-Kitab Al-A’rabiy] Na Hadithi kama hizi zimetajwa na watungaji wa vitabu vya Hadithi za kuzuliwa.
Na Imamu Al-A’ainiy anasema: “Imamu Bukhariy hakutaja, katika mlango huu unaohusu vilemba, kitu cha mambo ya kilemba, hivyo kama kwamba yeye hakukuta hoja sahihi, kwa mujibu wa sharti lake, kuhusu kilemba”. [U’umdatul Qariy: 21/307, Ch. Ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy].
Kipande cha kitambaa cha kilemba kinaitwa (Dhuaba), na kukirefusha ni mazoeo na haimaaanishi ibada, kwa hiyo ilivyopokelewa katika amri ya Mtume S.A.W., kwa Abdur-Rhman Ibn A’auf akirefushe, wakati alipomwelekeza vitani, haizingatiwi kuwa ni hukumu ya jumla, pia Isnad yake haina nguvu. [At-Twabaraniy ameipokea katika kitabu cha: [Al-Mu’jam Al-Awsat]. Na halikupokelewa katazo la kuvaa kilemba bila ya (Dhuaba); Jaabir Ibn Abullahi amepokea kuwa Mtume S.A.W., aliingia Makkah, na juu yake kipo kilemba cheusi [Ameipokea Muslim], na Hadithi hii ya Jaabir haikutaja ndani yake (Dhuaba), na hii inaonesha kuwa yeye hakuwa akikirefusha kipande cha kilemba kati ya mabega yake siku zote.
Na Maimamu wawili wa Hadithi wamepokea kutoka katika Hadithi ya Anas, kuwa Mtume S.A.W., aliingia Makkah, na juu yake yapo mavazi ya vita na kofia ya chuma ya vita ipo juu ya kichwa chake. Na hii inamaanisha kuwa yeye amevaa kitu kinachofaa hali yake, na hakuna hitilafu kati ya Hadithi mbili hizi kuhusu sura yake wakati kuingia kwake Makkah; kwa kuwa inawezekana kuwa wakati kuingia Makkah akiwa na kofia ya chuma kichwani, kisha akaivua, akakivaa kilemba baadaye, kwa hiyo kila mpokeaji alipokea alivyoiona. [Tazama: Ghiaa’ Al-Albaab Fi Sharh Mandhuumat Al-Adaab, na As-Safariniy: 2/246, Ch. Ya Muassasat Qurtubah].
Baadhi ya watu wanamlaumu yule anayefichua kichwa chake kuwa ni miongoni mwa uvunjifu wa maadili ya kiungwana, lakini twasema kuwa: Ungwana ni ukamilifu wa sifa za mtu kama ukweli, kusubiri kwa maovu ya wenzake, kutoa hisani kwa watu wa zama zake, na kutokufanya udhia kwa majirani. Na Imesemwa kuwa: Ungwana ni kushirikiana na tabia za wenzake na marafiki zake katika mavazi, kutembea, mwendo, utulivu, na sifa zote. Na imesemwa pia kuwa ni: Kutenda yasiyo ya kawaida ya wenzake. Na jumla ya kauli ya wanazuoni juu yake kuwa: Kujiepusha yanayosababisha kusemwa vibaya kidesturi. [Tazama: Tawdhihul Afkaar, na Al-Amir As-Sana’aniy, Ch. Ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah, Beirut].
Na jambo la kutoficha kichwa lilikuwa miongoni mwa kuvunja ungwana kwa Waarabu na Waislamu kwenye zama zilizopita, na mazoeo ya watu yalipita katika zama hizi kutohishimu yule anayefanya hivyo, na ile iliendelea mpaka hivi karibuni, kwa mfano hapa Misri.
Kuhusu kuvunja ungwana ni mambo yanayobadilika na kuhitilafiana kutokana na zama na mazoeo ya watu, na marejeo yake yanarejea desturi za watu wa zama maalumu. Kwa hiyo kuna mambo katika zama fulani yanazingatiwa kuwa miongoni mwa kuvunja ungwana, bali hayazingatiwi hivyo katika zama zingine.
Ash-Shatibiy aligawanya mambo ya mazoeo ya watu kwa mtazamo wa Sharia yawe migawanyo kadhaa: Kuhusu mazoeo yanayojiri kati ya watu, na hakuna dalili ya Sharia inayoyakubali au kuyakataza, nayo ni mazoeo yanayobadilika, akisema: “mazoeo yanayobadilika, miongoni mwake yanayobadilika kutoka kwa mema mpaka mabaya na kinyume chake; kwa mfano kufichua kichwa, na jambo hili linahitilafiana kutokana na mahali; nalo ni baya kwa waungwana wa nchi za mashariki, na silo baya kwa watu wa magharibi; basi hukumu ya sheria inahitilafiana kwa mujibu wa hayo, kwa watu wa mashariki ni jambo la kuvunja uadilifu, na kwa watu wa magharibi silo la kuvunja”. [Al-Muwafaqaat, na Ash-Shatibiy: 2/284, Ch. Ya Dar Al-Ma’rifah, Beirut]. Hakika tendo linabadilika liwe jema au baya kutokana na tofauti ya jamii.
Na kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia: Sharia imeacha kubaini sura ya nguo na namna ya kuuzunguka mwili na maelezo yake kwa kila kundi la watu, na namna inavyowachukulia, kwa kuangalia hali na mazoeo yao; hivyo kuzingatia hayo ni mambo ya maisha huitwa mambo ya lazima, majaribio, na mazoeo, na kuwa kuangalia mavazi ya wakati ni miongoni mwa uungwana, isipokuwa ni ya dhambi, na utofautishaji mavazi ni aina ya umashuhuri, na haijuzu kwa Muislamu kutofautisha wengine na watu wa wakati wake katika mavazi na mazoeo ya maumbo, ambayo yanamwingiza katika umashuhuri na kujitenga. Kwa hiyo kilemba cha kichwa ni jambo la mazoeo na sio la ibada.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas