Uhandisi wa Vinasaba Katika Nyanja ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uhandisi wa Vinasaba Katika Nyanja za Tiba.

Question

Je, inajuzu kuingiza au kutumia uhandisi wa vinasaba (vya kimaumbile) katika uwanja wa tiba na madawa? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kwa hakika kwamba Uislamu umesisitizia kutibu, na Sunna imetaja Hadithi nyingi katika jambo hilo, miongoni mwao: "Jitibuni; kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuweka ugonjwa isipokuwa aliuwekea dawa yake". Imetolewa na Abdu Dawud kutoka kwa Usamah Bin Shuraik, na Sunna imebainisha kuwa mumini mwenye nguvu ni mpenzi zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko mumini dhaifu, kama ilivyotaja katika Hadithi iliyopokelewa na Muslim kutoka kwa Abu Hurairah.
Kwa hiyo, asili ya kujitibu ni halali isipokuwa uhalali huu utakapopingana na yale ambayo hayajaruhisiwa Kisheria kama vile kuacha uharibifu mkubwa zaidi, wakati huo, hakujuzu kujitibu huko.
Na imedhihirika siku hizi kwa inayojulikana kama uhandisi wa vinasaba vya kimaumbile na kuutumia katika kutibu kwa baadhi ya magonjwa, na hapa linazuka swali la hukumu ya matumizi ya jambo hilo la kisasa katika kutiba.
Tukianza mwanzo kueleza Uhandisi wa vinasaba: Basi Istilahi ya Uhandisi wa vinasaba inayojengeka kwa maneno mawili Uhandisi na vinasaba. Na neno hili lina maana ya kuendesha mfumo wa hali ya vinasaba na kuvipangilia vinasaba hivyo katika maumbile yake ya Kikemikali kwa kuvigawanya gawanya, kwa maana ya kuvunja vunja vinasaba vyenyewe kwa vyenyewe na kuviunganisha kwa maana ya kuongeza maada ya vinasaba katika vinasaba vingine vilivyopatikana kwa kujitolea, kwa kutumia njia za kimaabara.
Na neno la pili ni Vinasaba, na hilo ni aina ya maada inayotayarishwa kwa matumizi ya kiuhandisi na ni vinasaba na mijengeko vya kikemia ambayo humjenga kiumbe hai . Na vinasaba kama tulivyotoa maelezo yake, ni Dalili za sifa za kuumbwa kwa kiumbe hai pamoja na mienendo yake. [Al Ka'inat na Handasat Al Mauruthaat kwa Dkt. Swaleh Abdul Azizi (warsha ya Vinasaba na Uhandisi wa Vinasaba) 111/1]
Hakika ya mwelekeo wa kisayansi walioufikia wataalamu hapana shaka kwamba sehemu ya mwelekeo huo ina masilahi kwa binadamu. Ambapo sehemu hiyo inalinda afya ya mwanadamu huyo kama vile upandikizaji wa kinasaba chenye kazi maalumu mwilini ili kiungo husika kiweze kufanya kazi yake ipasavyo.
Kama inavyojulikana katika upandikizaji wa vinasaba vya binadamu ambavyo hupelekea utoaji wa insulini katika aina za bakteria na kuacha vizaliane na kisha kuzalisha kiwango kikubwa cha insulini ya binadamu ambayo inaizidi kwa kiwango kikubwa sana insulini inayotokana na mimea katika tiba ya ugonjwa wa kisukari au kwa lengo la kujipatia homoni za ukuaji wa kinasaba ambacho huzalisha huizalisha insulini hiyo kwa ajili ya kuwatibu watoto wenye kasoro za ukuaji ambazo husababisha ufupi uliopindukia.
Au jinsi ya kuiandaa maada inayokosekana katika ugonjwa wa homofilia ambao huzorotesha mgando wa damu na kusababisha uvujaji wa damu mwilini, au maada ya introfiloni inayotumika katika kutibu baadhi ya aina za saratani, na vile vile mazoezi katika ulimwengu wa kilimo na ufugaji wa wanyama.
Na kitengo hichi cha Uhandisi wa Vinasaba kiasili ndani yake kinazingatiwa kuwa na sifa nzuri bali kinachukua nafasi ya utafiti na uangaliaji ambao Uislamu unaulingania na kuupendekeza: Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema : {Sema: Tembeeni katika ardhi na tazameni jinsi alivyo anzisha uumbaji; kisha Mwenyezi Mungu ndiye Anaye umba umbo la baadaye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu}. [AL ANKABUUT 20],
Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamuoni}. [AHA DHARIYAAT 21], na kwa aya nyingine nyingi ambazo zinatafuta jinsi ya kuangalia na kushuhudia, kwani kushuhudia kisayansi ni asili miongoni mwa asili ambazo wanachuoni wanazitumia, na Aya ambazo zinaamrisha kushuhudia na kutumia masikio na akili ni nyingi sana katika Qur'ani kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu amekutoeni matumboni mwa mamazenu, hali ya kuwa hamjui kitu, na amekujaalieni masikio na macho na nyoyo ili mpate kushukuru} [AN NAHLI 78]. [Tazama: Nadharaat Firiyah fii Ajiniyum Al Bashariy, Dkt. Abdullah Mohammad Abdullah, warsha ya Vinasaba na Uhandisi wa Vinasaba 738/2].
Na magonjwa mengi miongoni mwa magonjwa yanayorithiwa husababishwa na vinasaba vinavyoyazalishwa, na magonjwa mengi kati yake yanarejea katika mabadiliko ya muundo wake unaozorotesha kinasaba kwa kuzalika kimaumbile aina ya protini muhimu, na kutibu kwa vinasaba ni njia mpya inayotegemea zaidi uzalishaji wa chembe ndogo ndogo za kutibu zenye mfungamano na teknolojia ya kina mno, na tiba za wagonjwa na tafiti za kimajaribio juu yao vinaonesha kuwa utekelezaji wa siku za usoni unangojea aina hii ya tiba.
Na madaktari wanakiri pamoja na wanasayansi kwamba utekelezaji wa aina hii ya tafiti za kimajaribio na kimatibabu utafanyika kwa magonjwa yaliyoenea zaidi, ambapo huwakumba mamilioni ya wagonjwa Ulimwenguni; kama vile magonjwa ya saratani, ugonjwa wa mapafu ujulikanao kama virusi vya C (Kijidudu cha C), Ukimwi na magonjwa mengine ya moyo na matumbo; kama vile mafuta shahamu yanayorithiwa, na ukakamavu wa mishipa ya damu, na magonjwa ya mfumo wa hisia; ugonjwa wa pankisoni, na ugonjwa wa Zahaimari. [Tazama: Al Ka'inat na Handasat Al Mauruthaat kwa Dkt. Swaleh Abdul Azizi (warsha ya Vinasaba na Uhandisi wa Vinasaba)]
Ama kwa upande wa tiba ya vinasaba na panakusudiwa katika hili, tiba ya magonjwa kwa kuangazia walipofikia wanasayansi, na wanachokiendea ili wakifikie miongoni mwa maelezo yanayohusu jinome ya mwanadamu – ambayo ni ramani ya mwili mzima wa mwanadamu – na kuainisha sehemu ya kila kinasaba katika kila kromozoni ili kuweza kugundua siri maalumu ya kila kinasaba.
Na kujua mahusiano ya kila kinasaba na kile kinachokitangulia na kinachofuatia kwa lengo la kujua sababu za magonjwa ya kurithi, na kujua mjengeko wa kiurithi wa mtu yoyote ikiwemo uwezekano wa kutokea magonjwa maalumu; kama vile shinikizo la damu, au mishituko ya moyo, saratani na magonjwa mengine mengi, na tiba kwa njia ya vinasaba kwa magonjwa ya kurithika.
Na kuzalisha maada za kibaiolojia na homoni ambazo mwili unazihitaji kwa ajili ya kukua, kwani hakika Uislamu unatilia mkazo kwa kiasi kikubwa mno juu ya usalama na kutokuwa na Magonjwa pamoja na kujilinda nayo. Na Mtume S.A.W ametupa sisi mwongozo wa kujitibu na kututahadharisha na maambukizi kama ilivyokuja amri ya kuwatenganisha wagonjwa na wenye afya kwa ajili ya kulinda afya zao. [Tazama Utafiti wa: Haithiyat Al Ahkaam Ashar'iya kwa Baadhi ya Masuala ya kutibu, kwa Sheikh Ali Juma].
Na azimio la Baraza la Kifiqhi, linalofuata Chama cha Ulimwengu wa Kiislamu katika Mji Mtukufu wa Makka katika mkutano wake wa kumi na tano, ambao unakusanya hukumu kadhaa na vidhibitisho ambavyo vimetaja kwamba: Baraza la Mkusanyiko wa Wanachuoni wa Fiqhi ya Kiislamu walio chini ya Chama cha Ulimwengu wa Kiislamu katika mkutano wake wa kumi na tano uliofanyika katika Mji Mtukufu wa Makka, ambao ulianza tarehe kumi na moja, mwezi wa Rajabu, mwaka wa Elfu moja mia nne, kumi na tisa, inayoafikiana na tarehe thelathini na moja, mwezi wa Oktoba, mwaka wa Elfu moja mia tisa, tisini na nane. Limeangalia katika Suala la Waislamu kunufaika na elimu ya Uhandisi wa vinasaba ambavyo leo hii vinachukua nafasi muhimu sana kwenye nyanja za sayansi na maswali mengi yanaibuka kuhusu matumizi ya elimu hii ya Uhandisi wa chembe za vinasaba. Na imebainika katika Baraza kwamba mhimili wa elimu ya uhandisi wa vinasaba ni jinsi ya kuzitambua chembe hai za vinasaba na mjengeko wake na jinsi ya kuvihodhi kupitia kuondosha baadhi yake - kwa sababu za ugonjwa au zinginezo - au kuviongeza au kuvikutanisha vyenyewe kwa vyenyewe; kwa ajili ya kubadilisha sifa zake za kimaumbile zilizorithiwa.
Na baada ya kuangalia kwa kina na kudurusu na kuzungumzia yaliyoandikwa, na katika baadhi ya maamuzi na maazimio yaliyobobewa mikutanoni na katika makongamano. Baraza lilipitisha kwamba:
1- Kuhakikisha maamuzi yaliyotolewa na Baraza la Fiqhi ya Kiislamu, la Umoja wa Nchi za Kiislamu kuhusu (cloni) uzalishaji wa binadamu kwa njia ya vinasaba kwa namba ya 10/D/2/100, katika mkutano wa kumi uliofanyika Mjini Jadah, kutoka tarehe 23 hadi tarehe 28 mwezi wa Mfunguo Tano, mwaka wa Elfu moja mia nne, kume na nane kutoka Hijrah.

2- Kunufaika na elimu ya Uhandisi wa vinasaba katika kujikinga na maradhi au kuyatibu, au kupunguza makali yake, kwa sharti la kutokusababisha madhara makubwa.

3- Haijuzu kutumia aina yoyote ile ya vifaa vya uhandisi wa vinasaba na njia zake kwa malengo maovu na katika kila kinachoharishwa Kisheria.

4- Haijuzu kutumia aina yoyote ile ya vifaa vya uhandisi wa vinasaba na njia zake kwa malengo ya kumchezea chezea binadamu na majukumu yake binafsi au kuingilia mjengeko wa vinasaba kwa madai ya kuboresha kizazi cha binadamu.

5- Haijuzu kufanya uchunguzi wowote au matibabu ya aina yoyote au kuainisha ugonjwa kwa njia zinazohusika na sayansi ya vinasaba vya binadamu isipokuwa baada ya kutathmini kiundani na kwa maelezo yaliyotolewa kabla na faida zake tegemewa zinazofungamana na changamfu za aina hii na baada ya kujipatia ruhusa inayokubalika kisheria pamoja na kuulinda usiri kamili wa matokeo, na kuchunga hukumu za kisheria za Uislamu zilizo bora ambazo zinaheshimu na kulinda haki za binadamu na utukufu wake.

6- Inajuzu kuvitumia vifaa vya sayansi ya uhandisi wa Vinasaba na njia zake katika uwanja wa kilimo na ufugaji wa wanyama, kwa sharti la kuchukua tahadhari zote za kuzuia kutokea madhara ya aina yoyote - hata kwa siku za usoni - kwa binadamu, kwa wanyama au kwa mazingira.

7- Baraza linayatolea wito Mashirika na viwanda vinavyozalisha vyakula na Madawa na vitu vingine, vinavyonufaika na elimu ya uhandisi wa vinasaba na viweke wazi maelezo ya mchanganyiko wa bidhaa hizo; ili kuyashughulikia na kuyatumia katika uthibitisho kwa kuchukua tahadhari kwa yale yenye kudhuru au yaliyoharamishwa kisheria.

8- Baraza la Madaktari na wenye Maabara na Maofisi ya Majaribio mbalimbali yanausiwa kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujihisisha uchungaji wake pamoja na kujiepusha na madhara kwa mtu mmoja mmoja, kwa Jamii na kwa Mazingira. [Al Elaaj Aj Jiniy Min Mandhuur Al Fiqhi Al Islamiy, kwa Dkt. Ali Muhiy Edeen Al Qorah Daghiy].
Kutokana na yaliyotanguliza na katika tokeo la suala: basi yaliyokuwa katika uhandisi wa vinasaba, chochote kinachokuwa na manufaa ya umma kwa ajili ya binadamu, kama kuponesha maradhi na mfano wake basi hicho kinajuzu Kisheria, na kinachokuwa kinyume na hivyo na ambacho kinahatarisha au kudhuru na mfano wake, basi hicho hakiruhusiki Kisheria.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas