Muamala wa Mali Kauli.

Egypt's Dar Al-Ifta

Muamala wa Mali Kauli.

Question

Baadhi ya taasisi za kifedha za Kiislamu zina njia za kisheria zinazomhakikishia mhitaji kukidhi mahitaji yake na kulifikia lengo lake iwe ni kwa kupewa vitu na sio fedha, kama kwa mfano mtu anapohitaji mashine kwa ajili ya kiwanda chake au nyumba kwa ajili ya makazi na kadhalika. Kama ikiwa mtu anahitaji fedha, Mabenki ya Kiislamu yaliukubali muamala huu uitwao Malikauli, na jinsi ulivyo ni kwamba mtu mwenye shida anainunua bidhaa fulani kutoka katika benki kwa malipo yaliyowekewa muda, kisha yeye anaiuza bidhaa hiyo kwa mtu mwingine kwa thamani iliyo chini ya thamani yake ya asili, na mara nyingi inavyokuwa huyu mtu mwingine ni wa kutoka katika benki hiyo. Je, inaruhusiwa kwa mabenki ya Kiislamu kutumia njia hii ya kutunzia pesa kwa wenye kuhitaji, na kwamba njia hii ya juu juu lengo lake ni kwenda kinyume na sheria na haijuzu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
At Tawaruq katika lugha maana yake ni: kutenda kitendo (Warraqa). Na kauli ya uzani wake katika lugha (Tafaulu) ni kipimo cha neno ambalo lina maana ya Mfumo wa Malikauli, huja katika lugha kwa kumaanisha mbadiliko kama vile udongo unapogeuka na kuwa jiwe, na huja kwa ajili ya kukalifisha katika kinachopatikana katika vitendo, na huja kukalifisha kwa maana ya tabu. Na kwa hivyo, neno Malikauli hujulikana kama: Mwelekeo na Juhudi ikiwemo ukalifishaji pamoja na kukusudia fedha. [Mu'jam Maqayyis Al Lugha 101,102/6, Ch. Dar Al Fikr, na Taaj Al Aruos 458,466/26, Ch. Kuwait, na Al Qamuos Al Muheetw 280/ 3, Ch. Al Amitiyah]
Na Tamko la jina hilo halikutajwa katika vitabu vya zamani vya Fiqhi – kwa mujibu wa ujuzi wetu- isipokuwa katika vitabu vya wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Ahmad bin Hanbal, Na dhana yake kwao ni: Ni kununua bidhaa kwa muda maalumu kisha kuiuza papo hapo na kuchukua thamani yake kwa namna ambayo fedha ndio lengo. Al-Mardawi anasema katika kitabu chake cha: [Al-Insaaf 4/337, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Faida: Kama mtu alikuwa anahitajia fedha, akanunua kitu chenye thamani ya mia moja kwa mia moja na hamsini, basi hakuna ubaya wowote. Imeandikwa na - Imamu Ahmad – nayo ni madhehebu yaliyochaguliwa, na Wenzake wameyafuata, nalo ni suala la Tawarruq (Malikauli).
Dhana ya tawarruq (Malikauli) ya Fiqhi inakaribiana na dhana ya suala la: (kuazima) kilugha ni kukopa: na wanazuoni wa Fiqhi wametafsiri kuwa ni mtu kuuza alicho nacho kwa muda maalumu katika kikao cha makubaliano kwa thamani ya hapo hapo; ili asalimike na riba, Na pamesemwa katika aina hii ya uuzaji wa kitu; kwa kuwa mnunuzi wa bidhaa kwa muda maalumu anachukua kitu badala ya bidhaa hiyo; kwa maana ya fedha taslimu hapo hapo. [Al-Misbah Al-Muniir kidahizo cha (Ain) uk. 441, Dar Al-Fikr] Na tofauti baina ya Malikauli na Al-Iinah ni kwamba katika Malikauli mnunuzi anauza kwa mtu mwingine isipokuwa muuzaji, lakini katika Al-Iinah mnunuzi anauza kwa muuzaji mwenyewe.
Mabenki ya Kiislamu yanapitisha aina mbili za mikataba ya Malikauli:
Aina ya kwanza ni: Malikauli ya kweli, na mfumo wake ni: mtu kununua bidhaa kutoka benki kwa malipo yaliyoahirishwa, kisha anaziuza kwa upande mwingine taslimu, ili akidhi haja yake ya fedha.
Aina ya pili ni: Mauziano ya Malikauli yaliyopangika. Muamala huu hukamilika kwa mtu kununua bidhaa kutoka katika moja ya mabenki ya kiislamu kwa muda maalumu, kisha mtu huyo huyo huipa jukumu benki kuiuza bidhaa hiyo kabla hajaitia mikononi kiuhalisia.
Tofauti baina ya Malikauli iliyopangwa na ya kweli ni kuwa: mteja katika Malikauli iliyopangwa hapokei bidhaa hizi wala haziuzi mwenyewe, wakati mteja katika Malikauli ya kweli ana hiari kuchukua bidhaa au kuziuza mwenyewe katika soko, kwani kuzichukua bidhaa hizo kunamwezesha kufanya anavyotaka. Baadhi ya benki zinaweza kumwekea mteja aina mbali mbali za miamala za kuchagua katika mfano wa Malikauli uliopangika vyema; kwa lengo la kumfanya achague baina ya kupokea bidhaa yeye mwenyewe au kuipa benki uwakala wake au hata kuupa upande mwingine wa tatu wenye uhusiano na benki kwa ajili ya kuiuza bidhaa hiyo. [Rejea: Malikauli ya kweli na aina zake, kwa Dkt. Ibrahim Al-Dabo uk 2, utafiti wa Mkutano wa kumi na tisa ya Baraza la Fiqhi ya Kiislamu la Kimataifa lililofanyika katika nchi ya UAE.].
Ama aina ya kwanza ya Malikauli, ambayo watafiti wa sasa wanaiita Malikauli ya kifiqhi, wengi wa wanavyuoni wanairuhusisha, na maana yake ni kwamba: ile iliyopitishwa na madhehebu ya Imamu Abu Hanifa ni kuwa mauzo ya Al-Iinah yanachukiza [Al-Hidayah pamoja na maelezo yake Fathul Qadiir 7/211, Dar Al-Fikr].
Imamu Al-Kamal aliyapa madhehebu uhuru katika suala hili, alisema katika «Fathul Qadiir» [7/212, 213] baada ya kutaja aina za kuuza kwa muamala wa Al-Iinah: “Kinachotuka moyoni, hakika mambo yalivyo, hukitoa mlipaji ikiwa kitafanywa kwa sura inayomrejea mwenyewe au sehemu yake…. Ni mwenyekulazimishwa, na kama sio hivyo basi hakuna kulazimishwa isipokuwa tofauti na ya mwanzo kwa baadhi ya uwezekano; Ni kama vile mtu mwenye kudaiwa akawa anahitaji na afisa akawa anakataa kumkopesha bali anataka amuuzie kitu chenye thamani ya kumi kwa kumi na tano kwa muda watakaokubaliana, kisha akakinunua mwenye madeni na kukiuza sokoni kwa ile thamani ya kumi, na wala hakuna ubaya wowote katika jambo hili; kwani muda uliopangwa umekabiliana na sehemu ya malipo, na mkopo sio daima wajibu kwake, bali ni Sunna, Na iwapo ataacha kwa utashi tu kutoka kwake kuelekea katika nyongeza ndogo basi huko kunachukiza, au akaacha kwa pingamizi linalomwia ugumu basi haichukizi, hakika mambo yalivyo, hali hii hujulikana kuwa ni katika sifa maalumu za vitu, na kama kile kitu chenyewe kilichotoka kwake hakikurejea, basi hiyo haiitwi uuzaji wa kitu chenyewe; kwani hicho ni katika vitu vinavyorejeshwa sio chenyewe kwa sifa ya uwazi na kama sio hivyo basi kila uuzaji ni uuzaji wa kitu chenyewe..”
Wanavyuoni wa madhebu ya Imamu Malik hawakutaja suala la Malikauli moja kwa moja, na anayekaribia suala hili analitaja chini ya uuzaji wa muda. Sheikh Al-Dardiir anasema katika [Al-Sharhul Kabiir Limukhtasar Khaliil]: Kipambanuzi katika mauziano kwa kupeana muda: ni mauziano ambayo kwa uwazi wake ni halali lakini hupelekea katika yanayokatazwa, na kwa ajili hiyo, amesema: na imezuiwa kwa Madhehebu ya Maalik na Wafuasi wake kutokana na tuhuma kwa maana ya muda uliodhaniwa kuwa kilichokusudiwa ndani yake kimezuiliwa Kisheria; kwa ajili ya kuziba mwanya wa kukosea, kwa maana ya mauziano yanayojuzu kwa uwazi wake yaliyoyazidi malengo yake. Kwa maana ya kwamba Watu wengi wameikusudia kwa ajili ya kuifikia riba inayokatazwa kisheria, na hiyo ni kama vile (kuuza na kukopa), yaani kama vile mauzo yanayojuzu katika uwazi unaelekea kwa kuuza na kukopa. Hakika mambo yalivyo, tuhuma inayokatazwa ni kwamba njia hizo mbili za kuuza na kukopa zinazuiliwa. Kisha akasema: kwa kuwa yaliyotangulia ni ufunguzi wa mauziano kwa njia ya kupeana muda wa kulipa, ameyafuatanishia kwa maelezo juu yake na kinachokuwa na moja ya sababu mbili zilizotangulia kutajwa huzuiliwa, na kama sio hivyo basi haizuiliwi kwa kauli yake: (Na atakaeuza) kwa kunyoosha au mshabaha (kwa muda Maalumu) kama vile Mwezi mmoja, (kisha akainunua) kwa maana muuzaji akakinunua au aliyechukua nafasi ya muuzaji au wakili wake, au kwa idhini yake, bidhaa yenyewe aliyomuuzia mnunuzi au wakili wake (kwa jinsi ya bei yake) ambayo aliiuza kwa bei hiyo na aliibainisha, kwa kauli yake: (Kama kitu kinachoonekana)… (chakula)…na (kuonesha), ima anunue (kwa fedha taslimu au kwa Malikauli), hii ni ya kwanza, (au) kwa Malikauli iliyo kidogo kuliko hiyo (au zaidi yake), basi hizi ni hali nne kwa upande wa Malikauli na katika kila moja miongoni mwazo ima ainunue bidhaa (kwa thamani inayolingana) na ya mwanzo, (au kidogo) kuliko hiyo, (au zaidi ya hiyo), atajipatia sura kumi na mbili ambapo (kati ya hizo, tatu zinakatazwa na hizo ni zile zinazo kuwa na bei ndogo ndani yake)…. Na kwa mujibu wa sura tisa zilizobakia zote zinajuzu.
Na Sheikh Ad Desoqiy amesema katika kitabu chake: [Hashiyat Ad Desoqiy] akisema: "(Kauli yake: Na kinachokusanya moja ya sababu mbili zilizotangulia), kwa maana ya kuuza na kukopa, na kukopa kwa kutaka manufaa. (Kauli yake: na atakayeuza kwa Malikauli …) mpaka mwisho, ameashiria Mwandishi kwa kauli hii kwamba masharti ya mauziano ya Malikauli yanayoingia katika tuhuma ni matano: Yawe mauziano ya awali kwa Malikauli, na kama itakuwa kwa pesa taslimu basi yatakuwa ya pili ya kwa pesa taslimu au kwa Malikauli, na yote mawili hayamo katika mlango huu, na mnunuzi awe wa pili ndiye mchuuzi wa kwanza, na mchuuzi awe wa pili na mnunuzi wa kwanza au atakaechukua nafasi yake wa mwanzo ndiye mnunuzi wa pili au atakayechukua nafasi yake. Kwa hiyo nafasi ni ya kila mmoja na wakala wake ni sawa sawa kwa kujua wakala wa kuuza kwa mwingine au kununua kwake au kutojua kwake, na aina ya thamani ya manunuzi ya wa pili iwe ni aina ya thamani yake ya kwanza ambayo ameitumia kuuzia kwanza. [Asharhu Al Kabeer kwa Hashiyat Ad Desoqiy 76,77/3, Ch. Dar Ihyaa Al Kutub Al Arabiyah]
Na wanazuoni wa Madhehebu ya Shafi wanaona Kutokuwapo uharamu kukiuza kitu chenyewe, na wanakitaja katika jumla ya Mauziano yanayochukiza, na ni bora zaidi kutumia mfumo wa Malikauli; na hii ni kwa kuwa kukiuza kitu chenyewe, ni kuwa mnunuzi aliyenunua kwa kupewa muda anakiuza hapo hapo kwa yule yule aliyemuuzia. Ama picha nyingine ya Malikauli ni kwamba mununuzi anaiuza bidhaa kwa mtu mwingine asiyekuwa muuzaji wake wa kwanza kutoka kwa muuzaji huyo huyo.
Imamu Nawawi anasema katika kitabu cha: [Ar Rawudhah 416,417/3, Ch. Al Maktab Al Islamiy]: Kipambanuzi: sio katika vinavyokatazwa kuuzwa kwa muhula. Kuuza kwa muhula ni mtu kumuuzia mtu mwingine kitu kwa thamani itakayotolewa baadaye na kukabidhiwa kitu hicho, kisha akakinunua kabla ya kupokea malipo yake yaliyo chini ya thamani yake ya asili, kwa fedha taslimu. Na hivyo hivyo, inajuzu kuuza kwa thamani ya fedha taslimu na akanunua zaidi kutoka kwake hadi muhula wa malipo waliopangiana, iwe ni kwa kukabidhi thamani ya awali au la, na ni sawa sawa kitu hicho kitakuwa cha kawaida kwake aghalabu ndani ya nchi au la, basi muamala huo ni sahihi na unayojulikana katika vitabu vya wataalamu wetu."
Ama Madhehebu ya wanavyuoni wa Madhehebu ya Hanbali; hukumu wanayoitegemea ya Malikauli ni kujuzu. [Tazama kitabu cha: Kashaafu Al Qinaa' 186/3, na kitabu cha Al Inswaf 337/4, na kitabu cha: Sharhu Muntaha Al Iradat 26/2, Ch. Alam Al Kutub].
Na dalili ya kauli hiyo, ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba} [AL BAQARAH 275}. Na Mauziano katika Aya Tukufu ni tamko pweke lenye alifu na lamu katika lugha ya Kiarabu, nalo huhukumia katika ujumla na ujumuishaji wa aina ya kitu au umbile la kitu ikiwa halikuthibiti kwake ahadi kiakili au kumbukumbu, na hayo ni kadhalika katika Aya Tukufu. Na kwa hayo, humaanisha uhalali wa kila kinachoingia ndani yake na kutambulika kama mauziano, na wala hakitengeki katika hayo isipokuwa kinachotengwa na Sheria.
Imamuu Al Qutwubiy anasema katika tafsiri yake [256/3, Ch. Dar Al Kutub Al Maswriyah]: alipoongea juu ya Aya hiyo Tukufu: "Hii ni katika ujumla wa maana za Qur`ani Tukufu. Na alifu na lam ni za Umbile na wala sio za Ahadi; kwani hayakutangulia Mauziano yaliyotajwa yanayorejea katika maana hizo... Na ikiwa itathibitika kwamba mauziano ni ya jumla basi yatakuwa maalumu kwa kile tulichokitaja ambacho ni riba na mengineyo yanayokatazwa na kuzuia kufanyiwa mikataba; kama vile mvinyo, mzoga, na kuuza kilichokuwapo katika mimba ya mnyama, na nyinginezo miongoni mwa zilizothibiti katika Sunna na Ijmai ya umma yanayokatazwa na hayo ni madhehebu ya Wanachuoni wengi wa Fiqhi".
Na hakuna andiko lililopokelewa Kisheria au kwa Ijmai ya wanazuoni linalouzuia Muamala wa Malikauli. Na Muamala huu uko ndani ya kinachoitwa mlango wa Kuuziana; kwani muamala huu ni kuinunua bidhaa kwa deni kisha kuiuza bidhaa hiyo papo hapo, nao ingawa mara nyingi ndani yake huwa kuna hasara ya thamani ya malipo yanayotolewa baadae, isipokuwa hasara hii hulipika kwa kile kilichotokea ndani yake kwa kurahisisha jambo lake na kukidhi mahitaji yake. Ujumla wa Aya Tukufu unaligusia suala hili, na asili katika Miamala ni kuidhinishwa mpaka ipatikane dalili ya wazi inayothibitisha kinyume na hivyo; kwani Asili ndani yake ni kuzigeukia maana zingine bila kufanya Ibada.
Na Masheikh wawili walipokea kutoka na Abu Saidi Al Khudriy na Abu Hurairah R.A, kwamba Mtume S.A.W, alimtuma mtu mmoja wa Khaibar, basi akaja na tende za aina ya Junaib, basi Mtume S.A.W, akasema: "Je, tende zote za Khaibar ni kama hizo?" Mtu huyo akasema: hapana! Wallahi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu sisi tunachukua kibaba cha tende hizi kwa vibaba viwili na vibaba viwili kwa vibaba vitatu kwa tende hizo. Basi Mtume S.A.W., akasema: "Usifanye hivyo, ziuze tende zako zote kwa dirhamu kadhaa kisha ununue tende bora kwa dirhamu kadhaa. Na mwelekeo wa dalili inayotokana na Hadithi: Ni kwamba Mtume S.A.W, aliwaongoza Maswahaba wake kuelekea katika njia ya kujiweka mbali na riba kuelekea katika njia ya kulifikia lengo la mwenye tende mbaya ili ajipatie tende bora pamoja na kuzidiana baina ya pande mbili kwa kiasi bila ya kuwa njia ya lengo hili ni haramu. Na hivyo ni kwa mikataba miwili tofauti iliyo mbali mbali kabisa na kinachoiharibu, na wala haifanani na riba kwa kitu chochote, ingawa matokeo ya Muamala huu hupelekea mwishoni matokeo yale yale ambayo Muamala ulikuwa ukifanyika kwa riba (kibaba) kimoja kwa vibaba viwili hiyo ikawa inamaanisha kwamba inajuzu mauziano hayo ambayo yanapelekea kulifikia lengo kutokana nayo ikiwa ni kwa njia za kisheria zilizo mbali na kuwa kwake kama sura za miamala zilizoharamishwa.
Al Hafedh Ibn Hajar amesema katika kitabu chake: [Fateh Al Baariy 326/12, Ch. Dar Al Maarifah]: "Hila ni njia za kupelekea kwenye lengo kwa siri, nazo kwa wanazuoni zinagawanyika sehemu kadhaa kwa kulingana na mtumiaji, Na katika hila mbalimbali kuna njia za kutokea katika dhiki, na miongoni mwazo ni uhalali wa dharura, hakika mambo yalivyo ndani ya dharura kuna kuepukana na madhambi makubwa, na vilevile Masharti yote hakika ndani yake kuna kusalimika na kuangukia katika uzito, na miongoni mwake ni Hadithi ya Abu Hurairah na Abi Saidi katika kisa cha Bilal: "Ziuze zote kwa ujumla kwa dirhamu kisha ununue tende bora kwa dirhamu kadhaa."
Kwa hiyo kuamiliana kwa Muamala wa Malikauli kwa ajili ya kutaka kujipatia mzunguko wa fedha wa kutosha kunajuzi, na kwa kuwa matokeo yaliyotokana na Muamala kama huo yanayofanana na matokeo ya Muamala unaofanyika kwa kununua Kibaba kimoja kwa Vibaba viwili, hayaathiri kitu katika kujuzu kwa muamala huu na kuhalalika kwake, Kwa kuwa kwake jinsi Mtume S.A.W alivyoongoza - kumetokea kwa mikataba miwili inayojitegemea na inayokubalika kisheria na wala haihusiani kwa uhusiano wowote kwa upande wa kushurutisha, na kwa hivyo ikabainika kwamba kushabihiana mkataba unaokubalika kisheria kwa mwingine unaozuiwa hakutoshi kutoa tamko la uharamishaji wa Kisheria.
Inaongezewa kwa hayo: Ni kwamba mauziano kwa Muamala wa Malikauli yana mfanano na kuwa kama mialama mingi ya mauziano ambayo sio haramu. Na inajulikana kuwa biashara inajengeka kwa uwepo wa mzunguko wa fedha kwa njia ya kutafuta faida; na kwa ajili hiyo, utaona kwamba mfanyabiashara ana njia nyingi za kuchagua jinsi ya kuugeuza mtaji wake na kuwa mauziano kwa fedha taslimu na kwa mali, na anaweza kununu kwa fedha taslimu na akauza kwa Malikauli au kinyume chake. Na hakuna tofauti yoyote ya kuwa lengo lake katika hayo ni kunufaika kwa kinachouzwa, au kupata faida kutokana nacho au kujipatia mzunguko wa fedha unaohitajika kuzungusha mtaji, na yote hayo ni masilahi yanayozingatiwa hayafutwi na Sheria wala Sheria haiyahukumu kuwa ni batili.
Ama aina ya pili kutoka katika aina za miamala ya Malikauli: ni (Mauziano ya Malikauli yaliyopangika); basi hayo ni halali pia, na dalili ya hayo ni:
Kwanza: Dalili zalizotangulia za kujuzu kwa Miamala ya Malikauli ya kifiqhi, na kwa hivyo basi benki ikiwa inamiliki bidhaa kisha ikaziuza kwa mteja wake, halafu mteja akakabidhi pesa zake kisha mteja akaziuza kwa njia ya benki, basi hakuna matata, na mteja akiwakilishia benki kwa kukabidhi kwa niaba yake basi hakuna uzito pia, kutokana na usahihi kutoka kwa Madhehebu ya wanazuoni wa kihanbali, kwamba inajuzu kwa kuwakilisha mnunuzi kwa muuzaji kukabidhi bidhaa zilizouzwa [Kitabu cha: Al Iswaaf 469/4]. Bali pia inajuzu kwa benki kuziuza bidhaa kwa niaba ya mteja baada ya mteja kuiwakilishia benki katika kukabidhi bidhaa kwa niaba yake. Na Wanazuoni wa Fiqhi wa Madhehebu ya Shafi walikubaliana kujuzu kwa Muunganiko wa anayewajibisha na anayekubalika katika njia kama hizo.
Az Zarkashiy anasema katika kitabu cha: [ Al Manthuur 88,89/1, Ch. Wizara ya Waqfu ya Kuwait] na Tazama: kitabu cha Al Ashbaah wa An Nadhaa'r Uk. 280, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]: "Muunganiko wa anayewajibisha na anayekubalika unazuilika isipokuwa katika masuala mawili... (ya Pili) na anapompa mtu uwakala katika manunuzi na akamwidhinisha katika manunuzi hayo yeye mwenyewe na kisha akakisia thamani na akamzuia kuongeza, basi katika takwa hili, kwamba inapasa kujuzu; kwa kuwa Muunganiko anayewajibisha na anayekubalika hakika yake huzuia kwa ajili ya uwepo wa tuhuma, kwa dalili ya kujuzu katika hali ya baba na babu".
Bali inajuzu kwa benki kuziuza bidhaa kwa niaba ya mteja hata kama benki inajiuzia, au kwa mamlaka inayohusiana nayo, kutokana na simulizi moja miongoni mwa simulizi mbili, kutoka kwa Imamuu Ahmad kuhusu kujuzu mauzo ya mwenye wakala kwa nafsi yake, na alieichagua rai hii miongoni mwa wanazuoni wa Madhehebu ya hanbali ni Ibn Abduus katika kitabu chake: [At Tadhkarah], na Ibn Qadhiy Aj Jabal aliitanguliza rai hii katika kitabu cha: [Al Fai'q]. Tazama: [Kitabu cha: Al Feruo' 354/4, Al Inswaaf 376,376/5]
Basi kama itasemwa: hayo yanaielekea njia ya Uuzaji kwa malipo ya baadaye, na hiyo ni haramu katika sheria, kwa Hadithi iliyopokelewa na Ibn Omar R.A, kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Mtakapouziana kwa njia ya Uuzaji kwa malipo ya baadae kisha kuinunua tena bidhaa hiyo hiyo kwa bei ya chini, na mkaichukua mikia ya ng'ombe na mkaridhia kwa mazao na mkaacha Jihadi basi Mwenyezi Mungu Mtukufu Atakushushieni udhalili ambao hautaondoka isipokuwa kwa kurejea kwenu katika Dini yenu". [Imepokelewa na Ahmad na Abu Dawud] Tukasema: Hatuukubali uharamu wake kisheria, na dalili ya kujuzu kwake ni Hadithi ya swahaba ambaye alikuja na tende bora kutoka Khaibar, iliyotangulia kutajwa kwake, na ndani yake kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa mtu huyo: "Ziuze zote kwa ujumla kwa dirhamu kisha unumue tende bora kwa dirhamu kadhaa." Na Hadithi hiyo yenye maana huru, Mtume S.A.W, hakutofautisha baina ya sura ya kuingia kwa mtu wa tatu katika mauziano Na sura iliyopo, ni kwamba mauziano yakamilike baina ya Watu wawili bila ya uwepo wa mtu wa kati wa watatu wao. Na Msingi ni kwamba kilicho huru kinakuwa huru hivyo hivyo mpaka panapopatikana kitakachokifunga.
Imamuu An Nawawiy anasema katika kitabu cha: {Sharh ya Muslim 21/11. Ch. Dar Ihiyaa At Turath Al Arabiy]:
"Na wenzetu waliitumia Hadithi hii kama hoja pamoja na wale walioafikiana nao ya kwamba Suala la Uuzaji wa bidhaa kwa malipo ya baadae kisha kuinunua tena kwa bei ya chini, sio haramu, nao ni ujanja unaotumiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kulifikia kusudio la riba. Kwamba anataka kumpa dirhamu mia moja kwa dirhamu mia mbili, basi anamwuzia nguo kwa mia mbili kisha anainunua kwa mia moja, na mahali pa dalili kutoka katika Hadithi hiyo: Mtume S.A.W, amesema: Uzeni hii na nunueni kwa bei yake kutokana na ile! Na hakutofautisha baina ya kwamba anunua kutoka kwa mtu aliyenunua au kutoka kwa mtu mwingine, basi hiyo ni dalili ya kwamba hakuna tofauti, na hayo yote si haramu katika madhehebu ya Shafi na wengineo.
Na Hadithi inayotumiwa kwa dalili ya kuharamisha haithibiti. Kwani katika Isnadi yake kuna Abdu Abdulrahman Al Kharasaniy Ishaq Bin Aseed, Abu Hatem akasema juu yake: Yeye ni sheikh si mashuhuri na hashughuliki naye. Na Ibn Udaiy akasema: Yeye si maarufu, na Ibn Hayaan akasema: anakosa, na An Nabatiy akataja katika kitabu cha: [Dhail Al Kamel] kwamba Al Azadiy akasema juu yake: Munkari ya Hadithi ikaachwa. [Tahzeeb At Tahzeeb 198/1, Ch. Da'irat Al Maarif An Nedhamiyah katika Uhindu].
Na Ad Dhahabiy akazingatia katika kitabu cha: [Al Mizaan] kwamba Hadithi hiyo ni miongoni mwa Hadithi zake za Munkari. [Mizaanu Al I'tedaal 547/4, Ch. Dar Al Maarifah]. Na At Taqiy As Subkiy akaashiria kuidhoofisha katika kitabu cha: [Takmelat Al Majmuo' 145/10].
Ya Pili: Ni kuwa Muamala wa Malikauli kwa njia ya benki ni mkataba wenye Nguzo za Masharti yake ya wazi na yenye kuzingatiwa katika Mkataba wa kuuziana kwa namna ambayo huwajibisha kusihi kutokana nayo. Basi kauli ya Mtume S.A.W, "Uza Bidhaa zote kwa dirahamu…. Hadithi", ni sahihi na inatoa dalili, kwani asili katika mikataba ni kuhakikisha sura yake ya kisheria, mbali ya nia ya wenye mikataba, na asili katika kuzingatia mikataba ni maneno na siyo maana.
Na katika hilo, kinachofuatwa hapo ni tamko la Mkataba na sura yake, na wala sio nia zake na makusudio yake, na utakapothibitika usahihi wa Mkataba basi kiasili ni kwamba hulazimu kujuzu kutokana na kusihi huko. Kwani usahihi ni inayoendana na kutuka kwa kitendo chenye pande mbili za Kisheria, na kwa kuwa kwake kitu kinachoendana na sheria inapelekea kuwa ni kilichoidhinishwa ndani yake. Na idhini hiyo inapingana na zuio ambalo linaelekea katika uharamishaji.
Ya Tatu: Mkataba wa Malikauli ni mkataba unaohitajika sana kwa sasa, na haja ya mkataba huu inazingatiwa, na ni kama mikataba mingine na aina zake za kuzungusha fedha kiislamu na unazingatiwa ni mbadala wa miamala mingi ifanyikayo kinyume cha sheria katika benki za kawaida. Vile vile katika utekelezaji wa mfumo huu kwenye benki, serikali zinakuwa na uwezo wa kuzuia kile kinachoitwa (nakisi ya biashara), badala ya kuziba pengo hilo kwa njia zilizoharamishwa kisheria kama vile maidhinisho ya Hazina. Na kuweka sababu kujuzu huko kwa madai.
Al Imamuu As Sarkhasiy anasema katika kitabu cha: [Al Mabsuotw 75/15]: "Na mahitaji ya watu ndio asili ya Sheria ya Mikataba, kwa kuweka Sheria kwa namna ambayo hukidhi mahitaji hayo ya Watu, na kuafikiana na Misingi ya Sheria.
Bali kwamba mahitaji hayo hayakanushi uharamu tu bali pia yanakanusha ukaraha ambao wanazuoni wa kishafi wa baadae waliyataja katika kuuza kwa Malipo ya baadae, kwani ukaraha unafutwa kwa mahitaji, kama alivyosema Mwanachuoni mkubwa Assfariniy katika kitabu cha: [Ghezaa Al Albab 323/1, 342/1, 18/2, Ch. Mu'sasat Qurtubah, Misri].
Haisemwi kwamba Hakika mfumo huu uliopangika wa Malikauli kupitia benki una utata ndani yake wa uhalalishaji wa kilicho haramu, ambapo una ndani yake mwingiliano baina ya Mgharamiaji na Mwombaji wa Malikauli kwa uwazi au kwa kukusanya, au kwa kuzoeleka, unalenga kufanya hila ili kujipatia fedha zilizopo kuliko zilizotakiwa katika dhima na hiyo ni riba. Kwa hiyo bidhaa katika Malikauli kamwe hailengwi, bali hakika mambo yalivyo, bidhaa imeingia kwa ajili ya kuhalalisha uchukuaji wa fedha za haraka kwa fedha nyingi zitakazotolewa baadae, kwani hiyo ni hila ya kukifikia kilichoharamishwa, basi haijuzu. Na jawabu lake ni kama ilivyotangulia kwamba tuliamua kuwa zingatio katika mikataba ya mauziano kwa uwazi na kwa matamshi, kwani nia za watu na malengo yao ni mambo ya ndani; kwa hiyo tamko ndilo linalozingatiwa; kwani hilo ndilo liko wazi na linadhibitika.
Al Imamuu Al Mawardiy anasema katika kitabu cha: [Al Haawiy 642/5, Ch. Dar Al Fikr] katika kujibu kwa aliyeharamisha mauziano ya Malipo kwa awamu: "Na Ama kujibu kwa kauli yao kwamba hiyo ni sababu inaelekea katika Riba ya haramu basi ni kosa, bali hiyo ni sababu inayoizuia Riba ya haramu, na kilichouzuia uharamu kilikuwa ni Sunna".
Na haisemwi pia: Hakika mfumo huu una mauziano kabla ya makabidhiano, na haujuzu kisheria; kwa kuwa sisi hatusalimu amri kwamba makabidhiano hayajatokea, bali yametokea kihukumu kwa kule mnunuzi kuupokea mkataba unaotoa nafasi isiyo na kikomo ya kukitumia atakavyo kilichonunuliwa. Na kilichoandikwa ndani yake kina sifa zinazoiainisha bidhaa husika; kwani kukabidhiana katika kila kitu kunakuwa kwa mujibu wa jinsi kitu hicho kilivyo kama wasemavyo wanazuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi. [Tazama: Hashiyat As Shabramalsiy Ala Nihayat Al Muhtaaj 290/5, Ch. Dar Al Fikr]
Na kauli ya kwamba lazima pawepo makabidhiano halisi kwa maana ya kupokea kwa mkono, na kama siyo hivyo makabidhiano hayo hayatakuwa sahihi na hayawi zaidi ya kuwa jambo la kufikirika (mawazo) tu na lipo mbali mno na maana za Kisheria. Mauziano ya aina hii yanaweza kuwekwa katika mazingira ya kuwa miongoni mwa kuuza Kitu kisichokuwepo. Na hii inajuzu iwapo kitu hicho kitajulikana kilivyo na aina yake pamoja na sifa zake; kwa kuondoka shaka kwa wakati huo. Na ilivyo ni kwamba mkataba wa awali wa kuuziana unakamilika baina ya benki na muhusika wa Malikauli, kisha benki inaweka uwakala wa mnunuzi wa Malikauli katika upokeaji wa bidhaa isiyokuwepo hapo kisha kuiuza, kwa hiyo makabidhiano hapa yanatokea kiuhalisia kwa njia ya wakili, na mauziano ya pili hayawi mauziano ya kabla ya makabidhiano.
Kisha hakika ugumu wa mnunuzi kupokea bidhaa yeye mwenyewe au kutowezekana kufanya hivyo baadhi ya nyakati hakuhukumii kutokuwepo kwake: kwa kuwepo uwezekano wa kutokea makabidhiano ya bidhaa hiyo kupitia wakala wake, kuna uwezekano mkubwa pakawepo kwa Wakili, mambo na madaraka ambayo yanakufanya kuamiliana na pande mbalimbali za kuuza na kununua kuwa nyepesi zaidi kuliko kuamiliana moja kwa moja baina ya aliye na wakili na pande hizo. Na mfano wa hayo ni kipofu kuwakilishwa na anaeona katika manunuzi ya bidhaa na kukabidhiwa pamoja na kuiuza.
Basi kutokana na maelezo hayo; inadhihirika kwamba Muamala wa Malikauli kwa aina zake zote mbili; ya kifiqhi na ya kibenki ni halali, lakini kwa kuzingatia udhibiti wa mambo yafuatayo:
1- Kwamba muuzaji wa kwanza awe anaimiliki bidhaa kabla ya kuiuza kwa mnunuzi; kwa sababu ya kuzuia uuzaji wa kitu asichonacho mtu, na kwa hivyo basi, kutoka kwa Hakiim Bin Hezaam R.A, amesema: nilienda kwa Mtume S.A.W, na nikasema: mtu mmoja alinijia na akaniuliza kuhusu kukiuza kitu nisichokuwa nacho, nimnunulie sokoni na kisha nikiuze? Akasema: "Usiuze usichokuwa nacho" [Imepokelewa na Maimamu wanne].
2- Mtu asinunue bidhaa isipokuwa baada ya kuitia mkononi kwa uhakika au kwa hukumu, kwani kama hajakitia mkononi basi umiliki wake unakuwa haujatulia na kukamilika kwa kilichonunuliwa. Na Mtume S.A.W, amekanusha kwamba bidhaa haziuzwi katika pahali pa kununua, mpaka wafanyibiashara wazimiliki katika mahali pao. [Imepokelewa na Abu Dawud]. Na amesema Hakiim Bin Hizam; aliposema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi ninanunua vitu vinavyouzwa, ni kipi kilicho halali kwangu na haramu kwangu katika vitu hivyo? Na iwapo utanunua kilichouzwa basi usikiuze mpaka ukitie mkononi, [Imepokelewa na Ahmad]. Na inajuzu katika hayo kwamba mnunuzi anaweza kumwakilisha. Kama ilivyokubaliwa hapo juu.
3- Kwamba bidhaa inayouzwa iwepo papo hapo na sio ya kucheleweshwa, isije ikawajibisha kuuza deni kwa deni. Na imepokelewa na Ibn Omar R.A., wote wawili, kwamba Mtume S.A.W., amekanushia kuuza deni kwa deni. [Imepokelewa na Ad Darqutwuniy lakini kwa Isnadi yake dhaifu. Lakini Imamu Ahmad akasema: siyo katika hayo ni Hadithi sahihi, lakini mkusanyiko wa watu juu ya kwamba haijuzu kuuza kwa deni kwa deni. Na amefasiri manaa ya kuuza (Al Kali) kwa maana kuuza kwa deni kwa deni.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas