Muamala mbaya kwa Mke

Egypt's Dar Al-Ifta

Muamala mbaya kwa Mke

Question

Mume wangu ananifanyia muamala mbaya. Nini Hukumu yake?

Answer

Muamala mbaya anaoufanya mume kwa mkewe haujuzu kisharia; Uislamu umeamrisha mume kuishi vizuri na mkewe, na Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameeleza kuwa maisha ya ndoa yamejengwa kwa mapenzi na huruma, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: “Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wakezenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri” [Al-Roum:21]. Na Mtume S.A.W. amefanya kipimo cha ubora katika waume ni muamala mzuri kwa wake zao, Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Bibi Aisha R.A. kwamba Mtume S.A.W. amesema: “Mbora wenu ni yule aliyebora kwa familia yake, na mimi mbora wenu kwa familia yangu” imepokelewa na At-Tirmidhy.

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas