Ufumbuzi wa Kuacha Vitendo vya Puny...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ufumbuzi wa Kuacha Vitendo vya Punyeto.

Question

Ni upi ufumbuzi wa kuacha vitendo vya punyeto? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, Jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mazoea: ni kujizoesha kufanya kitu mpaka kikawa kawaida yako na kuendelea kukifanya kitu hicho mara kwa mara. [Al Mu'jam Al Wasetw 635/2, Ch. Dar Ad Da'wah]
Na mwenye mazoea ni mtu anayeyahifadhi mazoea hayo. [Al Muhkam kwa Ibn Sayidah 321/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Mazoea: ni kitu wanachoendelea watu kukifanya kwa mujibu wa akili na wakakirejea kwa kukikariri mara kwa mara. [At Ta'refaat kwa Aj Jurjani, Uk. 149, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na usiri ni kutokana na kukificha kitu. Al Laith anasema: "Siri: Siri: ni kitu kinachofichikana na kuwa moyoni mwa mtu: kwa maana ya kukifanya kwa kificho kiwe kitu hicho ni kizuri au kibaya". Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Na watakapoiona adhabu wataficha majuto yao. Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa}. [YUNUS 54]. Al Farraa' akasema: "Yaani wakaificha". [Tahdheeb Al Lughah 201/12, Ch. Dar Ihiyaa Al Kitabu Al Arabiy. Kwa mtindo mwingine]
Basi mazoea ya kisiri ni jambo fulani mtu analolizoea na akawa analirudiarudia siri. Kinachokusudiwa hapa: Ni kujizoesha kujitoa manii bila ya kumwingilia Mwanamke, kwa kutumia kiganja cha mkono na mfano wake, kwa siri na mara nyingi.
Kujitoa manii kwa mkono ikiwa ni kwa kuleta fikra za matamanio ni haramu kwa ujumla wake, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ambao wanazilinda tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka. [AL MUMINUUN 5-7]
Na anayetaka kinyume cha haya ni mwovu na hao ndio warukao mipaka. Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuhalalisha kujistarehesha isipokuwa kwa kumwingilia mke, au kijakazi, na kinyume na hayo ni haramu.
Na katika kauli kwa wanazuoni wa Madhehebu ya Hanafi na Shafi pamoja na Imamu Ahmad: Kwa maana ya kuchukiza kunakokatazwa. na ikiwa kujitoa manii kwa mkono kwa ajili ya kutuliza matamanio yaliyopindukia kiwango cha juu, ambapo panahofiwa kwa matamanio hayo kutumbukia katika uzinzi, basi inajuzu kwa ujumla wake, bali imesemwa kuwa ni wajibu kufanya hivyo. Kwani kufanya hivyo kwa wakati huo kunakuwa ni kufanya kilichokatazwa ambacho kimehalalishwa kwa dharura, na ni njia ya kufanya chenye madhara madogo kati ya vitu viwili vyenye madhara.
Na katika kauli nyingine ya Imamu Ahmad; Ni kwamba inakuwa haramu kama atachelea uzinzi; kwani yeye ana nafasi ya kufunga kama njia mbadala, na vile vile ana nafasi ya kuota kunakoyapunguza matamanio. Na ibara za kimaliki zinamaana ya maoni mawili: Kujuzu kwa ajili ya dharura, na uharamu kwa ajili ya kuwapo njia mbadala ambayo ni kufunga. Na Ibn Abdeen miongoni mwa wanazuoni wa Madhehebu ya Hanafi, anaona ya kwamba, ikiwa itajulikana kuwa hiyo ni njia ya kuepusha uzinzi basi itakuwa wajibu kwake. [Al Mauso'ah Al Fiqhiyah 98/4, Ch. Wizara ya Mambo ya Waqfu ya Kuwait]
Na kuzijua njia mbali mbali za kuacha kitendo cha punyeto ni muhimu sana; ili kuyaepuka mazoea hayo. Na ya kwanza na iliyo muhimu miongoni mwa njia mbadala ni dua na kumnyenyekea Mwenyezi Mungu Mtukufu akuepushe na mazoea haya mabaya. Ibn Atwaa' Allah As Sakandariy amesema: "Hakuna chochote unachokitaka wewe mwenyewe kikawa chepesi, na hakuna chochote unachokitaka kutoka kwa Mola wako Mlezi kikasita kukufikia." [Sharhu Al Hekam Al Atwa'iyah kwa Zaruoq Uk. 57, Ch. Dar As Sha'ab] na umwombe Mwenyezi Mungu Mtukufu dua ya wenye shida. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapomwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia.} [An Naml 62]
Na miongoni mwa njia hizo ni: Kuyatambua madhara yake kinafsi, kwa kuwa na hisia za kuvunjika moyo na kuhisi dhambi na kupungua hamu ya kutaka kuoa na kutojali ndoa. Na baada ya kuoa, kuishi bila ya kustarehe kwa kumwingilia mke, na kubadilisha uingiliali wa mke kwa punyeto. Na kama ukiyajua madhara yake haya ya kisaikolojia kabla ya ndoa na baada yake, litakuwa jambo muhimu sana.
Basi harakisha kuleta mabadiliko, kwani kubabaika, na kuchelewesha mabadiliko hayo na kuleta sababu na nyudhuru nyingi, huongeza nguvu ya Mazoea katika nafsi, na huwa vigumu mno kuibadilisha na huwa kama vile hali ya mgonjwa aliyecheleweshewa matibabu ya ugonjwa wake mpaka ugonjwa huo ukazidi na kummalizia maisha yake. Na kuanzia hapo ni muhimu sana kuharakisha kuleta mabadiliko katika kipindi cha ujana; kwani Mazoea ya kila aina yanapoota mizizi katika nafsi na kukomaa huwa vigumu kuyabadilisha.
Kuharakisha kuleta mabadiliko na kuanza kufanya hivyo, panahitaji kukariri mara kwa mara, kwa kutouendea tena mwenendo huo mpaka uondoke na kumalizika kidogo kidogo. Na hapana budi ujipongeze wewe mwenyewe unapofanikiwa kuachana na mwenendo huo kwa wiki moja kwa mfano au wiki mbili, mpaka uuimarishe mwenendo huu mpya unaoufuata. Unairidhisha nafsi yako kwa kuufuata mwenendo huu, na zoezi hilo ndiko kupambana na nafsi. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na wanao fanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yupamoja na watu wema.} [AL ANKABUUT 69] Kwani kupambana na nafsi yake ni kitendo endelevu kwa ajili ya kazi maalumu mpaka uwe mwenendo uliotulizana katika utu wa mtu na kuubadilisha mwenendo huo sio kitu chepesi.
Na miongoni mwa njia hizo ni kujiepusha na marafiki wabaya; {Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa unataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usimtii tuliyemghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake yakawa yamepita mpaka.} [AL KAHF 28]
Na Mtume S.A.W., amesema katika yaliyopokelewa na Al Bukhariy na Muslim kutoka kwa Abi Musa kutoka kwa Mtume S.A.W.: amesema: "Hakika mambo yalivyo, mfano wa rafiki mzuri unayekaa naye na rafiki mbaya unayekaa naye, ni kama vile mbeba miski na mhuzi. Mbeba miski: ima akakunukisha harufu nzuri au ukainunua kutoka kwake, au ukapata harufu nzuri, na Mhunzi: ima akazichoma nguo zako au ukapata harufu mbaya."
Na miongoni mwa njia hizo ni kushughulisha wakati kwa mambo yanayofaa kama vile kusoma, kujifunza, na kufanya mazoezi ya mwili. Kwani nafsi yako kama hujaishughulisha kwa haki basi itakushughulisha kwa kilicho batili. Na miongoni mwa njia hizo ni kuviepuka vyakula vizuri vyenye virutubisho vyote na vyenye mafuta na viungo na pilipili, kwani kupunguza vyakula hivi hupunguza matamanio, lakini apunguze kwa kiasi ambacho atakuwa na uwezo wa kufanya kazi wala hapotezi kujisomea kwake, kwani uwastani katika kila jambo ni miongoni mwa sifa za Mtume S.A.W..
Na Miongoni mwa njia hizo ni kuzidisha kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu mpaka imtokee aina ya kumwogopa Mwenyezi Mungu, na akapata matunda moyoni mwake ya woga utakaopelekea kujiepusha na mazoea haya ya punyeto. Na katika njia zinazofaa zaidi na zilizo bora ni kuoa ambako Mtume S.A.W, ametuelekeza tufanye hivyo katika Hadithi ambayo ilipokelewa na Al Bukhariy na Muslim kutoka kwa Abdullahi Bin Masuod R.A., aliposema: Tulitoka pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., na sisi ni vijana hatuwezi kitu cho chote basi Mtume S.A.W. akasema: "Enyi vijana, mnapaswa kuwa na uwezo wa kuoa, kwani kufanya hivyo huyaepusha macho kuangalia, na huiifadhi tupu, na asiyeweza basi anatakiwa kufunga kwani kufunga kwake ni kinga".
Na Mtume S.A.W, alielekeza njia nyingine badala ya kutoweza, na hiyo ni kufunga Saumu, kwani hakika kufunga hupunguza nguvu iliyopo mwilini na mabayo inayachochea matamanio.
Na kutokana na hayo, na katika maudhui ya swali: Kwa hakika kujiepusha na punyeto ni jambo linalohitaji juhudi pevu, mpaka Mwenyezi Mungu akuepushe na mazoea haya yenye madhara kiafya.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas